Kuku wangu wengi wameugua ghafla msaada tafadhali.

Kuku wangu wengi wameugua ghafla msaada tafadhali.

Kideri hicho dogo; hukuwachanja ndo maana wameugua. Nakushauri uwauze wote upate hela ukaanze upya. Magonjwa mengine yanavumilika lakini kideri ni noma.

Acha kuropoka si kila mzungu ni padri na pasipo tafiti hutakiwi kusema.
 
Kama kuna sakafu kadeki kwa kwa sabuni ya detto; kama hujapiga sakafu jaribu kumwaga majivu kwa wingi walau siku 10 / 15 kabla ya kuingiza kuku wapya.

Tumia v- rid ni sumu ya kupulizia/kuoshea mabanda
 
kaka nasikitika nilichelewa kuiona thread yako huenda ningekusaidia kwani kuku wako nadhan hawakuwa na tatzo kubwa ila ukiwa na tatzo tena jaribu kuni pm maana mm ni zao la mifugo tengeru nadhan umenipata
 
Habari za Jamiiforums.

Kuku wangu wengi wameanza kuugua mafua, na kufa kwa haraka,
Sijui wamekula nini?
tangu tarehe 2/2/14 kila siku kwenye banda ninakuta kuku aliyekufa"

Msaada wa haraka Jf Banda halijamalizika!!

Jaribu kuwa na vitabu vinavyoonyesha magonjwa na Tiba zake mkuu kinaweza kukusaidia sana
 
mkuu pole sana
wa kwangu waliugua hivyo hivyo ila dawa za shop ziligonga mwamba nikawapa alovera na pilipili kichaa nilikuwa natwanga pamoja na kichanganya katika maji ya kunywa kwa muda wa siku tatu na kuna ambao walikuwa wanasinzia na kukohoa ila huwezi amini walipona wote...
_na sasa kila mara nataka niwape alovera kuna uzi nilisoma huku kuwa ni dawa nzuri
 
ndugu hapa si jukwaa la siasa kama kakosea ushauri,ni mwendo wa kumwelewesha tu na sisi tutafaidi pia

Kuna thread nilianzisha kichwa chake ni 'mtaalam wa mifugo uliza chochote utasaidiwa nadhan utapata majibu sahihi, samahan kama nimekukwaza ila hakuna siasa hapo ni ukweli mchungu.
 
mkuu pole sana
wa kwangu waliugua hivyo hivyo ila dawa za shop ziligonga mwamba nikawapa alovera na pilipili kichaa nilikuwa natwanga pamoja na kichanganya katika maji ya kunywa kwa muda wa siku tatu na kuna ambao walikuwa wanasinzia na kukohoa ila huwezi amini walipona wote...
_na sasa kila mara nataka niwape alovera kuna uzi nilisoma huku kuwa ni dawa nzuri

Ndugu usiendelee kubahatisha inaelekea wewe tatzo lako ulishindwa kugundua ugonjwa ukapewa dawa isio sahihi na kumbuka hakuna dawa inayotibu magonjwa yote.
Muhimu unapouguliwa toa maelezo kamili ya mgonjwa kwa mtaalam(si muuza dawa),awaone mtaalam au peleka VIC ilyo karibu nawe.
 
marire kumbuka hii thread ni ya mwezi wa 2 na jamaa kuku ameshauza.
 
Habari za Jamiiforums.

Kuku wangu wengi wameanza kuugua mafua, na kufa kwa haraka,
Sijui wamekula nini?
tangu tarehe 2/2/14 kila siku kwenye banda ninakuta kuku aliyekufa"

Msaada wa haraka Jf Banda halijamalizika!!

Ee bana samahani, nimechelewa kuiona. Dawa bora ni kuku 100- 1Kg ya vitunguu saumu-20ltr ya maji ya kunywa,
hawafi tena.
 
Ndugu usiendelee kubahatisha inaelekea wewe tatzo lako ulishindwa kugundua ugonjwa ukapewa dawa isio sahihi na kumbuka hakuna dawa inayotibu magonjwa yote.
Muhimu unapouguliwa toa maelezo kamili ya mgonjwa kwa mtaalam(si muuza dawa),awaone mtaalam au peleka VIC ilyo karibu nawe.

kwa hiyo we huamini dawa za asili?vijijini ndio wanazitumia hizi na mama ndio aliniambia
 
kwa hiyo we huamini dawa za asili?vijijini ndio wanazitumia hizi na mama ndio aliniambia

Si zote zinafanya kazi sahihi kumbuka wao walifanya hivyo kwavile hakukuwa na wataalam unachotakiwa sasa ni kushirikiana na wataalam hata hzo za asili wataalam wanazifaham kuna kitu kinaitwa ITK tuulize.
 
kaka nasikitika nilichelewa kuiona thread yako huenda ningekusaidia kwani kuku wako nadhan hawakuwa na tatzo kubwa ila ukiwa na tatzo tena jaribu kuni pm maana mm ni zao la mifugo tengeru nadhan umenipata

Kaka hizi thread tunasoma wengi na tunajifunza na kuelimika sana kupitia watu,hata kama umechelewa ila itakua ni vema ukaeleza ni nini kifanyike ili na sisi wafugaji wengine kama litatukuta tatizo kama hili tutafaham nini chakufanya.
 
Chukua jani la aloevera lipondeponde alafu changanya na maji uwape kila siku kwa siku tatu wanapona haraka sana
 
Back
Top Bottom