Uchaguzi 2020 Kukubalika kwa Rais Magufuli/CCM: Kishindo cha asilimia 99.9% ni mawingu tu ya dalili, mvua ni 2020, ni lele tu, ngoma ni 2020!

Uchaguzi 2020 Kukubalika kwa Rais Magufuli/CCM: Kishindo cha asilimia 99.9% ni mawingu tu ya dalili, mvua ni 2020, ni lele tu, ngoma ni 2020!

Ripoti mbalimbali za 'World happiness index' zinaonesha kuwa Tanzania ni moja ya nchi zinazoshika nafasi za juu sana kwa watu wake kutokuwa na furaha. Jibu la kwa nini hali inakuwa hivyo halijawahi kuelezwa kwa ufasaha. Leo tutatoa jibu la swali hilo

Asilimia kubwa ya watanzania ni wanafiki vibaya mno. Wanafiki wanaweza kuwa kama 90% hivi ya watu wote. Sasa hawa wote hawawezi kuwa na furaha kwa sababu dhamira, fikra, na matendo yao huwa yanapingana muda wote na ukishajikuta kwenye hali hiyo hakuna namna unaweza kuwa na furaha. Ikumbukwe furaha ni 'State of mind'

Kama 8% hivi wanaweza kuwa sio wanafiki lakini ni watu wasiokuwa na ujasiri wa kusimamia vitu wanavyoamini, kwa hiyo kwa kawaida hawa hawachukui hatua kwenye yale wanayoamini ili kusaidia kubadili hali ya mambo. Hawa husubiria wenzao wafanye vile watakavyofanya. Utasikia wakisema 'sasa kama wao hawajafanya sisi tutatafanya nini? ngoja tuonea kama watafanya". Hawa nao hawana wala hawawezi kuwa na furaha kwa sababu dhamira zinapingana na matendo.

Kama 2% hivi iliyobaki, hawa ni wa kweli, wana dhamira njema na wanasimamia wanayoamini ila nao hawafanikiwi maana ni wachache mno, ni kama tone kwenye bahari. Ijapokuwa hawafanikiwi, hawa angalau wana furaha maana Imani, dhamira na matendo yao yanaendana.Hapa ndio unawakuta kama kina ustadh na wengineo wachache, ustadh nani huyu wanamuita mwenye kigari kidogo dogo!?

Tunazo option mbili tu; Kuchagua kuwa wanafiki au kuwa wakweli, kuwajibika au kila mtu aache akiamini mwenzake ndio anawajibika. Chaguo lolote tunaloamua kufanya lina gharama na faida yake.

Hata hivyo mpaka sasa haifahamiki kwamba ni kwa nini asilimia kubwa ya watanzania wamekuwa wakichagua kuwa wanafiki kuliko wakweli na kuchagua kutokuwajibika badala ya kinyume chake licha ya chaguo hilo kuwa na gharama kuliko faida ikiwemo kutokuwa na furaha,.

Hakuna namna ambayo 'index' ya furaha inaweza kupanda kama hali ya unafiki itabaki kama ilivyo kwa sababu unafiki na furaha ni sawa na shetani na malaika mmoja akiingia mwezake lazima atoke.

Mwisho, maisha bila ya furaha ni maisha yasiyo na maana na hakuna namna unaweza ukawa na furaha kama unaendekeza unafiki au kutokuwajibika hata kama utakuwa na cheo au pesa au kitu kingine chochote kwa kiasi chochote kile.
 
Kwa mujibu wa kichwa cha habari uko sahihi kwa msemo wa Kiswahili. Kwamba kushinda kwa 99.9% ni mwanzo tu na ngoma kukamilika ni 2020 inaweza kuwa sawa kwa mitazamo miwili.

Moja: Kwamba figisu zilizofanyika 2019 zitaendelea 2020, Hii hakuna asiyeiwaza.

Pili: Kwamba haya yataendelea 2020 kwa maana ya kukubalika haswa. Hili linahitaji tafakuri. Natamani sana mamlaka zitambue na kuheshimu haki za wengine kushiriki katika uwanja ulio sawa.

Kwa bahati mbaya hili halipo. Kwa mantiki hii nalazimika kuamini kwamba ni kweli ushindi unaweza kuwa wa zaidi ya 99.9% lakini kwa hila na sio katika mazingira yanayotoa fursa sawa kwa wahusika wote. Wakati mwingine mtu anaweza akaonekana mwendawazimu au mkatili aliyepitiliza kiwango iwapo atapanga mashindano ya kupigana, akamchukua mpinzani wake akamfunga pingu za miguu na mikono, then akamtandika kisawa sawa kwa makonde halafu akajitangaza mshindi. Najaribu kuiangalia hii filamu kimawazo tu!
 
Kwanza toa tathmini na mwenendo mzima wa Uchaguzi ulivyokuwa toka kujiandikisha,uchukuaji na urejeshwaji na uteuzi kwa wagombea,kampeni ,kupiga kura na kuhesabu na kutangaza washindi.Baada ya hapo utapata jibu lake,mkuu tumia uzee wako kusema ukweli.Ccm oyeeee
 
Dharau zote hizi za Maccm kwa watanzania zinachangizwa na Chadema kuwa na Mwenyekiti goigoi,dhaifu anayefinywa mara moja, na kuufyata mkia. Nakumbuka enzi za Dr. Slaa mambo hayakuwa hivi. Kwa rafu iliyochezwa Jumapili iliyopita basi hakuna shaka Kingeeleweka.
#Bring our HECHE 4 strong opposition#
 
Pascal Mayalla akili zote uliziacha bungeni. Hivi uchaguzi ulikuwa huru na wa haki?
Hukuziona figisu?
Kwanza mateso anayo yapata Erick Kabendera wewe ndio chanzo.
Wasukuma Ni watu wabaya sana
ukiiaoma hii thread kwa jazba utaambulia moshi. tulia soma nukta kwa nukta.

Mayalla nakubatiza rasmi Popo; ni vigumu kujitanabahisha u mnyama au u ndege.

*Chonde: usinifikishe kwenye kamati ya familia yako kwa ubatizo huu[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
"sasa sijui kama kule kutopiga kura kuchagua nako ndiko kukubalika kwenyewe..."

Andiko lako lote Ukweli upo hapa .
kabisa nilikua natafuta kumjibu brother hapa kwa kusoma kwa makin sana lakin baada ya kukutana na hiyo line hapo juu, nikaona kama uzi umepiga U-turn moja kali sana.
nikubaliane tu na manengelo ambae alishawah sema somewhere kuwa Nyuzi za Paskali ukizisoma kwa umakini basi utakuta zimekaa kinyume nyume sanaaa
 
kabisa nilikua natafuta kumjibu brother hapa kwa kusoma kwa makin sana lakin baada ya kukutana na hiyo line hapo juu, nikaona kama uzi umepiga U-turn moja kali sana.
nikubaliane tu na manengelo ambae alishawah sema somewhere kuwa Nyuzi za Paskali ukizisoma kwa umakini basi utakuta zimekaa kinyume nyume sanaaa


Ajabu had watu wanafungua uzi kumuombea teuzi😉😉Magufuli sio mjinga alishamsoma Paskal zaman sana yaan!sema tumuombee Paskal aendelee kuishi!maana mijitu inajitia wazimu daily hapa nchini!
 
Ha ha Mayalla bana ,unatumia dola kuwafungia wenzako walifanya siasa,unawazuia wasifanye coverage kwenye media still unajisifia?

Hiyo kansa ni hatari kwa Taifa
 
Kuna mada zingine unasoma unaishia kucheka tu.


Nyuzi zote za Paskal huwa ni comedy tosha kwangu!..yaan huw namuimagine anavyoandika mwenyew lazima acheke!haka katabia nimekakopi kwenye maisha yangu n wanangu😅!sema mkubwa ameshaanza ng'amua!dah raha sana!
 
Paskali,
Mimi ni msomaji wa mabandiko yako hapa JF kwa muda mrefu.
Nakushauri,andika kidogo,kwa kina na kwa utaratibu mzuri.Ukiandika kila siku na kwa kila jambo unatupunguzia ile hamu ya kusoma makala zako.
 
Watu wanaoiendesha hii nchi wana akili finyu sana. Wanafanya uhuni kama huu kuzuia uchaguzi usifanyike huku wakijua fika kuwa nchi ikiwa blacklisted hawana any back up plan to counter the situation.

Mtu akishalewa madaraka anakuwa wa hovyo nafuu hata mlevi wa pombe. Mugabe naye alikuwa na akili finyu hivi hivi hadi alipoidumbukiza nchi yake kwenye korongo. Bure kabisa.
 
Nyuzi zote za Paskal huwa ni comedy tosha kwangu!..yaan huw namuimagine anavyoandika mwenyew lazima acheke!haka katabia nimekakopi kwenye maisha yangu n wanangu[emoji28]!sema mkubwa ameshaanza ng'amua!dah raha sana!
Utajapokea mkong'oto toka kwa shemeji siku moja!
We endelea kumletea Upaskali wako uone
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nnaona unaongea kama Polepole ,niseme tu hakuna mshindi wala alie shindwa ktk kilicho fanywa na CCM chini ya Mwamvuli wa inayoitwa Serikali.
Ni watu wachache wenye kuelewa falsafa ya MAYALA katika uandishi wake. Mara nyingi watu wanasoma kama wasomao hadithi bila kuchenjua kilichomo ndani ya mistari. Kwa kufanya hivyo mnazifikiria makala zake pamoja naye binafsi ndivyo sivyo!
 
Back
Top Bottom