Kukumbushia... wabongo jamani duh!

Kukumbushia... wabongo jamani duh!

Bahati mbaya ni kwamba mimi nikishatapika huwa siwezi kumeza tena matapishi, hivyo suala la kukumbushia kwangu huwa halina nafasi kamwe.
 
kama watu wameachana lakini bado wanapendana dah hapo inakua issue... kwa sababu one day lazima ex akuibie mpenzi wako...tena wengine wanasemaga unanitunzia...kwamba wewe mlipie gharama zote lakini mi nikija nachukua jumla jumla... kuna watu wanakumbushia mpaka ile siku ya harusi...yaani bibi harusi yuko salon anatengenezwa, bwana harusi mtarajiwa yuko na ex wanakumbushiana...ni nomaaa!!
 
Kupasha kiporo muhimu!...hasa ukikuta kile kilchoungwa kwa karanga weweee!utasahau chakula fresh kwa muda huo!
 
woman_cheating2.jpg


Kweli wabongo tuna vituko vyetu wenyewe na tunawezana wenyewe. Mtu alikuwa amesafiri tena baada ya kuachana na mlijua hakuna uhusiano. Anarudi toka safari siku mbili tatu anampigia 'demu wake wa zamani'. Maneno ya hapa na pale mwisho anachomboza kuwa anataka kuwa naye kimapenzi. Msichana anang'aka jamaa anadai "lazima tukumbushie". Maneno mawili matatu msichana naye kakubali - alikuwa na mchumba! - akatafuta kisingizio wakaenda kwenye moja ya hoteli fulani na kweli 'wakakakumbushia" hadi vilivyokumbukwa vilipotazamana vikakonyezana!

Niliposikia hili nikawauliza jamaa zangu wa hapa na pale na wakasema ati ni 'kanuni' kuwa kama mliachana vizuri huku bado mkiwa na mapenzi mnapeana haki ya 'kukumbushia' mahali popote, wakati wowote na haijalishi kama mna mahusiano, mko kwenye ndoa na watu wengine au la. Kwamba haki ya "kukumbushia" ni mojawapo ya 'haki za msingi' za watu waliowahi kupendana.


Lakini kilichonichekesha kwenye kisa kingine ni kuwa jamaa alikuwa ameachana vibaya sana na msichana wake, tena ile ya kuachana na kumsema vibaya kwa watu wengi. Miaka ikapita jamaa akajikuta hana mtu na usiku mmoja akiwa amezidiwa baada ya kujikuta hana pa kwenda akampigia msichana yule simu ati ohh "tukumbushie"! Nasikia msichana aliporomosha matusi yaliyofuatana kama mabehewa ya treni hadi hadi kioo cha simu kikayeyuka!

Lakini wanaokumbushia wengine vibaya ni wasichana ambao wanaamini walikuwa ni 'the best' kwa yule mwanamme kiasi kwamba wamejipa haki kuwa wakionana tu yule mwanamme lazima alainike. Na ni kweli msichana mmoja aliyesikia mtu wake wa zamani anaoa aliapa kuwa hawezi kumuacha kwani huyo mwanamme alimuweka yeye moyoni na hakuna wa kuweza 'kumreplace". Kama utani baada ya harusi binti kajipeleka ofisini kwa jamaa! Well..... waliishia kwenda kukumbushia Zanzibar!!

Huku kukumbushia kuna faida zaidi au kuna hasara zaidi? NI mambo gani ya kuzingatia mtu au watu wanapoamua kukumbushia? Je katika kukumbushia ina maana mtu hajaridhika mapenzi ya sasa au bado anatamani 'vilivyopita'.

Hapo kwenye Nyekundu umenikumbusha mambo ya Mwanameka na Musa!aliposikia Musa ameoa!
 
Kupasha kiporo muhimu!...hasa ukikuta kile kilchoungwa kwa karanga weweee!utasahau chakula fresh kwa muda huo!
 
kukumbushia kutamu sana,tena haina gharama wala usumbufu!wanaume wanaamini ukisha mchojoa mwanamke hana ujanja tena
 
Mnaweza kufikiri kwamba mtaishia kukumbushia badala yake mka- restore kabisa. Hapo ndipo inapokuwa balaa!
 
Ndio maana huwa simshauri Kijana amuoe mwanamke ambaye ameshazaa na Mwanaume mwingine na huyo Mwanaume bado yuko hai. hili ni sehemu ya tatizo.
 
Mnaweza kufikiri kwamba mtaishia kukumbushia badala yake mka- restore kabisa. Hapo ndipo inapokuwa balaa!

Hii hutokea pale mmoja anapokuwa hana mahusiano ya kudumu huko aloko ndio mnaweza restore
Ila kama kaoa au kaolewa mrestore vipi, tena hii ya kukumbushia imenifanya nikaelewa ila dhana ya 'No Strings Attached'
Ni aina hiyo ya mahusiano

Ndio maana huwa simshauri Kijana amuoe mwanamke ambaye ameshazaa na Mwanaume mwingine na huyo Mwanaume bado yuko hai. hili ni sehemu ya tatizo.

On point, on point! Hasa kama awe alipenda ana akapenda, imekula kwako kwa kweli
 
Kiporo hakipikwi eeeh huwa tunapasha tu na kula na mtalaka hatongozwi
 
Ha ha ha ha, Mbu, mbona unataka kuwa bad boy?

Yaani unaniunganisha na huyu nikiwa nakonfesi mambo ya kukumbushia?
Anyway, huwa hamchunguzi kuku ndio bahati yangu lol
The Boss, sio kweli natania tu 🙂

The Boss toa ushuhuda bana, maana kisha mtu hataki kuungama humu akati haya matendo yanafanyika daily...
angalau Kongosho kaweka ushuhuda wake mezani..
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: Mbu
umalaya mtupu.... kukumbushia kitu gani?...uzinzi tu hakuna lolote


nilijua tu darling utakosekana mitaa hii . achana na hawa watu hny ni kiu zisizokatika ndio zinawasumbua , napenda ushauri wako beibii. karibu ntatangaza nia
 
Koh koh ..........nauliza tu hii kumbushia hiii.......... ukiwa huna mtu je wa kupasha kiporo (mwe naiga misemo ya Kongosho) unaruhusiwa kukubali kukumbushia au lah? Maana kama ukiwa tayari na mtu mwingine then wafuatwa eti mtu anataka kukumbushia nawe wamkubalia naona kama haijakaa sawa vile!
 
Back
Top Bottom