Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Vipi wako akienda kukumbushia?
![]()
Kweli wabongo tuna vituko vyetu wenyewe na tunawezana wenyewe. Mtu alikuwa amesafiri tena baada ya kuachana na mlijua hakuna uhusiano. Anarudi toka safari siku mbili tatu anampigia 'demu wake wa zamani'. Maneno ya hapa na pale mwisho anachomboza kuwa anataka kuwa naye kimapenzi. Msichana anang'aka jamaa anadai "lazima tukumbushie". Maneno mawili matatu msichana naye kakubali - alikuwa na mchumba! - akatafuta kisingizio wakaenda kwenye moja ya hoteli fulani na kweli 'wakakakumbushia" hadi vilivyokumbukwa vilipotazamana vikakonyezana!
Niliposikia hili nikawauliza jamaa zangu wa hapa na pale na wakasema ati ni 'kanuni' kuwa kama mliachana vizuri huku bado mkiwa na mapenzi mnapeana haki ya 'kukumbushia' mahali popote, wakati wowote na haijalishi kama mna mahusiano, mko kwenye ndoa na watu wengine au la. Kwamba haki ya "kukumbushia" ni mojawapo ya 'haki za msingi' za watu waliowahi kupendana.
Lakini kilichonichekesha kwenye kisa kingine ni kuwa jamaa alikuwa ameachana vibaya sana na msichana wake, tena ile ya kuachana na kumsema vibaya kwa watu wengi. Miaka ikapita jamaa akajikuta hana mtu na usiku mmoja akiwa amezidiwa baada ya kujikuta hana pa kwenda akampigia msichana yule simu ati ohh "tukumbushie"! Nasikia msichana aliporomosha matusi yaliyofuatana kama mabehewa ya treni hadi hadi kioo cha simu kikayeyuka!
Lakini wanaokumbushia wengine vibaya ni wasichana ambao wanaamini walikuwa ni 'the best' kwa yule mwanamme kiasi kwamba wamejipa haki kuwa wakionana tu yule mwanamme lazima alainike. Na ni kweli msichana mmoja aliyesikia mtu wake wa zamani anaoa aliapa kuwa hawezi kumuacha kwani huyo mwanamme alimuweka yeye moyoni na hakuna wa kuweza 'kumreplace". Kama utani baada ya harusi binti kajipeleka ofisini kwa jamaa! Well..... waliishia kwenda kukumbushia Zanzibar!!
Huku kukumbushia kuna faida zaidi au kuna hasara zaidi? NI mambo gani ya kuzingatia mtu au watu wanapoamua kukumbushia? Je katika kukumbushia ina maana mtu hajaridhika mapenzi ya sasa au bado anatamani 'vilivyopita'.
Chezeiya kiporo wewe, afu hakuna taabu ya kuanzan kusomana sijui nifanye hivi au vile.
Mnajuana na mnapiga mechi la kirafiki swaaafi.
Kongosho mumeo akisikia unalo...
Mnaweza kufikiri kwamba mtaishia kukumbushia badala yake mka- restore kabisa. Hapo ndipo inapokuwa balaa!
Ndio maana huwa simshauri Kijana amuoe mwanamke ambaye ameshazaa na Mwanaume mwingine na huyo Mwanaume bado yuko hai. hili ni sehemu ya tatizo.
This is a new revelation to me...kwahiyo haya mambo yanafanyika sana basi.
umalaya mtupu.... kukumbushia kitu gani?...uzinzi tu hakuna lolote
umalaya mtupu.... kukumbushia kitu gani?...uzinzi tu hakuna lolote