Parabolic
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 2,922
- 3,252
Wakati viongozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Rwanda wakikutana nchini Qatar kwa ajili ya mazungumzo ya kusitisha vita, waasi wa M23 wamegomea mkutano mwingine wa usuluhishi uliokuwa ufanyike nchini Angola.
Viongozi hao, Rais wa DRC, Felix Tshisekedi na Rais wa Rwanda, Paul Kagame, wamefanya mazungumzo ya ana kwa ana kwa mara ya kwanza tangu waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda walipoteka miji mikubwa miwili Mashariki mwa DRC ukiwamo wa Goma na kisha Bukavu mwezi Februari.
Tangu wakati huo, yalifanyika mazungumzo ya kutafuta Amani yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam, ambapo Rais Tshisekedi alimtuma Waziri Mkuu wake, Judith Suminwa kumwakilisha.
Hata kwenye mkutano wa Umoja wa Afrika uliofanyikia Addid Ababa nchini Ethiopia Februari 15, Rais Tshisekedi alimtuma Waziri Mkuu Suminwa, huku mwenyewe akienda nchini Ujerumani kulikuwa na mkutano wa usalama ulioandaliwa na Jumuiya ya Ulaya.
Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa na Qatar, ambayo emir wake aliendesha mazungumzo hayo mjini Doha, viongozi hao walitaka usitishaji mapigano wa haraka Mashariki mwa DRC.
"Marais walikubaliana kuhusu umuhimu wa kuendeleza mazungumzo yaliyoanzishwa Doha ili kuweka msingi imara wa amani ya kudumu," ilisema taarifa hiyo iliyonukuliwa na Aljazeera news.
DRC inaituhumu Rwanda kwa kutuma silaha na wanajeshi kusaidia waasi wa M23, madai ambayo Rwanda imekana.
Rais Kagame anakabiliwa na shinikizo kubwa kutoka nchi za Ulaya na Marekani, baada ya nchi hizo kumwekea vikwazo.
Mwanzoni mwa wiki hii Ubeligiji ilivunja uhusiano wake wa kidipolomasia na Rwanda kutokana na mzozo huo.
M23 ni moja kati ya makundi takriban 100 yenye silaha yanayopigania udhibiti wa maeneo yenye utajiri wa madini Mashariki mwa DRC, karibu na mpaka wa Rwanda.
Mgogoro huu umezalisha moja ya mizozo mikubwa ya kibinadamu duniani, huku zaidi ya watu milioni saba wakiwa wamepoteza makazi yao.
Kulingana na ripoti za wataalamu wa Umoja wa Mataifa, waasi hao wanaungwa mkono na wanajeshi wa Rwanda wapatao 4,000.
M23 waeleza sababu ya kugomea mazungumzo
Mazungumzo ya amani yaliyopaswa kufanyika Jumanne Machi 18 kwa lengo la kutafuta suluhu kwa mzozo huo yamekwama baada ya kundi la waasi la M23 kujiondoa.
M23 imeeleza sababu ya kususia mazungumzo hayo kuwa ni kutokana na vikwazo vya Umoja wa Ulaya dhidi ya baadhi ya viongozi wa kundi hilo, akiwemo kiongozi wao Bertrand Bisimwa.
Katika taarifa yake iliyonukuliwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), M23 imesema kuwa vikwazo hivyo "vinahatarisha mazungumzo ya moja kwa moja na kuzuia maendeleo yoyote."
Umoja wa Ulaya pia uliwawekea vikwazo makamanda watatu wa jeshi la Rwanda pamoja na mkuu wa wakala wa madini wa nchi hiyo kwa tuhuma za kusaidia waasi wa M23.
Uamuzi huo unazua maswali kuhusu hatima ya mazungumzo, mustakabali wa usalama mashariki mwa DRC, na hatua zitakazochukuliwa na pande husika ili kudhibiti hali ya mambo na mzozo unaoendelea DRC.
Pamoja na kujiondoa kwa M23, Serikali ya DRC imesema kuwa itaendelea na mazungumzo na makundi mengine ya waasi.
Juhudi hizo zinaungwa mkono na Umoja wa Mataifa (UN), Umoja wa Afrika (AU), na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), ambazo zinaamini kuwa mazungumzo ni njia bora ya kupata suluhu ya kudumu kwa mgogoro huu.
Wakati M23 wakisusia, ujumbe unaoiwakilisha DRC ulifika Luanda tayari kwa mazungumzo, ambapo msemaji wa Rais wa DRC Felix Tshisekedi ameliambia shirika la habari la AP na kunukuliwa na Aljazeera, kwamba wenyewe watashiriki mazungumzo.
Kujiondoa huko kwa M23 kunayaweka njia panda mazungumzo hayo ya kutafuta suluhu, kwani ndilo kundi lenye nguvu zaidi kijeshi miongoni mwa makundi ya waasi mashariki mwa DRC, hivyo hata kama makubaliano yatapatikana na makundi mengine, bado hali ya usalama haitaimarika kikamilifu.