King snr
JF-Expert Member
- May 25, 2015
- 1,165
- 1,470
Habari wakuu,
Hongereni kwa majukumu ya hapa na pale nimekuja kwenu kupata mawazo na ushauri hasa katika kukuza mtaji.
Biashara yangu Ni uuzaji wa laptop, desktop and accessories.
Nilianza biashara hii mtandaoni kwa kuwa napost bidhaa ambazo sina mteja akihitaji naenda kumchukulia changamoto ya hii biashara Ni kuaminiwa na watu maana wengi wameshapigwa Sana online Sasa inapelekea kupoteza wateja wengi.
Nilijitahidi nikafanikiwa kupata frem na Sasa kidogo wateja wanaweza kufika dukani na kuangalia mzigo.
Changamoto ninayopata saizi sio changamoto mbaya Sana maana Nina wateja wengi lakini wakija dukani hawakuti bidhaa za kutosha na hii Ni kutokana na kukosa mtaji wa kuwa na pc zangu mwenyewe hapa dukani wengine wanataka wakija dukani wachukue mzigo waondoke nao na sio stori za kuwaambia lipia hii nakuagizia.
Natamani nipate japo kiasi Cha 10M nichukue mzigo biashara ichangamke maana wateja Nina uhakika ninao wa kutosha,branding na marketing zote ziko vizuri.
Nawasilisha kwenu Kama Kuna ambaye anaweza kunishauri kwa chochote.
Karibu.