Naona malumbano haya ya wa JF siamini, inamaana CCM wana paraganisha vyama vya upinzani ili wa monopolize siasa ya bongo, sasa wamefanikiwa kuingilia ngome ya wana JF, hii ni hatari.
Mi nadhani kuanzisha kwa internet journalism, na the so called blogging ni kuwapa fursa watu wa kila aina fursa ya kujadili machungu yao, kukosoa, kukemea kurekebisha na kufundisha bila kuenda shule ya uandishi. Sasa kuanza kwa wana JF kulumbana eti fulani hajui kuandika nikuwafungia madirisha watanzania wengi tu ambao wanaweza kuchangia au kufaidika na michango ya humu JF. Ni bora tujaribu kuwaelewa, mjaribu kunielewa ninachotaka kueleza, mnisaidie nikikosea badala ya kuniponda na kunidhalilisha. Au alternative nyingine ni, ziwekwe criteria za kuwemo humu JF, pengine hii ni forum ya waandishi na wasomi tu. Tuwekeni wazi jamani.