Kula kuku wa kisasa si salama kwa afya

Kula kuku wa kisasa si salama kwa afya

hazole1

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2015
Posts
4,319
Reaction score
3,916
Kuna siku nilikula kuku wa kisasa ilikua jioni, asubuhi nikajikuta nimetoka na viupele kama vya kuku baada siku tatu nikaenda kupima wakaniambia nina fangasi, kwa akili ya haraka haraka kuna wazo likanijia nikahisi kuku wa kisasa huwa wanalishwa fangasi ili wakue kwa haraka kwa sababu kuku wa kisasa wanalishwa vitu vingi sana ambavyo hata vingine huwezi kuvijua na siku zote mfanya biashara anaangalia faida tu.
Na haitakuka kutokea mfanya biashara akaijali afya yako wewe ila swala la kulinda afya yako ni jukumu lako mwenyewe hasa kwa vitu ambavyo unaweza kuviepuka.
 
una matatizo yako tu mkuu,kapime kipimo kikubwa inawezekana una MIWAYA sio fungus wa kuku aliyeikwa au kukaangwa
 
pale unapogundua wahehe wanapiga vita ulaji wa kuku ili nafasi yake apatiwe mbwa

au mhehe anapoonesha mahaba kwa chakula anachokipenda

au unapogundua mhehe amefuga mbwa na wateja wamepungua

eti unaagiza nipatie chips mbwa aisee hebu nenda china
 
Mkuu huyo kuku hafai hata kidogo ni sumu inayoua taratibu. Lkn kwa story yako waone madaktari asijekuwa kichaka cha matatizo yako.
 
inawezekana... maana siku moja nilipita kigambon nikakuta paja limefungwa juu ikabid niulize kabla ya kununua kuwa ile ni nyama ya mbuzi au kondoo maana ilikuwa nyeupe, duuu? si wakaniambia lile ni paja la kuku
 
Kuna siku nilikula kuku wa kisasa ilikua jioni asubuhi nikajikuta nimetoka na viupele kama vya kuku baada siku tatu nikaenda kupima wakaniambia ninafangasi kwa akili ya haraka haraka kuna wazo likanijia nikahisi kuku wakisasa huwa wanalishwa fangasi ili wakue kwa haraka kwasaababu kuku wa kisasa wanalishwa vitu vingi sana ambavyo hata vingine huwezi kuvijua na siku zote mfanya biashara anaangalia faida tu.

Duu wewe ni muongo, utakuwa una tatizo wewe mwenyewe fangasi ni ugonjwa wa kawaida tu hautokani na kuku labda ungesema una aleji na kuku wa kisasa.
 
Kuna jamaa namfahamu sana kaaza kuota matiti kwa sbb ya kuku hawa wa kisasa.
 
Acha kutisha watu.....ulikula mbovu si kuku wa kisasa wote
 
Hata ukila samaki unaweza kutoka vipele......

Nenda hospitali kwa vipimo zaidi usisingizie kuku
 
kuna siku nilikula kuku wa kisasa ilikua jioni asubuhi nikajikuta nimetoka na viupele kama vya kuku baada siku tatu nikaenda kupima wakaniambia ninafangasi kwa akili ya haraka haraka kuna wazo likanijia nikahisi kuku wakisasa huwa wanalishwa fangasi ili wakue kwa haraka kwasaababu kuku wa kisasa wanalishwa vitu vingi sana ambavyo hata vingine huwezi kuvijua na siku zote mfanya biashara anaangalia faida tu.

baada ya kula huyo kuku , ulikunywa nini kama kitelemshio, usije kuwa ulikunywa kangala isiyopimwa ,ukasingizia kuku wa kisasa.
 
Back
Top Bottom