ERoni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2013
- 48,052
- 104,677
Hello wakuu,
Kuna kitu nimekiona, kipo na mara nyingi najiwazia nakuwa na wasiwasi juu ya afya zetu kama jamii. Hii tabia ya kula kila mahali, mazingira yoyote bila kujua namna chakula kilivyoandaliwa.
Ukipita kwenye mikusanyiko na sehemu zilizochangamka utakuta meza zimewekwa, kuna kila aina ya vyakula, vyakula vya haraka mnaita take away kuanzia chips, ndizi hadi bites kama maandazi, kachori na juice za kutengeneza majumbani.
Najiwazia tu na kuona kabisa hakuna regulations kwenye hivi vyakula, sidhani kama upo usimamizi wowote na hili linanipa wasiwasi hasa ukiangalia namna jamii ilivyoharibika. Unakulaje sambusa mtu anatembeza barabarani? Unamjua huyo mtu, unajua ni nyama gani ameandaa, unajua mazingira aliyopika hizo sambusa? Maswali ni mengi, binafsi nikiona mtu busy ananunua mapaja ya kuku wanaotembezwa na anajilia kwa raha zake namuwazia mengi.
Siku hizi kuna serial killers, mtu anaweza kuamua tu kuua watu kwa namna anavyotaka, iwe kuweka sumu kwenye chakula au vyovyote vile na kwa namna wanavyouza, ni ngumu kujua nani alifanya hilo tukio. Huwa nikishuka pale mbezi mwisho na kuona watu wanavyokula kachori, supu ya pweza nk najisemea moyoni kweli nchi bado imejaa ujamaa.
Tujihadhari sana hasa kula vyakula ambavyo hatujui mazingira yake ya maandalizi.