Kula ovyo kutakuja kutuathiri sana siku moja

Hahaha tunakula tu matumbo ya wabongo ya TBS, sema ukipata hela kidogo unaanza kugoogle madhara ya kula ugali haha
 
huku mbeya kuna kipindupindu sasa hivi

mbeya ndo kuna hili tatizo sana, usafi wa vyakula sio mzuri

na watu wanaoendekeza hizi tabia wanapata uzito uliokithiri
 
Matumbo yana TBS! kwa hiyo masikini hawajali chochote ili mradi matumbo yao yajae? Mimi masikini na nipo makini sana ninachokula mkuu.
 
Kwa kweli mauwaji ya aina hii hayapo hata haya ya mafuta ya Mangi nafikiri yametengenezwa tu ila sidhani kama waliotengeneza waliamua kuuwa watu
Kuhusu vyakula vya mitaani kwa kweli watu wanakula vingi vibaya na vizuri pia
Wengine wanauza kuku walionyongwa kwenye vibanda na vibaka na muuzaji huwezi kudhani ananunua mizoga na kuuza ila maisha yanaenda

Jamani binadamu tunauwezo wa kuvumilia njaa kama wanyama na ndege
Kwani nao kuna masiku huwa hawapati hata mlo mmoja
Ushauri muwe mnafunga hata siku mbili kwa wiki ni afya kwetu

Mimi sili mazagazaga hayo ya mitaani napika mwenyewe labda Nuts tu au mahindi
 
huku mbeya kuna kipindupindu sasa hivi

mbeya ndo kuna hili tatizo sana, usafi wa vyakula sio mzuri

na watu wanaoendekeza hizi tabia wanapata uzito uliokithiri
Mkuu,
Karne hii kutaja kipindupindu ni aibu tu. Kwamba watu wa Mbeya wamekuwa wachafu wa mazingira na uandaaji wa chakula ndoo maana wamefikia huko, sehemu yenye hali ya hewa nzuri na maji ya kutosha kukumbwa na hiyo pandemic ni aibu
 
Huwa nawaangaliaa wale wanaokula "MAKWASUKWASU aka NGOZI ya Ng'ombe" tena wanchomea zile wavu ndogo rangi rangi ili nyama isikimbie down chini 😄😄😄

Kuna jamaa nilimuona asubuhi na mapema huwa napita kila siku huwa anaunguza rangi zile square box wire, alioniona namuangalia ikanibidi aniambie mambo vip bro nikamjibu freshi tu huku napiga hatua 😅😅😅, na walaji wenyewe hawajui ule waya kautoa wapi maana mwamba saa kumi na mbili unusu hivii anaunguza waya for "bbq" 😅😅😅 balaa wakuu.
 
KULAKULA HOVYO NI KUBAYA MNO yapaswa kuchukua tahadhari kubwa hasa katika mazingira haya-:
1.Maofisini,
2.Sehemu ambapo umezoeleka sana,
3..Kwenye miradi ambapo wewe ni msimamizi au boss,
4.Kwa majirani na hasa kwenye "sherehe mswahili"
 
Hili ni janga kuu nchi nzima, ni kama watu wameamua kujitoa mhanga afya zao , Hili tatizo linachangiwa pia na umasikini uliokithiri kwa jamii nyingi za kitanzania.Wengi wanakula wanachokipata bila kujali usalama wake na sio wanachopenda/mudu
 
Unaweza kula mapaja ya kuku yanatembezwa na mtu hata humjui? Najua kifo kipo na tunatembea nacho ila muhimu kuchukua tahadhari, huwezi kuvuka barabara kizembe eti kwa vile kifo kipo na tunatembea nacho.
Kwa sasa siwezi kula kwa sababu nina uwezo wa kwenda sehemu nzuri nikakaa nikaagiza nikala.

Ila kipindi bado nimekula sana vitu vya kutembezwa hadi sambusa, kuku hao, mayai ya kuchemsha, zile keki wanazikata kata wanaweka kwenye deli, yaani kwa kifupi nimekula hadi maandazi ya kununua sokoni ambayo mtu anakaangia kwake anakuja kuuza sokoni, viperege vile.

Mbona tunakula tu mkuu na tupo fresh tu. Ujue ukiwa na hofu na kitu ni rahisi kukudhuru kuliko pale ambapo hautakitilia hofu.
 
Mkuu una roho mbaya mno, sasa hizi sambusa zangu hapa kariakoo nani atanunua watu wakisoma huu uzi wako?
Weka mazingira mazuri ya uandaaji wa sambusa zako mkuu, hatutaki kula vibudu na nyama za mbwa🤣
 
Kwa sasa siwezi kula kwa sababu nina uwezo wa kwenda sehemu nzuri nikakaa nikaagiza nikala.

Ila kipindi bado nimekula sana vitu vya kutembezwa hadi sambusa, kuku hao, mayai ya kuchemsha, zile keki wanazikata kata wanaweka kwenye deli, yaani kwa kifupi nimekula hadi maandazi ya kununua sokoni ambayo mtu anakaangia kwake anakuja kuuza sokoni, viperege vile.

Mbona tunakula tu mkuu na tupo fresh tu. Ujue ukiwa na hofu na kitu ni rahisi kukudhuru kuliko pale ambapo hautakitilia hofu.
Duh, mkuu muhimu kuangalia kinachoingia mdomoni aisee, na wala sio lazima mtu uwe na uwezo ndio ule vyakula visafi, ni maamuzi tu kuwa either utapika mwenyewe au utakula sehemu zenye maandalizi mazuri. Tunategemea teachers kama nyie ndio mfundishe watu hygiene, wewe ndio unapromote tena🤣🤣
 
Hello wakuu,
Kuna kitu nimekiona, kipo na mara nyingi najiwazia nakuwa na wasiwasi juu ya afya zetu kama jamii. Hii tabia ya kula kila mahali, mazingira yoyote bila kujua namna chakula kilivyoandaliwa.

Ukipita kwenye mikusanyiko na sehemu zilizochangamka utakuta meza zimewekwa, kuna kila aina ya vyakula, vyakula vya haraka mnaita take away kuanzia chips, ndizi hadi bites kama maandazi, kachori na juice za kutengeneza majumbani.

Najiwazia tu na kuona kabisa hakuna regulations kwenye hivi vyakula, sidhani kama upo usimamizi wowote na hili linanipa wasiwasi hasa ukiangalia namna jamii ilivyoharibika. Unakulaje sambusa mtu anatembeza barabarani? Unamjua huyo mtu, unajua ni nyama gani ameandaa, unajua mazingira aliyopika hizo sambusa? Maswali ni mengi, binafsi nikiona mtu busy ananunua mapaja ya kuku wanaotembezwa na anajilia kwa raha zake namuwazia mengi.

Siku hizi kuna serial killers, mtu anaweza kuamua tu kuua watu kwa namna anavyotaka, iwe kuweka sumu kwenye chakula au vyovyote vile na kwa namna wanavyouza, ni ngumu kujua nani alifanya hilo tukio. Huwa nikishuka pale mbezi mwisho na kuona watu wanavyokula kachori, supu ya pweza nk najisemea moyoni kweli nchi bado imejaa ujamaa.

Tujihadhari sana hasa kula vyakula ambavyo hatujui mazingira yake ya maandalizi.

Umeongea kitu kizuri sana ,kuna watu yaani sijui hawajielewi anakutana na mtu anauza juice kaweka kwenye vikopo yeye twende.

Leo nimesikia kuna watu wamepata madhara ya sumu kwa kula chapati na vitumbua vilivyokaangwa kwenye mafuta ambayo wana wasiwasi yalikuwa na sumu.
 
Duh, mkuu muhimu kuangalia kinachoingia mdomoni aisee, na wala sio lazima mtu uwe na uwezo ndio ule vyakula visafi, ni maamuzi tu kuwa either utapika mwenyewe au utakula sehemu zenye maandalizi mazuri. Tunategemea teachers kama nyie ndio mfundishe watu hygiene, wewe ndio unapromote tena🤣🤣
Mkuu uwezo ndio unaamua mtu ale sehemu za hovyo au za hadhi. Wewe hauoni watu wananunua hadi maji yaliyofungwa kwenye vimifuko wanakunywa? Jero tu ya kununua chupa ya maji mtu hana, ndio buku jero ya kuagiza wali kwa mama ntilie?
 
Kwa kweli mauwaji ya aina hii hayapo hata haya ya mafuta ya Mangi nafikiri yametengenezwa tu ila sidhani kama waliotengeneza waliamua kuuwa watu
Kuhusu vyakula vya mitaani kwa kweli watu wanakula vingi vibaya na vizuri pia
Wengine wanauza kuku walionyongwa kwenye vibanda na vibaka na muuzaji huwezi kudhani ananunua mizoga na kuuza ila maisha yanaenda

Jamani binadamu tunauwezo wa kuvumilia njaa kama wanyama na ndege
Kwani nao kuna masiku huwa hawapati hata mlo mmoja
Ushauri muwe mnafunga hata siku mbili kwa wiki ni afya kwetu

Mimi sili mazagazaga hayo ya mitaani napika mwenyewe labda Nuts tu au mahindi
Hayapo ila dunia inaenda kasi sana, wale jamaa wanaopiga risasi kwenye madarasa, mitaani soon wanaingia Afrika, just from nowhere mtu anaamua kuuwa watoto wadogo mashuleni, unadhani hayawezi kufika bongo?
 
Kuangalia sana mitandao ya kijamii kunafundisha mengi mabaya na mazuri pia
Watoto wadogo kuachiwa simu na kuperuzi kila wakati ndio sababu kubwa
Wanajifunza mabaya mengi na wanahoji mengi
Hao wanaouwa wamejifunza humu na sehemu kama USA ambapo mtu anaweza kuwa na kila aina za bunduki kwake yaani jeshi la mtu mmoja sasa hapo mtoto anazinguliwa shule anaamua kwenda kuwamaliza watu
Kama tutaendelea kuwa na maadili yetu basi madhara sio mengi kwetu

Angalia zamani majambazi walikuwa hawauwi kwa silaha bali wanaiba na kukimbia ila baada ya kuwapa hifadhi wakimbizi ndio wengi wakaingia na silaha na kuanza kuteka Mabasi na kuuwa
Ila mwamba alipoingia aliwalaza wengi na kufa wengine walikimbia nchi na tukawa na amani

Tuombe amani na kulea watoto wawe na tabia njema
Kwa mfano mwaka huu kuna baadhi ya nchi wameweka misimamo kwenye mitandao
Australia ni marufuku sasa mtoto chini ya miaka 16 kuperuzi mitandaoni ila sijui itafanyaje kazi
 
Hello wakuu,
Kuna kitu nimekiona, kipo na mara nyingi najiwazia nakuwa na wasiwasi juu ya afya zetu kama jamii. Hii tabia ya kula kila mahali, mazingira yoyote bila kujua namna chakula kilivyoandaliwa.

Ukipita kwenye mikusanyiko na sehemu zilizochangamka utakuta meza zimewekwa, kuna kila aina ya vyakula, vyakula vya haraka mnaita take away kuanzia chips, ndizi hadi bites kama maandazi, kachori na juice za kutengeneza majumbani.

Najiwazia tu na kuona kabisa hakuna regulations kwenye hivi vyakula, sidhani kama upo usimamizi wowote na hili linanipa wasiwasi hasa ukiangalia namna jamii ilivyoharibika. Unakulaje sambusa mtu anatembeza barabarani? Unamjua huyo mtu, unajua ni nyama gani ameandaa, unajua mazingira aliyopika hizo sambusa? Maswali ni mengi, binafsi nikiona mtu busy ananunua mapaja ya kuku wanaotembezwa na anajilia kwa raha zake namuwazia mengi.

Siku hizi kuna serial killers, mtu anaweza kuamua tu kuua watu kwa namna anavyotaka, iwe kuweka sumu kwenye chakula au vyovyote vile na kwa namna wanavyouza, ni ngumu kujua nani alifanya hilo tukio. Huwa nikishuka pale mbezi mwisho na kuona watu wanavyokula kachori, supu ya pweza nk najisemea moyoni kweli nchi bado imejaa ujamaa.

Tujihadhari sana hasa kula vyakula ambavyo hatujui mazingira yake ya maandalizi.
Sidhani kama kuna anayependa kula vitu vilivyoandaliwa kwenye mazingira ya hovyo ila umasikini ndio tatizo. Mfano mtu ameshinda njaa kutwa nzima hata chai hajanywa jioni apewe offer ya chipsi za stend au kachori halafu akatae aseme hii imeandaliwa kwenye mazingira machafu. Inawezekana? Na uwezo wa kununua chakula hoteli ya kifahari hana. Je afanyeje? Tena mwingine unakuta ni homeless
 
Nakubaliana sana na wewe! Huwa najiskia vibaya zaidi pale ambapo mzazi ananunua na kumpa na mtoto. Hakuna kujali wala nini...halafu tunapambana mpaka leo kama nchi na utapiamlo..sa zingine ni hivi vitu watoto wanapewa , minyoo tele..afya inatokea wapi hapo.
 
Back
Top Bottom