Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Matumbo yana TBS! kwa hiyo masikini hawajali chochote ili mradi matumbo yao yajae? Mimi masikini na nipo makini sana ninachokula mkuu.Hahaha tunakula tu matumbo ya wabongo ya TBS, sema ukipata hela kidogo unaanza kugoogle madhara ya kula ugali haha
Mkuu,huku mbeya kuna kipindupindu sasa hivi
mbeya ndo kuna hili tatizo sana, usafi wa vyakula sio mzuri
na watu wanaoendekeza hizi tabia wanapata uzito uliokithiri
Nmesha kuacha to yeye 🤣🤣🤣Am sorry,sirudii kurukia mada za watu kwa kweli🙉
Kwa sasa siwezi kula kwa sababu nina uwezo wa kwenda sehemu nzuri nikakaa nikaagiza nikala.Unaweza kula mapaja ya kuku yanatembezwa na mtu hata humjui? Najua kifo kipo na tunatembea nacho ila muhimu kuchukua tahadhari, huwezi kuvuka barabara kizembe eti kwa vile kifo kipo na tunatembea nacho.
Duh, mkuu muhimu kuangalia kinachoingia mdomoni aisee, na wala sio lazima mtu uwe na uwezo ndio ule vyakula visafi, ni maamuzi tu kuwa either utapika mwenyewe au utakula sehemu zenye maandalizi mazuri. Tunategemea teachers kama nyie ndio mfundishe watu hygiene, wewe ndio unapromote tena🤣🤣Kwa sasa siwezi kula kwa sababu nina uwezo wa kwenda sehemu nzuri nikakaa nikaagiza nikala.
Ila kipindi bado nimekula sana vitu vya kutembezwa hadi sambusa, kuku hao, mayai ya kuchemsha, zile keki wanazikata kata wanaweka kwenye deli, yaani kwa kifupi nimekula hadi maandazi ya kununua sokoni ambayo mtu anakaangia kwake anakuja kuuza sokoni, viperege vile.
Mbona tunakula tu mkuu na tupo fresh tu. Ujue ukiwa na hofu na kitu ni rahisi kukudhuru kuliko pale ambapo hautakitilia hofu.
Ushaniharibia biashara boss.Weka mazingira mazuri ya uandaaji wa sambusa zako mkuu, hatutaki kula vibudu na nyama za mbwa🤣
Hello wakuu,
Kuna kitu nimekiona, kipo na mara nyingi najiwazia nakuwa na wasiwasi juu ya afya zetu kama jamii. Hii tabia ya kula kila mahali, mazingira yoyote bila kujua namna chakula kilivyoandaliwa.
Ukipita kwenye mikusanyiko na sehemu zilizochangamka utakuta meza zimewekwa, kuna kila aina ya vyakula, vyakula vya haraka mnaita take away kuanzia chips, ndizi hadi bites kama maandazi, kachori na juice za kutengeneza majumbani.
Najiwazia tu na kuona kabisa hakuna regulations kwenye hivi vyakula, sidhani kama upo usimamizi wowote na hili linanipa wasiwasi hasa ukiangalia namna jamii ilivyoharibika. Unakulaje sambusa mtu anatembeza barabarani? Unamjua huyo mtu, unajua ni nyama gani ameandaa, unajua mazingira aliyopika hizo sambusa? Maswali ni mengi, binafsi nikiona mtu busy ananunua mapaja ya kuku wanaotembezwa na anajilia kwa raha zake namuwazia mengi.
Siku hizi kuna serial killers, mtu anaweza kuamua tu kuua watu kwa namna anavyotaka, iwe kuweka sumu kwenye chakula au vyovyote vile na kwa namna wanavyouza, ni ngumu kujua nani alifanya hilo tukio. Huwa nikishuka pale mbezi mwisho na kuona watu wanavyokula kachori, supu ya pweza nk najisemea moyoni kweli nchi bado imejaa ujamaa.
Tujihadhari sana hasa kula vyakula ambavyo hatujui mazingira yake ya maandalizi.
Mkuu uwezo ndio unaamua mtu ale sehemu za hovyo au za hadhi. Wewe hauoni watu wananunua hadi maji yaliyofungwa kwenye vimifuko wanakunywa? Jero tu ya kununua chupa ya maji mtu hana, ndio buku jero ya kuagiza wali kwa mama ntilie?Duh, mkuu muhimu kuangalia kinachoingia mdomoni aisee, na wala sio lazima mtu uwe na uwezo ndio ule vyakula visafi, ni maamuzi tu kuwa either utapika mwenyewe au utakula sehemu zenye maandalizi mazuri. Tunategemea teachers kama nyie ndio mfundishe watu hygiene, wewe ndio unapromote tena🤣🤣
Hayapo ila dunia inaenda kasi sana, wale jamaa wanaopiga risasi kwenye madarasa, mitaani soon wanaingia Afrika, just from nowhere mtu anaamua kuuwa watoto wadogo mashuleni, unadhani hayawezi kufika bongo?Kwa kweli mauwaji ya aina hii hayapo hata haya ya mafuta ya Mangi nafikiri yametengenezwa tu ila sidhani kama waliotengeneza waliamua kuuwa watu
Kuhusu vyakula vya mitaani kwa kweli watu wanakula vingi vibaya na vizuri pia
Wengine wanauza kuku walionyongwa kwenye vibanda na vibaka na muuzaji huwezi kudhani ananunua mizoga na kuuza ila maisha yanaenda
Jamani binadamu tunauwezo wa kuvumilia njaa kama wanyama na ndege
Kwani nao kuna masiku huwa hawapati hata mlo mmoja
Ushauri muwe mnafunga hata siku mbili kwa wiki ni afya kwetu
Mimi sili mazagazaga hayo ya mitaani napika mwenyewe labda Nuts tu au mahindi
Kuangalia sana mitandao ya kijamii kunafundisha mengi mabaya na mazuri piaHayapo ila dunia inaenda kasi sana, wale jamaa wanaopiga risasi kwenye madarasa, mitaani soon wanaingia Afrika, just from nowhere mtu anaamua kuuwa watoto wadogo mashuleni, unadhani hayawezi kufika bongo?
Sidhani kama kuna anayependa kula vitu vilivyoandaliwa kwenye mazingira ya hovyo ila umasikini ndio tatizo. Mfano mtu ameshinda njaa kutwa nzima hata chai hajanywa jioni apewe offer ya chipsi za stend au kachori halafu akatae aseme hii imeandaliwa kwenye mazingira machafu. Inawezekana? Na uwezo wa kununua chakula hoteli ya kifahari hana. Je afanyeje? Tena mwingine unakuta ni homelessHello wakuu,