Wapwa na mabinamu
of recent nimehamia pemba ambako samaki ni chakula chao cha kila siku
ila mi kutoka bara naona maisha yatakuwa magumu kama nisipojua mila na desturi za kumla samaki
naombeni ushauri njia ipi bora ya kumla samaki hasa katika mazingira hayo?
natanguliza shukrani!:rolleyez:
hebu nipe japo mfano wa picha FL1...
nimeshatoka kule.....mmmh.....ngoja kwanza samaki asagwe kwen blenda? mbado kuona
ushauri:
msimamishe kwenye sahani kisha uanze kula chini kwenda juu ukianza na upande mmoja kisha ukimalizia na upende wa pili, mboga za majani hurti ziwepo pembeni na pili pili kidogo eidha pili pilimbuzi ama pilipili manga inafaa mradi upate kale ka muwasho.! usisahau kunawa mikono kabla hujaanza kula, pengine unaweza kuona akiangukia ubavu au chali chali we endelea kumla hivyo hivyo mpaka uhakikishe hamu/shibe yako imefika mahali pake.
huyu shurti lake akiliwa upande mmoja unageuzia mwigine ..hata kichwa kinaliwa binamu ..ikiwezekana na mifupa kama meno yako ni meupe na yenye nguvu ..kwa raha zako
FL1 unatutamanisha na huyo samaki
Mi ninavyojua mila za huko, samaki analiwa upande mmoja, ukifika kwenye mwiba wa kati huutoi ila unamgeuza na kuanza kula upande wa pili.
Wataalam wanadai samaki hageuzwi, bali unautoa ule mwiba wake wa kati, halafu unaendelea kumla.
Mmh jamani, I hope ni samaki yule yule wa majini ndio tunamzungumzia, isije ikawa kuna tafsida ndani yake!