MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Naandika kwa masikitiko makubwa sana ikiambatana na huzuni. Hili tatizo la ajira ni karibu dunia nzima kwa sasa hasa Afrika. Ila tunachotofautiana ni namna ya kukabiliana na tatizo. Nchi nyingi za Afrika tunatumia mbinu za hovyo kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana.
Wanasiasa, viongozi wa dini na public figures wengine kila mara wamejitokeza hadharani na kuwataka vijana wajiajiri ili kujikwamua kwenye hali ngumu. Mimi naona hizo ni porojo ambazo zimewachosha kabisa vijana. Kwanza kudhani kila mtu anaweza kuwa mfanyabiashara ni kosa kubwa mno. Kudhani kuwa kijana akipata mtaji na kujiajiri atafanikiwa ni dharau kubwa kwa ujasiriamali na biashara kwa ujumla. Biashara ni zaidi ya mtaji. Wengi hawana vipaji wala mbinu za kudumu kwenye biashara wanazoanzisha ambapo matokeo yake ni kufeli vibaya kisha kijana kupata stress. Wakati kijana kafeli hupokea lawama kutoka kila kona na mwisho wa siku madhara mengine huanza.
Mimi nadhani serikali ingefikiria upya kuhusu mikopo inayotolewa kwa vijana kupitia 10% ya mapato ya halmashauri kama ina tija au la. Binafsi najua ile mikopo ipo kisiasa sana na mara nyingi huwa haileti matokeo yoyote kwa vijana. Ni ngumu sana kundi la watu zaidi ya 10 wakawa na vision moja ya biashara. Hata kama vision itakuwa moja ni ngumu kuwa pamoja wakati wa mchakato wa kutimiza ndoto.
Mimi nadhani serikali ingetoa mikopo isiyo na riba kuwawezesha wale vijana ambao tayari wameshaanza biashara na zinaonyesha kukua ili ziwe kubwa na kuajiri vijana wenzao. Kwa mfano serikali inaweza toa Tsh 20m kwa biashara ya kijana wa kitanzania ambayo tayari imeshaanza na inafanya vizuri ikiwa pamoja na kulipa kodi. Tsh 20m kwa vijana 10000 ni kama bilioni 200 kitu ambacho serikali hii inaweza. Na hizo bilioni 200 wapewe benki kama NMB au CRDB kuzifuatilia. Yaani wawe mawakala. Au Takukuru wawe mawakala wa hiyo mitaji. Hapo hela zitarudi na vijana watapambana.
Kuna vijana wanaofanya vizuri sana kwenye biashara za kilimo, sanaa, ufugaji, ufundi na fani zingine ila mitaji midogo. Hawa wawezeshwe baada ya kutoa hela kwa makundi ambayo hujiunga tu ili kupata hela za halmashauri na kuzitumia hovyo. Serikali ikalitazame na hili.