Kuleni Tikitimaji (Water Melon) kwa tahadhari

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Sio kila kinacholiwa kinaweza kuliwa wakatiti wowote. Leo nitawapeni kwa uchache elimu kuhusu ulaji wa vyakula.

Vyakula vimegawanyika katika makundi makuu 6 ya kutia nguvu, kujenga mwili, kulinda mwili, kutia joto, madini na maji.

1. Katika kundi la Vyakula vya kutia nguvu (carbohydrates) viko mahindi, ubwabwa, uwele, ulezi, ngano, mihogo, mtama, viazi, maharage, kunde, n.k. Usagaji na ufyonzwaji mwilini wa kundi hili la vyakula unahitaji vimeng'enyo vinavyohitaji mazingira yasiyokuwa na acid kali, yaani vinahitaji alkaline environment kuanzia mdomoni hadi tumboni na kwenye utumbo.

2. Katika kundi la vyakula vya kujenga mwili (proteins) viko nyama za aina zote, mayai, maziwa. Usagaji wa vyakula hivi vinapoliwa unahitaji vimeng'enyo (enzymes) vinavyohihitaji kufanyakazi kwenye mazingira ya uchachu (acid) mwingi tumboni. Yaani kwenye alkaline environment nyama, maziwa, mayai havisagwi na kufyonzwa vizuri mwilini.

Ushauri: Kuhusu kula vyakula vya Carbohydrates na Protini: Usichanganye kwa wakati mmoja makundi haya mawili ya vyakula kwenye mlo mmoja li kuurahisishia mfumo wako wa chakula katika kusaga chakula ulichokula.

Kama utavichanganya pamoja mwili wako utavyonza sumu nyingi kutoka tumboni zinazotokana na kuoza (ferment) kwa chakula ambacho kinachelewa kusangwa tumboni, pia unaweza kupata kansa ya tumbo na utumbo. unashauriwa Kula ugali/ubwabwa na maharagwe,

nyegele, choroko, dengu, n.k badala ya kula ugali/ubwabwa pamoja na nyama, mayai au maziwa ili kusaidia tumbo kusaga chakula haraka. Kula nyama, maziwa au mayai masaa 3 kabla au baada ya mlo wenye vyakula vya kutia nguvu.

3. Katika kundi la vyakula vinavyolinda mwili yapo matunda na mboga za majani. Matikiti maji ni miongoni mwa matunda yanayopendwa duniani kote yenye madini mengi hasa mbegu zake,

LAKINI sasa tikiti maji na nyanya (oxalate) vina tabia mbaya ya kuzuia usagaji na ufyonzwaji wa aina nyingine za vyakula na virutubisho (madini na vitamins) na kuukosesha mwili rutuba na kusababisha vyakula kukaa sana tumboni.

Matikiti maji yanapoliwa na vyakula vingine kwa wakati mmoja yanaweza kusababisha hali ya kujisikia kichefuchefu pia.

Ushauri:

a) Kuhusu tikitimaji: tikiti maji liliwe masaa 3 kabla au baada ya kula vyakula vingine.

b) Usile chakula pamoja na nyanya mbichi, nyanya ina kemikali (oxalate) inayozuia virutubisho vingine kufyonzwa haraka mwilini.

c) Kula vyakula vya carbohydrates na proteins pamoja na mboga za majani (greens) ili kuboresha usagaji na ufyonzwaji wake.

d) Maji yana tabia ya kupunguza kasi ya kusaga na kumeng'enya chakula tumboni, hivyo usinywe maji wakati wa kula, kunywa maji saa 1 baada au kabla ya mlo.

e) Kuchanganya nafaka (mahindi, mchele, mtama, ulezi, ngano, n.k) kwenye mlo mmoja hakuleti faida yoyote ya kiafya mwilini, aina moja tu ya nafaka ambayo haikukobolewa sana inaleta faida inayokusudiwa. epuka gharama zisizo za lazima kwa kuchanganya aina nyingi za nafaka au proteins (mayai, nyama, maziwa, samaki) kwa wakati mmoja kwenye mlo mmoja, hakuna faida kiafya kufanya hivyo.

f) epuka kuchanganya matunda baridi (matango, matikiti, parachichi, ndizi, karoti, n.k) na yale makali (machungwa, passions, ukwaju, mabungo, matofaa, maembe, zabibu, ndimu, limau, n.k) kwenye mlo mmoja au kuyachanganya na sukari. Yaani kula tango tu, au chungwa tu, au tikiti maji tu au ndizi tu kwa wakati mmoja.

g) Vyakula vilivyochachuka kama vile mtindi, kabichi, togwa, mbege, mvinyo vinasadia kusaga chakula haraka tumboni. Ukivipata usiviache.

h) Kunywa maziwa peke yake kwa wakati wa peke yake, angalau nusu saa kabla au baada ya kula milo ya aina nyingine au dawa. Epuka chai za maziwa pia kama unaweza.

Usiku: Usiku mwili unahitaji protein zaidi ili kupata matofali (amino acids) ya kuujenga mwili na kurekebisha sehemu za mwili zilizoharibika na kuumia wakati wa mchana.

Wakati wa kulala mwili hauhitaji chakula kingi cha kutia mwili maana kazi zinazohitaji nguvu nyingi hakuna. Hivyo,

ni marufuku kula sahani ya ugali/ubwabwa na kwenda kupanda kitandani kulala wakati huo huo, maana chakula hakitasangwa vizuri na mwili utatengeneza sumu nyingi sana na kuwa na uwekezano wa kuota ndoto mbayambaya tu usiku kucha.

Asubuhi: Mwili unahitaji chakula cha kutosha cha kutia nguvu, na matunda, juice, siagi, asali, sukari, mkate, kiporo cha ubwabwa ili kuupatia mwili nguvu nyingi za kuendesha mitambo ya mwili inayohitaji nguvu (break fast).

Ianze siku yako kwa mlo wenye rutuba zote na kukutia nguvu nyingi sana.

Kama una swali lolote kuhusu namna ya kuchanganya vyakula uliza ujibiwe! Asalam aleykum.
 
Asante. Ila nadhani mpaka hapa nilipo fikia huo ndio utaratibu wa maisha na wazee wangu waliishi hivyo ... sasa nadhani hizi sumu za kula ugali nyama au wali nyama nimezizoea

ruksa, kupanga ni kuchagua. Kumbuka kuwa matumbo ya wazee wetu yalikuwa na uwezo mkubwa wa kusaga nyama kuliko haya ya kwetu kutokana na aina za kazi zao walizokuwa wakifanya mchana kutwa. Walikuwa wakitoka jasho nyingi na kunywa maji mengi yanaoziondoa sumu za vyakula. Yako makundi ya watu hata leo wenye uwezo mkubwa wa kuziondoa sumu hizo mwilini kama vile wanamichezo (mpira, ngumi, riadha, makuli, n.k).

Hata makabila ya wafugaji yanakula nyama tu bila ya kuchanganya na ugali wala ubwabwa ndio maana yamehimili kuweko. Kauli kama hii ya kwako ni sawa na tangazo rasmi kwako la maandalizi ya kupokea magonjwa ya moyo, kisukari, misuli, mifupa, kansa, mafigo na uzee wa mapema. Wazee wenu walikuwa hawana viyoyozi, magari, masoda, majuice, chips, na kuku wa kizungu kwenye milo yao, walikuwa wakifanyakazi nzito na kutoka jasho lenye chumvi nyeupe kabisa linalotoka na sumu walizokula.
 
Kuna vitu vingine ukivisikia na kujitafakari unaishia kujisemea.........."I should'nt be alive"

Lakini maisha yanadunda na kusonga mbele...

Asante kwa maujuzi tumekusikia na tutaifuatilia!
 

alekhum asalam kalfa!?????
 
Kuna vitu vingine ukivisikia na kujitafakari unaishia kujisemea.........."I should'nt be alive"

Lakini maisha yanadunda na kusonga mbele...

Asante kwa maujuzi tumekusikia na tutaifuatilia!
Usikate tamaa kabla ya kupata majibu ya kwanini siku hizi magonjwa ya moyo, mafigo, kansa, ugumba, utasa, kisukari, watoto wanaozaliwa na hitilafu na unene kupita kiasi vinaongezeka kwenye jamii zetu kuliko zamani.
 
Wacha mwili wako utoke jasho basi ili upunguze sumu mwilini, piga vita matumizi ya kupita kiasi ya viyoyozi maofisini, na kwenye magari, fanya mazoezi ya kutosha hadi jasho likutoke na kunywa maji mengi kila siku vitakusaidia pia kutoa sumu mwilini kwako.
 
Inakuwaje hapa penye red ulinganisha na penye green?



 
Inakuwaje hapa penye red ulinganisha na penye green?

Hapo pekundu: Usichanganye proteins na carbohydrates kwenye mlo mmoja.

Hapo pa green: Unaweza kula vyakula vya proteins au carbohydrates pamoja na mboga za majani (protein + greens or Carbohydrates + greens). Kila mlo ni vizuri ukaliwa na mboga za majani
 
1) Unaweza kurejea notice zako vizuri hasa pale kwenye kijani?

2. Unaweza kuandika vyakula vya protein ni vipi?


 
kavulata

Nashukuru sana ndugu kavulata Ila naomba unisaidie hili: Niliwahi kusikia kuwa si vizuri kula chakula na maji wakati mmoja at least mpaka itakapopita nusu saa au maji yanyweke nusu saa kabla ya kula chakula.

Tafadhali naomba unifahamishe zaidi kuhusu hilo.
 
Last edited by a moderator:
1) Unaweza kurejea notice zako vizuri hasa pale kwenye kijani?

2. Unaweza kuandika vyakula vya protein ni vipi?

Kuna makundi ya aina 2 za proteins:

1. protein halisi (class 1 au pure protein), hizi ni proteins zinazotokana na wanyama, samaki, ndege, na wadudu, maziwa na mayai. Usagaji wa aina hii ya protein kwa binadamu ni kazi ngumu sana inayohitaji tumbo liwe na tindikali (acid) kali sana inayoruhusu enzymes zinazomeng'enya protein (pepsin) ziweze kufanya kazi ili mwili uweze kuzipata amino acids zilizomo kwenye nyama hizo,

na wakati mwingine kutegemeana na aina nyama huna budi kuzisadia enzymes hizi kwa kuipika sana nyama ili ilainike ama kuilegeza nyama kwa viungo kama utovu wa mapapai, vitunguu saumu, tangawizi, vinegar, n.k ili kurahisisha usagwaji wake tumboni. Kwa ujumla matumbo yetu huwa hayataki kabisa kusikia habari za nyama ila tunayalazimisha tu. Hivyo kitendo chochote kitakachoshusha acid tumboni kitasababisha janga kwenye usagaji wa nyama tumboni.

Bahati mbaya vyakula vya aina ya carbohydrates vinasababisha kuishusha acid hii vinapoliwa kwa kusababisha kuzalishwa kwa bicarbonates nyingi kwenye mate na tumboni ili kuruhusu saliva amylase na alpha amylase viweze kumeng'enya carbohydrate yako uliyokula na hatimaye uweze kupata sukari (glucose). Ndiyo maana hutakiwi kuchanganya carbohydrates na proteins za aina hii ili kupunguza kulitatiza tumbo lako.

2. protein hafifu (class 2), hizi ni zile proteins zinazotokana na mimea kama vile maharage, nyegere, soya, njugumawe, fiwi, choloko, n.k. ndani ya mbegu hizi za mimea kuna kiasi cha starch pia. Protein kutoka kwenye mbegu za mimea ni rahisi sana kusagwa na miili yetu kuliko protein inayotoka kwenye nyama za ng'ombe, mbuzi, nyati, kuku, n.k. Hivyo unaweza kuila pamoja na vyakula vya carbohydrates bila kusababisha usumbufu mkubwa wa usagaji tumboni.

Tafiti zinaonyesha kuwa kula chakula pamoja na mboga za majani hakuna madhara
 

Maji yanasaidia kuyeyusha vyakula tunavyokula lakini maji yanatabia pia ya kupoza kasi ya kumeng'enya vyakula vyetu kwa njia tatu:
1. Maji yana-dilute concentration ya enzymes zinazohitajika kumeng'enya chakula
2. Maji yana-dilute concentration ya gastric juice inayohitajika kutoa mazingira sahihi ya kumeng'enya proteins au carbohydrates
3. Maji baridi sana tumboni yanapunguza kasi (deactivate) ya mimeng'enyo kumeng'enya vyakula kwa wakati. Maji na vinywaji baridi sana sio vizuri kwa usagaji wa vyakula tumboni, kunywa maji ya kawaida tu sio mabarafu unajimaliza mwenyewe.
 

Shukran sana kwa somo mkuu.


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…