kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
- Thread starter
-
- #81
Asante sana kavulata kwa muongozo,ila kuna mambo mengine ni ngumu kumuongoza mtu mzima na ukizingatia ni mawifi naweza onekana mchoyo bure,ila nitajitahid kadri ya uwezo wangu,asante sana.
Mambo muhimu kuhusu mgonjwa:
1. Kupunzika: Dawa kubwa kuliko zote kwa mgonjwa ni kupunzika (resting), kupunzika kunasaidia mgonjwa kutumia chakula anachokula kwa kujenga upya na kuponyesha sehemu zilizoharibika (zinazoumwa)
2. Chakula: Mgonjwa apewe vyakula vingi kutoka kundi la vyakula vya protein labda kama ugonjwa wake utakataza kupewa protein nyingi. Protein ndiyo inayotoa matofali ya ujenzi wa mwili wa mgonjwa. Mpe chakula cha kutia nguvu kiasi kidogo lakini kiasi kikubwa cha proteins. Nyama inatoa protein grade 1, lakini huwa inasangwa kwa shida tumboni na kusababisha mwili kuwa na sumu nyingi. Saidia usagaji wa nyama kwa kuipika sana, kuisaga, kuiwekea viungo vya kulainisha na kutafuna vya kutosha. Kama ni lazima kula nyamba peke yake na kupunzika kama wanavyofanya wanyama wanaokula nyama, mfano, simba akishakula nyama huwa anapunzika hadi nyama isagwe tumboni.
3. Matunda na Mboga: Kula sana vyakula hivi kila wakati. Vyakula vibichi huwa vinaupa mwili zawadi kubwa kuliko vyakula vilivyopikwa sana, vyakula vibichi ndo silaha kubwa wanayoitegemea wanyama na ndege wa porini kuweza kupambana na maradhi.
4. Maji mengi: mgonjwa apewe maji ya kunywa mengi ili kuosha mwili kutokana na madawa anayokunywa /meza
5. Uchunguzi: Sehemu muhimu ya matibabu ni kujua unaumwa nini kwanza kabla ya kumeza dawa. Kama mgonjwa wako ana TB ni bora achunguzwe damu pia ili kujua kama ana damu, maji, na kinga ya mwili ya kutosha. Maana takwimu siku hizi zinaonyesha kuwa 50% ya wagonjwa wote wenye TB huwa pia wana HIV (co-infection).
6. Dawa: Tumia dawa kama unavyoelekezwa na wataalamu wako, zingatia maelekezo yote kuhusu dozi, wakati, na masharti ya kumeza dawa.
7. Screening contacts: TB ya mapafu inaambukizwa kwa njia ya hewa, hivyo watu wote walio karibu au wanaomhudumia mgonjwa lazima waende hospitali kuchunguzwa kama wamepata maambukizi ya TB. Maana kabla ya kugundulika kuwa ana tb alikuwa akiishi na kushirikiana na watu wengine bila masharti wala tahadhali zozote.
8: Food supplements: Mwili wa mgonjwa una mahitaji ya ziada ya chakula, unaweza kuuongezea kwa kuupatia baadhi ya virutubisho kwa kumeza vidonge kama vile multivitamins, folic acid, vitamin A, Iron, n.k ili kuurahisishia upatikanaji wa virutubisho hivyo