Kuleni Tikitimaji (Water Melon) kwa tahadhari

Kuleni Tikitimaji (Water Melon) kwa tahadhari

Asante sana kavulata kwa muongozo,ila kuna mambo mengine ni ngumu kumuongoza mtu mzima na ukizingatia ni mawifi naweza onekana mchoyo bure,ila nitajitahid kadri ya uwezo wangu,asante sana.

Mambo muhimu kuhusu mgonjwa:
1. Kupunzika: Dawa kubwa kuliko zote kwa mgonjwa ni kupunzika (resting), kupunzika kunasaidia mgonjwa kutumia chakula anachokula kwa kujenga upya na kuponyesha sehemu zilizoharibika (zinazoumwa)

2. Chakula: Mgonjwa apewe vyakula vingi kutoka kundi la vyakula vya protein labda kama ugonjwa wake utakataza kupewa protein nyingi. Protein ndiyo inayotoa matofali ya ujenzi wa mwili wa mgonjwa. Mpe chakula cha kutia nguvu kiasi kidogo lakini kiasi kikubwa cha proteins. Nyama inatoa protein grade 1, lakini huwa inasangwa kwa shida tumboni na kusababisha mwili kuwa na sumu nyingi. Saidia usagaji wa nyama kwa kuipika sana, kuisaga, kuiwekea viungo vya kulainisha na kutafuna vya kutosha. Kama ni lazima kula nyamba peke yake na kupunzika kama wanavyofanya wanyama wanaokula nyama, mfano, simba akishakula nyama huwa anapunzika hadi nyama isagwe tumboni.

3. Matunda na Mboga: Kula sana vyakula hivi kila wakati. Vyakula vibichi huwa vinaupa mwili zawadi kubwa kuliko vyakula vilivyopikwa sana, vyakula vibichi ndo silaha kubwa wanayoitegemea wanyama na ndege wa porini kuweza kupambana na maradhi.

4. Maji mengi: mgonjwa apewe maji ya kunywa mengi ili kuosha mwili kutokana na madawa anayokunywa /meza

5. Uchunguzi: Sehemu muhimu ya matibabu ni kujua unaumwa nini kwanza kabla ya kumeza dawa. Kama mgonjwa wako ana TB ni bora achunguzwe damu pia ili kujua kama ana damu, maji, na kinga ya mwili ya kutosha. Maana takwimu siku hizi zinaonyesha kuwa 50% ya wagonjwa wote wenye TB huwa pia wana HIV (co-infection).

6. Dawa: Tumia dawa kama unavyoelekezwa na wataalamu wako, zingatia maelekezo yote kuhusu dozi, wakati, na masharti ya kumeza dawa.

7. Screening contacts: TB ya mapafu inaambukizwa kwa njia ya hewa, hivyo watu wote walio karibu au wanaomhudumia mgonjwa lazima waende hospitali kuchunguzwa kama wamepata maambukizi ya TB. Maana kabla ya kugundulika kuwa ana tb alikuwa akiishi na kushirikiana na watu wengine bila masharti wala tahadhali zozote.

8: Food supplements: Mwili wa mgonjwa una mahitaji ya ziada ya chakula, unaweza kuuongezea kwa kuupatia baadhi ya virutubisho kwa kumeza vidonge kama vile multivitamins, folic acid, vitamin A, Iron, n.k ili kuurahisishia upatikanaji wa virutubisho hivyo
 
Saf sana doctor, so nyama ziliwe na chakula gan?? I mean tambi, ndiz au viaz???
 
Saf sana doctor, so nyama ziliwe na chakula gan?? I mean tambi, ndiz au viaz???

Kama una hamu ya kula nyama, mwambie mchoma nyama akupe nyama tu basi ule, kama ana salad mwambie akuwekee na salad tu basi ule pamoja na nyama yako. Usianze tena kuagiza na ugali, viasi, n.k. Ukizidiwa sana kula nyama na ndizi maana hazina starch nyingi kama ugali, viazi na wali. Usinywe tena bia, soda wala maji hapo hapo utaharibu. Kama unataka bia kunywa bia zako mbili kisha ondoka zako achana na nyama choma wala kitimoto kwa wakati huohuo, ila unaweza kunywa bia na vitu vidogo vidogo kama karanga, korosho,......
 
Nakiri kuwa kubadilisha tabia hasa ulaji wa vyakula sio kazi ndogo, lakini ukimudu kutakupunguzia mateso ya magonjwa, matumizi mabaya ya fedha na kukuongezea furaha. Dawa zinaua vijdudu mwilini na chakula kinaponyesha.
 
Mambo muhimu kuhusu mgonjwa:
1. Kupunzika: Dawa kubwa kuliko zote kwa mgonjwa ni kupunzika (resting), kupunzika kunasaidia mgonjwa kutumia chakula anachokula kwa kujenga upya na kuponyesha sehemu zilizoharibika (zinazoumwa)

2. Chakula: Mgonjwa apewe vyakula vingi kutoka kundi la vyakula vya protein labda kama ugonjwa wake utakataza kupewa protein nyingi. Protein ndiyo inayotoa matofali ya ujenzi wa mwili wa mgonjwa. Mpe chakula cha kutia nguvu kiasi kidogo lakini kiasi kikubwa cha proteins. Nyama inatoa protein grade 1, lakini huwa inasangwa kwa shida tumboni na kusababisha mwili kuwa na sumu nyingi. Saidia usagaji wa nyama kwa kuipika sana, kuisaga, kuiwekea viungo vya kulainisha na kutafuna vya kutosha. Kama ni lazima kula nyamba peke yake na kupunzika kama wanavyofanya wanyama wanaokula nyama, mfano, simba akishakula nyama huwa anapunzika hadi nyama isagwe tumboni.

3. Matunda na Mboga: Kula sana vyakula hivi kila wakati. Vyakula vibichi huwa vinaupa mwili zawadi kubwa kuliko vyakula vilivyopikwa sana, vyakula vibichi ndo silaha kubwa wanayoitegemea wanyama na ndege wa porini kuweza kupambana na maradhi.

4. Maji mengi: mgonjwa apewe maji ya kunywa mengi ili kuosha mwili kutokana na madawa anayokunywa /meza

5. Uchunguzi: Sehemu muhimu ya matibabu ni kujua unaumwa nini kwanza kabla ya kumeza dawa. Kama mgonjwa wako ana TB ni bora achunguzwe damu pia ili kujua kama ana damu, maji, na kinga ya mwili ya kutosha. Maana kwa siku hizi 50% ya wagonjwa wote wenye TB huwa pia wana HIV.

6. Dawa: Tumia dawa kama unavyoelekezwa na wataalamu wako, zingatia maelekezo yote kuhusu dozi, wakati, na masharti ya kumeza dawa.

7. Screening contacts: TB ya mapafu inaambukizwa kwa njia ya hewa, hivyo watu wote walio karibu au wanaomhudumia mgonjwa lazima waende hospitali kuchunguzwa kama wamepata maambukizi ya TB. Maana kabla ya kugundulika kuwa ana tb alikuwa akiishi na kushirikiana na watu wengine bila masharti wala tahadhali zozote.

8: Food supplements: Mwili wa mgonjwa una mahitaji ya ziada ya chakula, unaweza kuuongezea kwa kuupatia baadhi ya virutubisho kwa kumeza vidonge kama vile multivitamins, folic acid, vitamin A, Iron, n.k ili kuurahisishia upatikanaji wa virutubisho hivyo
Asante sana kavulata kwa ushauri,huyu mgonjwa wangu ni muathirika wa HIV toka siku nyingi sana,Mungu akiniwezesha wikiend hii nitajitahidi kutembelea kule mwanzo alikokuwa anaishi maana ana watoto 2 nao waende wakacheki afya zao kama hiyo TB haijawakumba.

Naomba pia ushauri namna ya kumsaidia asubuhi analalamika anakuwa amechoka sana kiasi kwamba hawezi kufanya lolote kabisa,analegea kabisa akisha kunywa dawa mpka labda mchana mida ya saa 7 au 8 ndo anachangamka.
 
Last edited by a moderator:
Nimetuma maswali yangu x3 imegoma sijui kuna nini!!!
 
Mkuu kavulata nimekusoma vizur,
Kwenye BMI umeelezea kwa atakaezid vipi kwa alie below 18.5 huyu nakabiliwa na nini?
Halafu naomba kujua kwa aliepatwa na stroke huyu nilizama atakuwa na tatizo la moyo au ni vitu tofauti kabisa
Kingine nakushukuru kwa elimu ya tikitikimaji kwani nimekuwa nikayala sana halafu naishia kujiskia vibaya na saa nyingine choo kinaleta shida hadi ikafikia wakati nikawa nayatilia shaka haya matunda.
Kwahyo nime conclude na nitakula kwa tahadhar.
Asante sana mkuu..
 
Last edited by a moderator:
Asante sana kavulata kwa ushauri,huyu mgonjwa wangu ni muathirika wa HIV toka siku nyingi sana,Mungu akiniwezesha wikiend hii nitajitahidi kutembelea kule mwanzo alikokuwa anaishi maana ana watoto 2 nao waende wakacheki afya zao kama hiyo TB haijawakumba.

Naomba pia ushauri namna ya kumsaidia asubuhi analalamika anakuwa amechoka sana kiasi kwamba hawezi kufanya lolote kabisa,analegea kabisa akisha kunywa dawa mpka labda mchana mida ya saa 7 au 8 ndo anachangamka.

Dawa za TB (anti tuberculosis) ni mchanganyiko wa dawa nyingi zenye nguvu kubwa, hasa kwa mtuamiaji ambaye tayari afya yake imeshadhoofika, isitoshe dawa hizi zinatakiwa kumezwa asubuhi kabla mgonjwa hajakula (empty stomach), hivyo mgonjwa atasikikia kuchoka sana na pengine hata kichefu2 hasa kwa miezi 2 ya kwanza ya kumeza dawa, baada ya hapo dozi itapunguzwa kidogo na mgonjwa atajisikia nafuu. Baadhi ya dawa zilizomo kwenye mchanganyiko wa dawa za anti-tb hasa ile inayoitwa Isoniazid inaweza kusababisha ganzi kwenye miguu (peripheral neuropathy) na kusababisha ashindwe kutembea vizuri, hivyo pamoja na dawa na vyakula kwa mgonjwa pia mi muhimu mgonjwa akapewa dawa ya pyridoxine (Vitamin B6) kama msaada wa kupunguza tatizo hili la ganzi lisijitokeze kwa ukubwa. Hata hivyo lazima aendelee na kumeza dawa hata kama anachoka sana au anapata ganzi miguuni ili kuzuia vijidudu vya tb kuwa sugu. Ganzi ikizidi mpeleke hospitali akawekewe pyridoxide (vitamin B complex) kwenye drip la maji. Inshallah atapata nafuu. Dawa zinaua wadudu lakini chakula kinaponya.
 
Mkuu kavulata nimekusoma vizur,
Kwenye BMI umeelezea kwa atakaezid vipi kwa alie below 18.5 huyu nakabiliwa na nini?
Halafu naomba kujua kwa aliepatwa na stroke huyu nilizama atakuwa na tatizo la moyo au ni vitu tofauti kabisa
Kingine nakushukuru kwa elimu ya tikitikimaji kwani nimekuwa nikayala sana halafu naishia kujiskia vibaya na saa nyingine choo kinaleta shida hadi ikafikia wakati nikawa nayatilia shaka haya matunda.
Kwahyo nime conclude na nitakula kwa tahadhar.
Asante sana mkuu..

BMI yako ikiwa chini ya 18.5 ina maana kuwa una uzito wa mwili mdogo sana isivyotakiwa (under-nutrition)ongeza kiasi cha chakula mwilini. hata hivyo BMI haitumiki kwa wajawazito, wazee sana, na watoto wadogo.
 
Mkuu kavulata nimekusoma vizur,
Kwenye BMI umeelezea kwa atakaezid vipi kwa alie below 18.5 huyu nakabiliwa na nini?
Halafu naomba kujua kwa aliepatwa na stroke huyu nilizama atakuwa na tatizo la moyo au ni vitu tofauti kabisa
Kingine nakushukuru kwa elimu ya tikitikimaji kwani nimekuwa nikayala sana halafu naishia kujiskia vibaya na saa nyingine choo kinaleta shida hadi ikafikia wakati nikawa nayatilia shaka haya matunda.
Kwahyo nime conclude na nitakula kwa tahadhar.
Asante sana mkuu..

pole sana, elimu ya vyakula ni muhimu sana, elimu hii inatoka kwa Mungu mwenyewe ndiyo maana hata wanyama porini wanaishi miaka nenda rudi bila kwenda hospitali. Usile hovyo hovyo, baadhi ya vyakula vikichanganywa pamoja vinatengeneza sumu mwilini, vingine vinatengeneza mawe kwenye mafigo, vingine vinaharibu kokongosho, ubogo, ini, n.k. Lakini viko vingine vikiliwa peke yake au kuchanganywa ni dawa ya kitu fulani mwilini. Ukiwadadisi sana wanyama na ndenge wanavyokula utagundua na kujifunza mengi. Mnyama pekee ambae usiige matendo yake na ikiwezekana usiyaguse mazao yake ni nguruwe, ndiyo maana hakuna anayekula damu, maziwa, utumbo, figo, na maini ya nguruwe hata akiwa mpenda nyama vipi. Ndiyo maana kuna watu wanaoamini kuwa mapepo yote yalikimbilia kwa nguruwe hii sio kweli lakini ukweli ni kuwa nguruwe hachagui vyakula, anakula hata nyama, majani, ugali, wali, dagaa, samaki, mashudu kwa wakati mmoja na kusababisha mwili wake kujaa sumu nyingi sana kupaswa kuliwa na binadamu, hata wazee wa kale sana wa Kiyahudi na Kiarabu walilifahamu hili mapema hadi wakakataza nguruwe asiliwe kabisa. Kutokana na sumu iliyoko kwenye nyama ndiyo maana hata wanyama wanaokula nyama kama simba, fisi, mbwa, chui, paka n.k hawaliwi na binadamu wala wanyama wengine pia. Simba hawezi kumkamata na kumla fisi, chuo, mbwa, n.k hata kama akiwa na njaa vipi kwakuwa nyama zao zina sumu nyingi kutokana na kula nyama za wanyama wengine. UkiFuatilia kwa makini binadamu wanaokula wanyama wanaokula nyama kama vile mbwa, simba, n.k utagundua kuwa wanapatwa na hitilafu fulani. Nyama ni mbaya wapendwa kuleni kwa tahadhari.
 
Kila mtu ni lazima atafute siku moja kila wiki ya kupiga deki mfumo wake wa chakula. Kutokana na kula vyakula kila siku tumbo pia huwa linahitaji kufanyiwa usafi angalau mara 1 kwa wiki. Tumbo, utumbo, ini na mafigo huwa yanafurahia pia kupata off au kupunguziwa mzigo japo kwa masaa 12 kwa wiki. Wamasai na baadhi ya makabila huwa wanafanya hivyo kwa kunywa dawa zinazowafanya waharishe sana na kukiondoa chakula chote na wadudu kama minyoo na bacteria kwenye mfumo wa chakula ili kutoa ahuweni kwa tumbo. Lakini njia bora na sahihi ya kupiga deki na kupunzisha tumbo, utumbo, ini na mafigo ni kwa kuacha kula, yaani kufunga (fast) kwa masaa 12 mfululuzo kila wiki mara moja. Kufunga kunasaidia pia mwili kuzoa na kuchoma sumu na takataka nyingi zisizofaa mwilini ambazo ni chanzo cha magonjwa na upungufu wa kinga mwilini. Unaweza kushinda kutwa nzima kwa kunywa maji na kula matunda tu hadi jioni. Kufunga kunasaidia kuchoma chakula na mafuta yaliyozidi mwilini. Hata wazee wetu wa zamani walifahamu uhusiano uliopo kati ya kufunga na afya. Mfano, waislamu wanatakiwa kufunga siku 36 za lazima kila mwaka (Ramadhani), hii ni sawa na kufunga siku 1 kwa kila siku 10 wakichanganya na kufunga suna zao mbalimbali itakuwa wanafunga siku 1 kwa kila siku 7. Wakristo nao wanatakiwa kufunga kwa lazima siku 40 kwa mwaka (Kwaresma), hii ni sawa na kufunga siku 1 kwa kila siku 9, wakichanganya na kufunga kwasababu za maombi yao binafsi inakuwa sawa na kufunga siku 1 kila siku 7. Wanafahamu kuwa hata Mungu alifanyakazi siku 6 na ya 7 akapunzika, bila shaka alipunzika hata kula. Hii inaonyesha kuwa wazee wetu walikuwa na elimu kubwa sana kuhusu vyakula na afya. Walijua kuwa kufunga kunawasaidia kuondoa vitambi na magonjwa kama pressure, kisukari, ugumba, uhanithi, moyo na unene. Hebu wafuatiliwe watu wote wenye tabia ya kufunga kila wakati kama masheikh na wachungaji utagundua kitu hapo kuhusu afya zao na umri wao wa kuishi vikoje. Kama wewe una presure, kisukari, ugumba, au uhanithi (kuishiwa nguvu za kiume) dawa yako kubwa kuliko zote ni kufunga mara kwa mara na mazoezi. unaweza kufunga mchana na kunywa maji na matunda tu.

Nakushauri ndugu yangu na wewe jifunze kufunga kila mara ili uboreshe afya yako, kufakamia kama nguruwe kila wakati sio deal. Kitambi, matako, mapaja na shingo kubwa ni dalili ya magonjwa ya pressure, stroke, moyo, mafigo, kisukari na mifupa siku za usoni, acha, cha, cha sio afya, uzuri wala utajiri ni shiiiida!. Ni heri masikini mwenye sura mbaya na afya njema kuliko tajiri mzuri mgonjwa.
 
Kila mtu ni lazima atafute siku moja kila wiki ya kupiga deki mfumo wake wa chakula. Kutokana na kula vyakula kila siku tumbo pia huwa linahitaji kufanyiwa usafi angalau mara 1 kwa wiki. Tumbo, utumbo, ini na mafigo huwa yanafurahia pia kupata off au kupunguziwa mzigo japo kwa masaa 12 kwa wiki. Wamasai na baadhi ya makabila huwa wanafanya hivyo kwa kunywa dawa zinazowafanya waharishe sana na kukiondoa chakula chote na wadudu kama minyoo na bacteria kwenye mfumo wa chakula ili kutoa ahuweni kwa tumbo. Lakini njia bora na sahihi ya kupiga deki na kupunzisha tumbo, utumbo, ini na mafigo ni kwa kuacha kula, yaani kufunga (fast) kwa masaa 12 mfululuzo kila wiki mara moja. Kufunga kunasaidia pia mwili kuzoa na kuchoma sumu na takataka nyingi zisizofaa mwilini ambazo ni chanzo cha magonjwa na upungufu wa kinga mwilini. Unaweza kushinda kutwa nzima kwa kunywa maji na kula matunda tu hadi jioni. Kufunga kunasaidia kuchoma chakula na mafuta yaliyozidi mwilini. Hata wazee wetu wa zamani walifahamu uhusiano uliopo kati ya kufunga na afya. Mfano, waislamu wanatakiwa kufunga siku 36 kila mwaka (Ramadhani), hii ni sawa na kufunga siku 1 kwa kila siku 10 wakichanyanya na kufunga suna inakuwa siku 1 kwa kila siku 7. Wakristo wanatakiwa kufunga kwa lazima siku 40 kwa mwaka, hii ni sawa na kufunga siku 1 kwa kila siku 9, wakichanganya na kufunga kwasababu ya maombi yao binafsi inakuwa sawa na kufunga siku 1 kila siku 7. Wanafahamu kuwa hata Mungu alifanyakazi siku 6 na ya 7 akapunzika, bila shaka alipunzika hata kula. Hii inaonyesha kuwa wazee wetu walikuwa na elimu kubwa sana kuhusu vyakula na afya. Walijua kuwa kufunga kunawasaidia kuondoa vitambi na magonjwa kama pressure, kisukari, ugumba, uhanithi, moyo na unene. Hebu wafuatiliwe watu wote wenye tabia ya kufunga kila wakati utagundua kitu hapo. Kama wewe una presure, kisukari, ugumba, au uhanithi (kuishiwa nguvu za kiume) dawa yako kubwa kuliko zote ni kufunga mara kwa mara na mazoezi. unaweza kufunga mchana na kunywa maji na matunda tu.

Nakushauri ndugu yangu na wewe jifunze kufunga kila mara ili uboreshe afya yako, kufakamia kama nguruwe kila wakati sio deal. Kitambi, matako, mapaja na shingo dalili ya magonjwa pressure, stroke, moyo, mafigo, kisukari na mifupa siku za usoni, acha, cha, cha sio afya.

From now ntakuwa nafunga angalau mara moja kwa week, thank's 4u'r advice.
 
Hapa unatoa Ushauri visichanganywe pamoja.
Ushauri: Kuhusu kula vyakula vya Carbohydrates na Protini: Usichanganye kwa wakati mmoja makundi haya mawili ya vyakula kwenye mlo mmoja li kuurahisishia mfumo wako wa chakula katika kusaga chakula ulichokula.

Hapa tena unashauri viliwe pamoja.
c) Kula vyakula vya carbohydrates na proteins pamoja na mboga za majani (greens) ili kuboresha usagaji na ufyonzwaji wake.

Unatuchanganya mkuu sasa,tuchanganye au tusichanganye? Maana mtaani wali nyama,ugali maharage ndio vyakula vikuu.
 
Hapa unatoa Ushauri visichanganywe pamoja.

Hapa tena unashauri viliwe pamoja.

Unatuchanganya mkuu sasa,tuchanganye au tusichanganye? Maana mtaani wali nyama,ugali maharage ndio vyakula vikuu.

pole kwa kuchanganyikiwa lakini meseji ilikuwa kwamba Nyama + greens au carbohydrates + greens vinaweza vikaliwa pamoja bila kuleta shida, ila nyama + carbohydrates ni shiiida!
 
Mara kuleni matikiti kwa tahadhari, mara funga, mara kuleni protini na kabohaidreti mara mbogamboga... Mantiki ipo wapi hapa?? Anyway, ushauri mzuri mwenye macho na aone.
 
pole kwa kuchanganyikiwa lakini meseji ilikuwa kwamba Nyama + greens au carbohydrates + greens vinaweza vikaliwa pamoja bila kuleta shida, ila nyama + carbohydrates ni shiiida!

Shukrani mkuu mtaani kula ugali/wali na mboga za majani unaonekana umefulia na pia kula nyama na mboga za majani hazishibishi.
 
Mara kuleni matikiti kwa tahadhari, mara funga, mara kuleni protini na kabohaidreti mara mbogamboga... Mantiki ipo wapi hapa?? Anyway, ushauri mzuri mwenye macho na aone.

Kazi unayo, Kukataa kwako kubadilika namna ya kula hakutafuta ukweli kuhusu vyakula na magonjwa yanayosababishwa na ulaji mbaya wa vyakula. Ninachokifanya mimi hapa ni kurudisha hisani na kutoa ahsante kwa wananchi kwa kunisomesha kwa kodi zao ndani na nje ya nchi kwa kuwarudishia bure japo elimu kidogo ya nilichokipata, na huo ndio mchango wangu kwao na kwako. Vinginevyo, tutaonana wodini ukiwa na pressure, ugumba, uhanithi, stroke, shida ya kisukari au moyo kwa hela nyingi sana, hasa baada ya umri wako kufikia miaka 40 na kuendelea. Chini ya miaka 40 habari za namna ya kula vyakula inaonekana kuwa ni porojo za saa za jioni, samahani sana mkuu kwa kukuchanganya na uzi huu.
 
Shukrani mkuu mtaani kula ugali/wali na mboga za majani unaonekana umefulia na pia kula nyama na mboga za majani hazishibishi.

Kweli hiyo, lakini wajiulize kwani nyani na ngedere wana hela gani mbona wanaishi porini bila kulalamika kisukari, pressure, stroke, na mafigo? Huko vijijini je mbona hela hakuna lakini matukio ya stroke na visukari ni machache sana? Ukweli ni kwamba vijijini wanakula mboga za majani nyingi na kula nyama kidogo sana siku za sikukuu za Eid na Krismas tu. Wanafunga sana kwa kukosa chakula na kufanya mazoezi sana bila ya hiari yao.
 
Back
Top Bottom