Kuleni Tikitimaji (Water Melon) kwa tahadhari

Ushauri: Kuhusu kula vyakula vya Carbohydrates na Protini: Usichanganye kwa wakati mmoja makundi haya mawili ya vyakula kwenye mlo mmoja li kuurahisishia mfumo wako wa chakula katika kusaga chakula ulichokula.
Kwa hiyo tukila ugali tule ugali mkavu, tukila nyama tutafune kitoweo peke yake, na ukiagiza chai ya maziwa (protini) na chapati (wanga) basi ule unywe chai ya maziwa kwanza umalize halafu usubiri baadae uanza kutafuna chapati peke yake.... ukikabwa???

I mean, if I said this professional advice is wrong it would be an understatement of a century, I mean this is a colossal absurdity. Tumefundishwa ku conserve vitoea, nchi yetu bado ni masikini mno kutuambia tuanze tabia za kutafuna vitoeo!
 
Mkuu kavulata hivi kula mchemsho wa kuku aliyechemshwa na ngozi yake lakini kutokula ngozi yake na kula mchemsho wa kuku aliyetolewa ngozi kabla ya kuchemshwa kuna usalama sawa kiafya?
 
Mkuu kavulata hivi kula mchemsho wa kuku aliyechemshwa na ngozi yake lakini kutokula ngozi yake na kula mchemsho wa kuku aliyetolewa ngozi kabla ya kuchemshwa kuna usalama sawa kiafya?
Ngozi ya kuku ina mafuta mengi (cholesterol) yasiyotakiwa kuwa mengi mno mwilini, kama utaacha kula ngozi yake ina maana utapunguza kiasi cha cholesterol (rehemu) yako mwilini inayosababisha magonjwa ya moyo (coronary heart diseases) na pressure (Cardiovascular diseases). Kama unaweza toa ngozi ya kuku kabla ya kuichemsha ili kupunguza mchuzi wenye mafuta mengi ni sawa, kukwepa kuila baada ya kupika pia ni sawa, kitu kikubwa hapo ni kwamba ngozi ya kuku ina rehemu nyingi.
 

Hii sio amri kuwa kila mtu lazima ale hivyo lahsha! hapa tunajaribu kujibu matatizo ya wananchi ya vitambi, magonjwa ya moyo, stoke, kisukari, mafigo, ugumba na uhanithi ambayo yanazidi kuongezeka ndani ya jamii zetu. Zamani magonjwa haya yalikuwa yako ulaya na Marekani zaidi lakini sasa yameivamia jamii yetu na wanajamii hawajui cha kufanya juu ya kadhia hii. ndani ya jamii wanajitokeza matapeli na wajanja wachache ambao wanatumia ujinga wa wananchi kuhusu vyakula na afya zao kuwadanganya kuwa wanaweza kutibu shida zao (kisukari, pressure, mafigo, uhanithi, ugumba, n.k) kwa kutumia vyakula na kulipa hela nyingi sana kwao ili wapate nafuu. Mimi hapa najaribu kutibua janja yao kwa kuwapa bure wana jf elemu kuhusu the general rules za vyakula na magonjwa. Najua wako wanaochukia kwa kuwafumbua macho wananchi lakini potelea mbali Mungu atajua.

Back to your concerns: Nilianza kwa kusema kuwa ugali/wali, n.k unaweza kuliwa pamoja na legumes and vegetables comfortably kutokana na sababu za kisayansi kuhusu food digestion (carbohydrates) processes. Nikasema nyama pia kutokana na mahitaji yake katika usagaji tumboni inaweza kuliwa pamoja na vegetables (greens) bila kuhitaji mashariti ya ziada. Lakini nikasema pia class 1 protein ukiila pamoja na starches/carbohydrates vitakinzana kwenye digestion yake, na hii sio mimi ila ni sayansi ya darasa la sita tu la usagaji wa protein na carbohydrate na mimeng'enyo gani na mazingira gani yanayohitajika. Rudi kule kwenye biology yako ya chini kabisa ukaone namna vyakula mbalimbali vinavyosagwa, kufyonzwa, kusambazwa na kuunguzwa na kuhifadhiwa (glucogenesis and glycolysis) mwilini. Hata leo uliza ni watu wangapi wakinywa maziwa au chai ya maziwa wanapata shida utagundua wako wengi sana ingawa hawajui kwanini inakuwa hivyo. Wako watu wengi hii leo wakila nyama, mayai au samaki wanapata shida nyingi sana lakini hawajui ni kwanini inakuwa hivyo, lakini hakuna mtu atakwambia kuwa nina allergy na ugali, mchicha, wali, nyegere, mgagani, maharagwe, mnavu, n.k kwanini? hii inaonyesha kuwa chakula cha asili ya binadamu ni mimea sio nyama na mazao yake.

Wewe binadamu make up yako kuanzia dental formular, utumbo na umbo lako havikutayarishwa kula nyama ila tunalazimisha tu kula nyama kwa kuipika na kuichoma ili ilainike ndo maana wala nyama nyingi wote bila mpangalio wana shiida fulani, kama kwa sasa hawana basi wasubiri baada ya kutimiza miaka 45-50+. I know that it is dificult for you to change your eating behavour, however, be informed of food combinations knowledge then eat knowingly. Unaweza pia uka google tu kuhusu "food combinations" or "mixing foods for digestion" or bad food mixing" huenda ukaambulia chochote ndugu yangu katika afya na jf.
 
Thanks...mi ndio maana sili kabisa usiku...ila nakula vizuri asubuhi na mchana...

Ila hapo kwenye kula kiporo cha ubwabwa asubuhi hapo siyo kabisa...nilisikia kwa mtaalamu mwingine kuwa kinaleta kitambi ...nimesahau maelezo lakini yanahusiana na kuwa hata upashe vipi ni cha baridi huwezi linganisha na wali fresh...hivyo hakisagiki vizuri...tokea nisikie nimekipigia ex...
 

Kwahiyo kazi ya friji itakuwa ni nini kama hutaki kula kiporo? jiongeze kidogo. Ila kiporo kilichoachwa nje ya friji huwa kinachacha, na siku zote chakula kilichochacha ni rahisi sana kumeng'enywa na tumbo na kutoa calories nyingi
 
naomba uniambie kazi ya tikiti maji katika mwili kwsb wengi wanasema ni dawa sasa sijui ni dawa ya nini
 
Kazi ya friji kumbe ni kuweka viporo...thanks nimejiongeza...

Kwahiyo kazi ya friji itakuwa ni nini kama hutaki kula kiporo? jiongeze kidogo. Ila kiporo kilichoachwa nje ya friji huwa kinachacha, na siku zote chakula kilichochacha ni rahisi sana kumeng'enywa na tumbo na kutoa calories nyingi
 

Hakuna maziwa kwa ajili ya adults duniani, maziwa yoooooote ni kwa ndama na watoto wachanga basi, watu wazima tunapokunywa chai ya maziwa tunafoji tu, ndiyo maana wengi wao yanawatoa nishai wakiyanywa, hivyo hivyo hakuna nyama kwa chakula cha binadamu binadamu anapokula nyama anafoji tu ndio maana wako watu wakila nyama wanapata gout, allergy na madhara mengine. Hata pale kwenye bustani ya Eden walikokuwa Adam na Eva hapakuwa na nyama bali mimea na matunda tele. pole sana kama ninakukwaza kwa elimu hii kwa umma lakini ukweli ndo huo. Kitambi, matako, mapaja na miguu (usafiri) mkubwa utakubeba kwenye mipango yako kwa muda mfupi, lakini baada ya umri wa miaka 40 na kuendelea kitambi, matako, mapaja, miguu na uzito mkubwa vitakuwa balaa kwako badala ya kuwa sifa na uzuri. Utakuja kuitafuta hii thread wakati ikiwa imeshafutwa na haipo tena jf. Wale Ma-Rastafari na vegetarians huwa hawali nyama kabisa, umeshawahi kuwauliza kuwa huwa wanakula ugali/wali na nini?
 
kavulata, hapo kwenye kufunga, je? ukifunga bila kula chochote kwa masaa 12 ni sahihi? I mean, bila kunywa maji wala matunda. Na kama si sahihi, athari zake ni zipi? na kama ni sahihi faida zake ni zipi?
 
Last edited by a moderator:
kavulata, hapo kwenye kufunga, je? ukifunga bila kula chochote kwa masaa 12 ni sahihi? I mean, bila kunywa maji wala matunda. Na kama si sahihi, athari zake ni zipi? na kama ni sahihi faida zake ni zipi?

Tumboni kuna madawa makali sana yenye uwezo wa kuunguza na kuua vijidudu, kuchoma kuta za tumbo na utumbo na hata kugandisha maziwa fresh na kugeuka mtindi kwa sekunde chache tu. Kemikali hizi huwa zinazuiwa zisiharibu kuta za tumbo na utumbo na uwepo wa chakula tumboni, bila kuwepo chakula tumboni kemikali hizi zinaweza kuharibu mfuko wa tumbo na utumbo na kusababisha vidonda vya tumbo (ulcers). Hata wazee wa zamani wanalijua hili, ndiyo maana kabla ya kufunga wanaanza kwa kula daku alfajiri ili kuepusha majanga kama hayo, hata hivyo pamoja na kula daku wako watu wengi waliopata vidonda vya tumbo (gastric au duodenal ulcers) kwasababu ya kufunga. Ndo maana hapa mimi nakushauri unywe maji na matunda ili kuukinga ukuta wa tumbo usijekuunguzwe na kemikali kali za tumboni na kupata vidonda vya tumbo.
 
naomba uniambie kazi ya tikiti maji katika mwili kwsb wengi wanasema ni dawa sasa sijui ni dawa ya nini

Tikiti maji lina maji mengi sana na sukari vinanayosaidia kazi mbalimbali za mwili, ukila tikiti utakuwa na uhakika wa kujiongezea maji na sukari mwilini kwako. Lakini pia tikiti lina makapi (nyuzi) mengi ambayo yanakusaidia kupata choo laini na hata kuzuia kansa za tumboni na utumbo. Lina vitamin C na madini mengi kama vile Potassium, Mg, Ca, P ambayo ni muhimu sana mwilinini. mbegu zake zinasemekana kuwa zina madini ya Zinc (Zn) yanayosaidia sana kwenye uimarishaji wa kinga ya mwili, hivyo usiteme mbegu. Lakini pia watu wenye vidonda vya tumbo na acid nyingi tumboni wanashauriwa kula matunda kama tikiti, tango, parachichi badala ya machungwa, pasions na mengine makali ili kupunguza uchachu tumboni.
 
Kazi ya friji kumbe ni kuweka viporo...thanks nimejiongeza...
He kumbe wewe unaweka nini kwenye fridge bana! mimi naweka humo viporo vya maharagwe, matunda, ubwabwa, soda, juice, bia, samaki, n.k ambavyo nimeshindwa kuvila na kuvimaliza leo ili nikutane navyo tena kesho hata keshokutwa. Sasa kama umeshindwa kula leo chakula hadi kikifika kesho si kitakuwa kiporo cha wali, bia, soda, maharagwe, nyama, samaki, juisi, n.k? Kumbuka hata Rais alimuweka kiporo Mh. Muhongo kabla hajajiuzulu mwenyewe. Hivyo kiporo ni kitu chochote kinachoachwa leo ili kiliwe kesho.
 
Aisee sipiki zaidi ya mahitaji ya familia...hii ndio formular ya nyumbani kwangu...kikibaki kinamwagwa...sijazi makorokocho kwenye friji...nijuavyo friji ni kwa ajiri ya raw foods...yani nile frozen kabisa kisa nini ? na save gesi au?

 
Aisee sipiki zaidi ya mahitaji ya familia...hii ndio formular ya nyumbani kwangu...kikibaki kinamwagwa...sijazi makorokocho kwenye friji...nijuavyo friji ni kwa ajiri ya raw foods...yani nile frozen kabisa kisa nini ? na save gesi au?

Ok, huo ni utawala wako wenye utaratibu huo, ila wako wanaonunua mafriji, deep freezers, microwaves, thermos, n.k kwaajili ya kuhangaikia viporo viweze kutumika tena bila kuleta madhara. Lakini kama unaweza kula chakula fresh ni vema sana.

Kanuni muhimu kuhusu vyakula ni:
1. Nafaka ziliwe bila ya kukobolewa
2. Kupika vyakula kunaharibu ubora wa vyakula (tafuta na kula vyakula vinavyoweza kuliwa vibichi kama mihogo, asali, mboga n.k)
3. Kula tunda lenyewe badala ya kukamua juice
4. Tumia mbegu zenye mafuta badala ya kuyakamua mafuta kutoka kwenye mbegu hizo
5. Nunua vyakula vilivyohifadhiwa kwenye mazingira mazuri
6. Kula chakula mara moja baada ya kupikwa (usipende kula viporo)
7. Pasha vizuri chakula kiporo kama ni lazima ule kiporo
8. Funika vizuri chakula kama utalazimika kuchelewa kukila
9. Nawa mikono kabla ya kula
10. Pika/choma nyama hadi iive vizuri (kama ni lazima ule nyama)
 
Hata pale kwenye bustani ya Eden walikokuwa Adam na Eva hapakuwa na nyama bali mimea na matunda tele.
Kwanza habari za Adam na Eva na Bustani ya Eden and such hazihusiki katika mada ya kisayansi kama hii. They just do not go together, please!

Lakini, tuki assume kwamba sababu zako za kutokula nyama ni za kitaalam, well, Wahindi hawali nyama, lakini wanaishi maisha mafupi kuliko Westerners na nyama zao. How you explain that, Mr. Vegan?
 

Achana na wahindi kabisa wewe dugu yangu, wahindu wengi hawali nyama lakini wana tabia ya kula kupita kiasi animal products kama vile maziwa na jibini (animal fat), pia wanakula sana sukari na sweets (halua, n.k) bila kufanya mazoezi ya kutosha hivyo kusababisha kuwa wanene sana na kuyafanya maisha yao yawe kama unavyosema wewe. Hivyo kwa tabia yao hiyo wengi wao huwa wana shida ya unene, mifupa, kisukari, pressure, mafigo, kansa, stroke na maradhi ya moyo kulikosababisha wawe na hospitali na wataalamu wengi wa magonjwa ya moyo. Lakini pia kuna tatizo la genetic pool kwa magonjwa hayo, wengi wao wanarithi pia magonjwa hayo kutoka kwa vizazi vyao.

Lakini kama ukifika Marekani (western) leo utaifuta kauli yako hiyo kwani huko ndiko utawakuta watu wenye kisukari, pressure, kansa, stroke, shida za moyo, mafigo na unene kupita kiasi ambao maisha yao pia sio marefu ki vile, hali iliyosababisha kila daladala lao liwe na sehemu maalum kwa wagonjwa hao wenye matatizo ya lishe mbaya wanaotumia wheel chairs. Hii inasababisha watu wenye hela (matajiri) waachane na kula nyama kabisa siku hizi huko Western unakosema. Nyama zinabaki ni kwa watu masikini sana na wanajeshi wao tu.

Eden: Kama nyama kingekuwa miongoni mwa vyakula vizuri na vitamu saana kwa binadamu tungesoma na kusikia kuwa pale kwenye bustani ya Eden kulikuwa na nyama choma, michemsho, makange na roast za kila aina kwaajili ya Nabii Adam na mkewe Hawa. Lakini tunaambiwa palikuwa na matunda matamu ya kila aina kwenye bustani zile. Kumbuka kuwa viumbe vyote vinavyotakiwa kula nyama huwa vina sifa zifuatazo:

1. Meno yao ya mbele (canies) yamechongoka
2. Wana utumbo mfupi sana kuliko binadamu na wanyama wengine wasiotakiwa kula nyama ili kurahisisha chakula kisikae sana tumboni
3. Wanapata chakula chao kwa kukimbia sana (hii inawasaidia kufanya mazoezi makali na kuunguza mafuta ya ziada kwenye miili yao)
4. Wana kucha kali
5. Wanakimbia kwa kasi kuliko wanyama ambao ni chakula chao
6. Wana tabia ya kupunzika kabisa wakishakula chakula chao (nyama) bila kula vyakula vingine tena hadi baadaye sana
 
Yes nakula donor natengeneza mwenyewe...nachanganya ngano na mahindi vyote visokobolewa...naosha tu...
Yes kwangu these days sinywi juice nakula matunda...

Na siku hizi (more than a year) situmii sukari wala maziwa...(watoto wangu sababu ni wadogo wao siwazuii hili...ila mume wangu naendelea kumshauri aache sukari...)

Soda nimeachana nazo...nakunywa maji ya kutosha ili nisichanganye kiu na njaa...na mwili wangu ni mzuri na wala situmii diet yoyote zaidi ya mazoezi ya indoor (tena chumbani)


Nina utundu sana wa kusoma articles za lishe though kuna lots of info ambazo zinakinzana...

kabla sijala najiuliza nilacho kina faida na hasara gani mwilini mwangu...nimeepuka vyakula vingi viso na mpango kwa kujiuliza huku...kama ma chocolate sijui ma keki...etc...

 
Namba 6 mbona mwenyewe unasema 'usipende kula viporo' afu unanishangaa mimi kutokula viporo...je unasoma unachoandika au umekikurupua mahali?

Kumbuka nimesema sili viporo sababu ya knowledge niloipata mahali kuwa si vizuri...wewe ukaanza kuni criticize....sasa hapa na wewe unakubali kuwa si vizuri...

Mimi huwa nasoma side effects na kuzisahau...lakini nachukua conclusion kuwa hiki ni kibaya...viporo ni vibaya...hata kama maelezo nimeyasahau...

Kama wanavyosema sousage ni mbaya...sikumbuki why lakini sili tena sousage...(nakumbuka kidogo kuhusu too much salt...sijui na nini)

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…