Kwanza habari za Adam na Eva na Bustani ya Eden and such hazihusiki katika mada ya kisayansi kama hii. They just do not go together, please!
Lakini, tuki assume kwamba sababu zako za kutokula nyama ni za kitaalam, well, Wahindi hawali nyama, lakini wanaishi maisha mafupi kuliko Westerners na nyama zao. How you explain that, Mr. Vegan?
Achana na wahindi kabisa wewe dugu yangu, wahindu wengi hawali nyama lakini wana tabia ya kula kupita kiasi animal products kama vile maziwa na jibini (animal fat), pia wanakula sana sukari na sweets (halua, n.k) bila kufanya mazoezi ya kutosha hivyo kusababisha kuwa wanene sana na kuyafanya maisha yao yawe kama unavyosema wewe. Hivyo kwa tabia yao hiyo wengi wao huwa wana shida ya unene, mifupa, kisukari, pressure, mafigo, kansa, stroke na maradhi ya moyo kulikosababisha wawe na hospitali na wataalamu wengi wa magonjwa ya moyo. Lakini pia kuna tatizo la genetic pool kwa magonjwa hayo, wengi wao wanarithi pia magonjwa hayo kutoka kwa vizazi vyao.
Lakini kama ukifika Marekani (western) leo utaifuta kauli yako hiyo kwani huko ndiko utawakuta watu wenye kisukari, pressure, kansa, stroke, shida za moyo, mafigo na unene kupita kiasi ambao maisha yao pia sio marefu ki vile, hali iliyosababisha kila daladala lao liwe na sehemu maalum kwa wagonjwa hao wenye matatizo ya lishe mbaya wanaotumia wheel chairs. Hii inasababisha watu wenye hela (matajiri) waachane na kula nyama kabisa siku hizi huko Western unakosema. Nyama zinabaki ni kwa watu masikini sana na wanajeshi wao tu.
Eden: Kama nyama kingekuwa miongoni mwa vyakula vizuri na vitamu saana kwa binadamu tungesoma na kusikia kuwa pale kwenye bustani ya Eden kulikuwa na nyama choma, michemsho, makange na roast za kila aina kwaajili ya Nabii Adam na mkewe Hawa. Lakini tunaambiwa palikuwa na matunda matamu ya kila aina kwenye bustani zile. Kumbuka kuwa viumbe vyote vinavyotakiwa kula nyama huwa vina sifa zifuatazo:
1. Meno yao ya mbele (canies) yamechongoka
2. Wana utumbo mfupi sana kuliko binadamu na wanyama wengine wasiotakiwa kula nyama ili kurahisisha chakula kisikae sana tumboni
3. Wanapata chakula chao kwa kukimbia sana (hii inawasaidia kufanya mazoezi makali na kuunguza mafuta ya ziada kwenye miili yao)
4. Wana kucha kali
5. Wanakimbia kwa kasi kuliko wanyama ambao ni chakula chao
6. Wana tabia ya kupunzika kabisa wakishakula chakula chao (nyama) bila kula vyakula vingine tena hadi baadaye sana