Kuliko Bilion 34 kujenga soko Kariakoo bora soko lihamishwe

Kuliko Bilion 34 kujenga soko Kariakoo bora soko lihamishwe

instagram

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
2,118
Reaction score
4,863
Inaonekana watu wa mipango miji wamelala na viongozi wetu akili zimeganda. Nimeona leo kwamba soko la k'koo litajengwa upya kwa Billion 34, leo siyo mwaka 1970 jamani kwanini pesa zote zitumike kujenga soko tena eneo lenye tatizo la msongamano wa watu badala ya kulihamisha soko pembezoni mwa mji? Au wazanzibari wao kila kitu wanataka kiwe karibu na feri ili wakitoka Zanzibar wasipate usumbufu[emoji23]? Maana naskia tena kuna mradi mwingine wa soko la jangwani[emoji26][emoji26].

Mimi nazani tuachane na hili soko la kariakoo tena serikali ingetumia opportunity hii kujenga mradi wa kuwezesha kariakoo kupumua kwa kubomoa lile soko na kupanda miti eneo lile na kutengeneza city park yenye bustani na benchi za watu kupumzika. Itungwe sheria iundwe mamlaka ya City park Authority ya kusimamia mambo haya kwenye miji yetu ipendeze. Tuache fikra kwamba kila eneo lazima lijengwe mji ule hauna hata sehemu ya kupumzika, mtalii akienda k'koo leo hii hakuna hata sehemu ya kupumzika labda ale chips sehemu ambayo imejaa joto la moshi wa jiko la mkaa na hewa ya mafuta ya kukaanga.

Kwanini bado serikali inakaa na kuwaza kujenga jenga sehemu yenye msongamano hata parking za magari hakuna badala ya kujenga miradi ya kuboresha changamoto za mji kama kujenga jengo la parking pale kwenye soko japo mimi ningetamani pasijengwe chochote ipandwe miti tu pale mji upumue.

Leo tunataka kufanya makosa yaleyale ya kujenga mwendokasi jangwani kwa kujenga soko jingine pale la wamachinga badala ya kujenga daraja flyover la kutoka magomeni kwenda faya au interchange ya kutoka magomeni kwenda faya kwenda salender kwenda karume na kupanda miti mirefu ya misitu jangwani ili kusaidia joto la mji kupungua.

Ukizingatia eneo la jangwani ndiyo aneo peke kwenye mji wa dar es salaam lenye unapana wa kutosha ndani ya jiji lenye kutosha kujenga 4 tier interchange ambazo kwa Africa ziko mbili tuu, moja iko Ghana na nyingine iko South Africa.

Yani pale inasukwa interchange moja matata sana kono moja linaenda faya kono jingine linaenda magomeni, kono jingine linasambaa hadi salender , kono jingine linasambaa hadi mitaa ya ilala karume, kono jingine linakatiza hadi kinondoni studio au nyuma yake pale.

Hela tunazo invest kwenye mavitu yasiyo na kichwa (madege, ma dreamliner) tunaweza tukatoa kitu cha maana sana pale jangwani chenye kupunguza changamoto nyingi sana za mji na kutujengea heshima kubwa sana kama jiji.

N:B Yani kwa asiyeelewa umuhimu wa misitu katikati ya mji ni kwamba binadamu tunazalisha kiwango kikubwa sana cha Co2 gases kwa tunavyopumua na moshi wa magari na viwanda, pia majiko tunayopikia ya mkaa sasa jiji linakuwa na hewa chafu sana ya co2 sasa wenzetu kama hongkong wamezungusha misitu kwenye jiji lao ili kuthibiti kiwango kikubwa cha Co2 gases kwa sababu misitu inanyonya gesi za Co2 na ku release gases za Oxygen hivyo kusaidia mji kuwa Na hewa safi na kusaidia ubongo kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. Kinyume chake ni sisi hapa.
View attachment 1999008
 
Una chuki na wamachinga eh!!?

Nchi ni yetu sote, nenda Hong Kong kawaulize wanapumlia wapi kalafu uliza maendeleo yao then njoo na porojo zako.
Wewe hongkong hujaona kuna misitu? Wamachinga siyo lazima walundikane sehemu moja k'koo mji umekuwa kuna vitongoji vingi sana vya kuwasambaza hata tegeta, mbezi, kinyerezi, mbagala kuna wamachinga kwani lazima kariakoo?
 
Una chuki na wamachinga eh!!?

Nchi ni yetu sote, nenda Hong Kong kawaulize wanapumlia wapi halafu uliza maendeleo yao then njoo na porojo zako.
Wanapumulia wapi? Unapajua hongkong wewe kweli?
images%20(2)%20(1).jpg
 
Wewe hongkong hujaona kuna misitu? Wamachinga siyo lazima walundikane sehemu moja k'koo mji umekuwa kuna vitongoji vingi sana vya kuwasambaza hata tegeta, mbezi, kinyerezi, mbagala kuna wamachinga kwani lazima kariakoo?
Hahahaha, we jamaa!! Misitu Hong Kong!!?
 
Bongo sihami maana patam sana.Kumbe ule moto ulio wafanya watu masikini sijui kwa nn msingewaambia wahamishe vitu vyao kuliko hasara na presha hata kufa huko waliko[emoji24][emoji24][emoji24]
 
Kama huo ndo misitu basi sis tunayo ya bonde la muhimbili
Sasa muhimbili ni msitu au swamp. Hongkong kuna msitu mkubwa na wajapani walitumia msitu huo katika vita vya dunia mwaka 1941 kumtandika muingereza hadi muingereza aka surrender na japani ikaitawala hongkong kwa miaka mitatu Hadi ilipo surrender na kuiachia hongkong kwa utawala wa muingereza. Wewe unajua nini.
 
Kumbe ule moto ulikuwa project ya watu wachache ili kuja na kitu hiki. Poleni sana mliopoteza mali zenu
 
Ukizingatia eneo la jangwani ndiyo aneo peke kwenye mji wa dar es salaam lenye unapana wa kutosha ndani ya jiji lenye kutosha kujenga 4 tier interchange ambazo kwa Africa ziko mbili tuu, moja iko Ghana na nyingine iko South Africa

Yani pale inasukwa interchange moja matata sana kono moja linaenda faya kono jingine linaenda magomeni, kono jingine linasambaa hadi salender , kono jingine linasambaa hadi mitaa ya ilala karume, kono jingine linakatiza hadi kinondoni studio au nyuma yake pale.

Hela tunazo invest kwenye mavitu yasiyo na kichwa (madege, ma dreamliner) tunaweza tukatoa kitu cha maana sana pale jangwani chenye kupunguza changamoto nyingi sana za mji na kutujengea heshima kubwa sana kama jiji.

offset_771279.jpg
 
Inaonekana watu wa mipango miji wamelala na viongozi wetu akili zimeganda. Nimeona leo kwamba soko la k'koo litajengwa upya kwa Billion 34, leo siyo mwaka 1970 jamani kwanini pesa zote zitumike kujenga soko tena eneo lenye tatizo la msongamano wa watu badala ya kulihamisha soko pembezoni mwa mji? Au wazanzibari wao kila kitu wanataka kiwe karibu na feri ili wakitoka Zanzibar wasipate usumbufu? Maana naskia tena kuna mradi mwingine wa soko la jangwani[emoji26][emoji26].
Mungu akubari bro una mawazo mazuri sana,na kwahakika ulishatembea nchi nyingi hasa za wenye akili wahusika wamekusikia
 
Mungu akubari bro una mawazo mazuri sana,na kwahakika ulishatembea nchi nyingi hasa za wenye akili wahusika wamekusikia

Una hoja nzuri ila hapo kwa Wazanzibari umekosea sana. Sijui lengo lako ni nini? Tujenge utaratibu wa kujenga hoja bila kutumia maneno yasiyopendeza.

Kimsingi, tunahitaji miji yetu mikubwa kuipanga upya si Dar tu. Dar tunahitaji kuijengea kitovu kipya cha biashara. Hapo kati kati pameelemewa. Hakuna pakumua.

Tujenge kitovu kipya cha biashara cha kisasa kitakachobeba taswira ya kitaifa na Kimataifa. Tuwe na miji mipya ya kibiashara ktk majiji yote. Na Rais aliongea vizuri jana kuhusu suala la mipango miji. Tucheze na lengo la 11 la SDGs kuhusu sustainable cities. Miji yetu iwe na creation area, bustani nzuri, tupande miti na if possible kila kaya ktk miji mikubwa penye nyumba yenye eneo ipande japo miti miwili ya matunda.

Sorry nimemlenga mleta mada si wewe Trondheim Said. Nime quote vibaya.
 
Umeongea vizuri kuhusu Sustainable Cities, ila nimejaribu ku google kama kuna mamlaka yoyote inayoshughulikia mambo hayo hakuna. Kwenye miji iliyoendelea kila mji una mamlaka ya kushughulikia na green cities (City Park Authorities). Uki google Mamlaka kama hizo Tanzania utakutana na Hamidu city park[emoji23].
IMG_20211105_075520.jpg
 
Ujenzi wa soko la kariakoo ulilenga kuhudumia watu kulingana na mahitaji yao miaka hiyo !

Ni muda sasa waje na ujenzi wa soko jipya la kisasa.
 
Rushwa,tamaa,chuki binafsi, siasa ndio inayotusumbua.

Kariakoo ilipangiwa kujengewa kwanza miundo mbinu ya kukidhi ukuaji wa jiji kwa miaka 100,kipindi cha miaka ya 60,na wakati ule Ujerumani Magharibi ikitaka kutufanyia kazi hiyo.Na wakati ule majengo mengi yalikuwa madogo na mengine ya udongo.
Lakini ikaja kuhamisha makao makuu ya nchi kwenda Dodoma ,wakidhani wakihamisha makao makuu,tatizo litapungua au kukoma kabisa.

Mara waliokuwa mabingwa na wachochezi wakutaka Dodoma iwe makao makuu wakarudi kimya kimya Dar.Tukazidi kubanana bila kuweka mikakati mipya ya mipango miji.

Tatizo la serikali zetu ni hawana utashi.
 
Back
Top Bottom