Kuliko Bilion 34 kujenga soko Kariakoo bora soko lihamishwe

Wamachinga hawafuati sheria wanafuata vibe la biashara. Palipo na msongamano wa watu na wao utawakuta ila sio uwapeleke sehemu wasubirie kufuatwa na wateja hiyo hawatokubali. Wao wanafuata wateja wanapokwenda.

Ndio maana maeneo yao ni pembezoni mwa barabara, pembezoni mwa vituo vya daladala, kwenye masoko makubwa, nje na ndani ya stand.

So machinga kimsingi wanafanya biashara katika mazingira ambayo kisheria si rasmi na yanavuruga utaratibu.

Say NO kwa MACHINGA. Tufanye biashara rasmi.
 
Ya ubungo bilioni 200 ,hii itakuwa trilioni 4 tunaweza
Trillion 4 ni pesa ndogo sana. Hivi unajua pesa nyingi sana inatumika kwenye mawizara na taasisi za serikali na impact ni sifuri.

Hiyo pesa tukiokota okota huko tunapata zaidi ya 4 trillions na ni ndani ya maiaka miwili tu.
 
Umesema vitu vya maana sana aseee..tatizo la nchi hii linajulikana sikuzote..ni viongozi wa ccm.

#MaendeleoHayanaChama
Nashindilia hapo shida ni wazee wa CCM na watoto wao na wapambe wao. Hawa inabidi watoke.
 
urafiki pana vibe sana. kumbuka kuna soko la ndizi na mazao mengine pale kuelekea mabibo. ni kwa vile serikali nayo imeelekeza akili zake kariakoo tu. wangepaendeleza pale, pange vaibika kinoma
 
Una chuki na wamachinga eh!!?

Nchi ni yetu sote, nenda Hong Kong kawaulize wanapumlia wapi halafu uliza maendeleo yao then njoo na porojo zako.
Unadhani Hongkong hawana parks? Sha Tin Park? Hamna mji wa maana usio na park. Hata jirani zetu wana Uhuru Park acha Central Park ya New York. Shida yetu tunadhani tukijana maghorofa ndio tutaheshimiwa. Ka Botanical garden ketu kamebanwa mpaka kamekosa pumzi.

Amandla...
 
Una chuki na wamachinga eh!!?

Nchi ni yetu sote, nenda Hong Kong kawaulize wanapumlia wapi halafu uliza maendeleo yao then njoo na porojo zako.
Kwa kweli kariakoo imesongamana sanaa
 
Hongera mkuu...UMEWAZA
 
Uko sawa kabisa ila watu wanakupinga bure Tu. Btw kupinga kuunga hoja ni haki ya ya MTU
 
Uko sawa kabisa ila watu wanakupinga bure Tu. Btw kupinga kuunga hoja ni haki ya ya MTU
Fikiria tumeagiza ndege mpya nne kwa $700 million. Hizo pesa tungejenga ma interchange kama hayo mawili au zaidi. Ila watu wanashobokea ndege ambazo hata hawajui zinaruka wapi. Ila madaraja hayo kila mtu angepita kuwahi foleni ya kwenda kwao mida mibovu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…