Kuliko kununua gari used Bongo bora usubiri uagize tu used Japan

Kuliko kununua gari used Bongo bora usubiri uagize tu used Japan

Laiswa

Member
Joined
Jun 28, 2018
Posts
61
Reaction score
94
Kwa muda nimejaribu kutafuta hivi vigari vidogo kama IST, Vits , Allex nk

Vingi madalali wanauza Mil 10 mpaka 13 almost bei ya kuagiza mil 14 - 16 Japani.

Hapo ukishanunua Bongo jiandae tena na mil 2 za kurekebisha gari angalau uweze kutembelea.

Kwa ushauri tu usikimbilie kununua gari used Bongo subiri ujazie jazie uagize kabisa, uwe na uwakika wa kutuamia angalau miaka 2 bila kwenda garage zaidi ya kumwaga tu oil.
 
Sababu ya kununua za mkononi, ni sawa na ile sababu ya kutoboa exhaust, gari ya CC1500 unataka iungurume kama gari yenye 5.4L, ilimradi kujitutumua tu!

Bajeti ni 15m, anatamani kumiliki SUV, ukizifuata Japan, mpaka unaitembelea hapa mji wa DP World, ni 24m kwa uchache sana.

Sasa anatembezewa Forester, namba T..DXV, anaambiwa 15.8m, anaona ndoto ndo inatimia hivyo, chap analipa.
 
IST used mbona hata 8M unapata ukitaka za kulenga mbona zipo saana tu mkuu
Hata 6m unapata, tatizo safari za garage baada ya hapo zitakuwa nonstop. Tofauti na yule anayeagiza Japan straight, anakuwa na 3yrs ya kuendesha bila kufanya matengenezo ya kuumiza kichwa.
 
Naendelea na utafiti wangu,wapi nitapata Forester XT langu.
 
Unaweza kupata gari nzuri ukitulia hapahapa tz.siku hizi gari ni body engine zipo nyingi na zinatengenezeka . Muhimu utulivu usiwe unahamu kubwa ya kumiliki gari utapigwa. Nenda taratibu huyo anaye kuambia Leo gari milon 10, kesho utashangaa imepostiwa inataka mlioni 8
 
Hapa unachoogopa ni nini? Hata ukiagiza toka jep itafika kipindi tu utawajua mafundi garage. Au la usiliendeshe uliweke ndani.
 
Kwa muda nimejaribu kutafuta hivi vigari vidogo kama IST, Vits , Allex nk

Vingi madalali wanauza Mil 10 mpaka 13 almost bei ya kuagiza mil 14 - 16 Japani.

Hapo ukishanunua Bongo jiandae tena na mil 2 za kurekebisha gari angalau uweze kutembelea.

Kwa ushauri tu usikimbilie kununua gari used Bongo subiri ujazie jazie uagize kabisa, uwe na uwakika wa kutuamia angalau miaka 2 bila kwenda garage zaidi ya kumwaga tu oil.
unafikiri kuna mtu anapenda kununua,ila inabidi,mtu m7 amejichanga kwa jasho na damu,mwaka mzima,ndo kapokea mchezo atafanyaje,na hela kwa sisi extended family haitunziki.
Ila madalali wanaharibu sana biashara,gali la m5,wao wanasema m8,na hawashuki chini ya 7.
 
Hapa unachoogopa ni nini? Hata ukiagiza toka jep itafika kipindi tu utawajua mafundi garage. Au la usiliendeshe uliweke ndani.
Hapo unazungumzia baada ya miaka miwili sasa ndo utanza kuona icho kipind ambacho wengi ndo huanza kuuza sasa magari
 
Shida kubwa Watanzania tunakasumba ya kuangaliwa namba, D au E, unaweza kukuta gari ni namba c au b lakini bado inadai,hii inategemea na matumizi ya mtu. Waswahili wengi wanapouza magari yao Huwa hawasemi ukweli kuhusu tatizo la Hilo gari pia magari mengi ni mazuri Kwa mwonekano lakini hayana service. Kabla hujanunua kagua matatizo yote ya gari harafu tafuta ghrama zake ,SASA unapo nunua hakikisha unabageni mpaka inapatikana Ile Hela ya kwenda kurekebisha matatizo uliyo yagundua, usliltumie kabla hujafanya service. Kwa gari kama Toyota au gari za kijapani sio gharama Sana kufanya service
 
Back
Top Bottom