Kulikoni Kenyata kuzomewa jana bungeni hadi kukaa chini?

Kulikoni Kenyata kuzomewa jana bungeni hadi kukaa chini?

Unafikiri kuzomewa rais kumemshushia heshima kiasi gani katika jamii yake(wananchi wake) unadhani uyo rais baada ya kuzomewa aliathirika kiasi gani kiakili kitu ambacho kinaweza kuchangia kufanya maamuzi ya kitaifa yasiyo na tija kwa taifa?
Kama wanausalama wangegundua hili jambo mapema wangeweza kumuepusha rais na hiyo aibu kwa kuchukua hatua mbadala ie kuahirisha hiyo hotuba (ratiba ) au kuwadhibiti katika vizuizi vya upekuzi magetini kwa kuwanyanganya izo filimbi nk
 
Hii ni aibu sana kwa rais na serikali yake kwa ujumla.pia inaonyesha madhaifu makubwa sana (mnoo) kwa idara yao ya usalama hasa kitengo cha inteligence

Hii si aibu, kaka. Ni demokrasia inavyofaa kuwa.

Sio eti kwa sababu mtu fulani amekupita umri kila kitu asemacho ni ukweli. Kama Wakenya, tunakubaliwa kupinga na kujieleza (kuji-express).

Sio aibu.
 
Back
Top Bottom