Kulikoni Mamalaka ya Huduma za Meli (TASAC) kujilipa posho kwenye vikao vya bodi zaidi ya Tsh milioni 600!

Safari ni ndefu nchi yetu kupata maendeleo. Hapa lazima hatokee kichaa mmoja aanze kuwacharanga kila mhujumu uchumi kwa risasi hata kama ni mjomba wake labda tutaheshimiana. Magufuli aliwalinda watu wake wanaoitwa Sukuma gang akawaumiza watezi wake. Hii ndiyo shida ya hii nchi. Kila ajae atawalinda watu wake na kuwabana wengine. Huu mwendo utaweza kuendelea kwa muda na ndio mfumo wa Afrika anyaway ndiyo maana Afrika tuko Nyuma. Kule Afrika ya kusini shirika la ndege lilikuwa linaenda vizuri tu chini ya GM mzungu. Wakamwondoa wakamweka kamama fulani ambaye ilisemekana ni girlfriend wa mkuu. Hapo ndipo shirika liliharibika na bado wakaendelea kumwachia yule mama aendeshe shirika mpaka shirika lilipokuwa mahututi. Siasa za Afrika ni shida kwelikweli.
 
Hizi hela magufuli alikuwa anajuwa zinakokwenda.
 
Kuna Mzee mmoja anajiita Mkinga, alikuwa mkosoaji sana kila TV utamkuta anachambua mabaya ya serikali, alivyowekwa kwenye hiyo bodi kapumzika anakula posho tu.

Sisi wanyonge tunakanyagana uwanjani kuaga mwili wa mwamba wa Africa.
Kumbe mkinga kelele zote zile wakamua kumweka kwenye bodi ya ulaji kakaa kimyaa?[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kuna tatizo kwenye mifumo yetu. Board members wala sio watendaji kwenye taasisi walau wakikutana Mara 2 au 3 kwa mwaka inatosha kabisa. Mimi nahisi kuna vikao hewa kati ya hivyo 23, watu wameandikia tu wamegawana mpunga
 
Mzee Mkinga alipokuwa na njaa alikuwa anaonge kwelikweli ila aliposhiba kawa kimyaaaa
 
TASAC ni tatizo kubwa sana ktk kuiua bandari yetu ya Dar es Salaam ambayo serikali inewekeza pesa nyingi sana kwenye kuiboresha. Sheria iliyopitishwa mwaka juzi, ambayo imeipa Tasac kuwa agent pekee kwa meli zooote zinazokuja Tanzania, kasoro meli za Container tu, ni sheria kandamizi inayotakiwa kubadilishwa haraka sana.

Haiwezekani mtu ananunua mzigo wake, akija hapa, anaambiwa ni lazima aitumie Tasac kama agent wake, wakati huo huo, TASAC ndiye msimamamizi wa masuala ya bahari, sasa anajisimamiaje yeye mwenyewe?

Bila kusahau, TASAC huyo huyo amepitisha sheria kuwa yeye ndio mkaguzi wa mizigo yote inayoshuka bandarini, tena ikiwa imeweka rate za juu sana ambazo inaifanya bandari yetu inakuwa ghali zaidi.

Ni wakati muafaka sasa sheria ya Mandatory agency to Tasac ipelejwe bungeni na kubadilishwa, ili wenye mizigo wawe na uhuru wa kuchagua / appoint agent wanayemtaka kusimamia mizigo yao.

Kwa jinsi mifumo ya TRA (Tancis), TPA, na wao wenyewe TASAC wabaki kuwa Tallying company, ili kuhakikisha seriki haipotezi mapato yake, lakini sio Tasac kuwa agent pekee, wawekezaji wanaikimbia bandari ya Dar es Salaam, sababu ya urasimu wa kuwa na agent mmoja tu, ambaye anafanya anavyotaka yeye, kwa kuwa mteja hauna uamuzi wa kuchagua agent unayemtaka.

Msigwa, lifikishe hili kwa Mh. Rais aliangalie kwa upya.

Kitendo cha Tasac kuwa ndiye agent pekee kinaondoa ufanisi na uwanibikaji, maana wanajua wateja hawana option. Na hii ni kumnyima mteja uhuru wa kuchagua na kuua ajira ya makampuni hinafsi ya uwakala wa meli (hadi sasa, kampunj zaidi ya 10, zilizokuwa zimeajiri maelfu ya watanzania zimefungwa)..... pia ni sawa na kusema watu wote ni lazima watumie line za TTCL tu kwa mawasiliano, hayo makampuni mengine yatafanya nini? Mteja anakosa uhuru anapopata huduma mbaya ya kuhama na kwenda kwa mtoa huduma mwingine

Yunaomba sana mama, hili la TASAC kuwa kila.kitu bandarini liangaliwe kwa upya ni sheria irelebishwe haraka sana, kama kqeli tunataka kufanikiwa.

Haiwezeni TASAC huyoguyo ni:-
1) Msimamizi na mdhibiti wa masuala ya baharini na mtoa leseni
2) Wakala wa meli (Shipping Agent)
3) Wakala wa Forodha (Clearing Agent)
4) Tallying Company (mandatory)
5) and all others

Huu ni urasimu unaoua bandari yetu.
 
Kabla ya kuanzisha TASAC, je serikali ilipitia na kujiridhisha kama,wanaleta zao linalochanua au waliutengeneza kwa madhumuni ya watu wachache?
Shipping haina siasa mambo ya kuokota watu nje ya professional itaendelea kutugharimu.
 
Ila si wanatoa gawio serikalini mbona mistake kidogo maneno kibao wabongo TASAC ni best katika kutoa huduma zao maana wanafanya kwa commitment kubwa kuliko hao wengine na swala la bodi madudu yashajulikana soon inaweza kuvunjwa na mkurugenzi mpya kashateuliwa

We ujue katika clearing and forwarding TASAC ni professional acheni hayo makampuni yenu ya kihindi ndo yamejaa huku posta kunyanyasa wafanyakazi tu ishu ni bodi inaweza kuvunjwa mda wowote ule

Wameajiri maelfu ya watu waivunje ili iweje acheni zenu kaeni mtulie
 
Wataka kusema kampuni za private zimefungwa kisa TASAC [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]mbona zipo izo ni kuyumba kwa biashara kumbuka Tasac wana tunzo ya huduma bora kingine baadhi ya items nyingi hao private hawawezi kuact kama maagent wa kuondoa shehen zao watu wako kisheria na rate imepungua ni affoidable

Uitoe tasac atakaye ratibu usalama wa vyombo vya majini ni nan

Kuharibu bodi tu ndo unaongea yote haya[emoji1787][emoji1787][emoji1787]na LATRA je utasemaje
 
Kuna tatizo kwenye mifumo yetu. Board members wala sio watendaji kwenye taasisi walau wakikutana Mara 2 au 3 kwa mwaka inatosha kabisa. Mimi nahisi kuna vikao hewa kati ya hivyo 23, watu wameandikia tu wamegawana mpunga
Bodi ni tatizo sana kuivunja wanaleta kiwingu pesa wanshapata kwanza mazee hayana jipya kuleta ujuaji

Mama kacheza kama pele huyo mkurugenzi mpya ni kijana na alivyotishwa na ni mtu wa mungu sana anaonekana ni shekhe mzuri tu anaweza kubadilisha sana ila asiendelee na bodi ile wale washakuwa nunda kuwatimua tu wanaweza kumcontroll kwa namna yeyote mazee yashastaafu mitaji ipo kwa nn wasiwatoe tu
 
Ndiyo muelewa kwamba hakuna aliye mtakatifu au mkamilifu...
 
Yule mzee wangu yupo bodi ya wakurungezi TPA. Saizi haongei tena kwenye TV.
Hoja ilikuwa ni kurudisha Shirika la meli la taifa (NASACO) na wengine walikuwa wanataka Tuanzishe Mamlaka ya Usafiri wa Majini (Tanzania Maritime Authority) kama nchi za wenzetu.

Bungeni ukapita mswaada wa kuanzisha TASAC na ingesimamia majukumu yote.
 
Kuna Mzee mmoja anajiita Mkinga, alikuwa mkosoaji sana kila TV utamkuta anachambua mabaya ya serikali, alivyowekwa kwenye hiyo bodi kapumzika anakula posho tu.

Sisi wanyonge tunakanyagana uwanjani kuaga mwili wa mwamba wa Africa.
Table manners, sio maadili kuongea ongea muda wa kula
 
Kuna Mzee mmoja anajiita Mkinga, alikuwa mkosoaji sana kila TV utamkuta anachambua mabaya ya serikali, alivyowekwa kwenye hiyo bodi kapumzika anakula posho tu.

Sisi wanyonge tunakanyagana uwanjani kuaga mwili wa mwamba wa Africa.
Yupo Body ya TPA mwezi mmoja nyuma nilionana nae,mzee anarudi kuwa kijana saizi hawezi kupiga tena kelele (Vieteee+kiyoyozi+posho mlima=Kimya kirefu)

Kipindi kile alikuwa anaongea Sana, baadhi ya vitu vilikuwa kweli na vingine alikuwa anatoa mbwembwe. Kuna mishe alikuwa akiziweka hadharani ambazo hizo kampuni anajua zinapiga hela kilaini Sana.
 
Yule jamaa hata kama mada inahusu ongezeko la joto dunian ukimpa nafasi ya kuchangia lazima ataongelea bandari

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Kabla ya kuanzisha TASAC, je serikali ilipitia na kujiridhisha kama,wanaleta zao linalochanua au waliutengeneza kwa madhumuni ya watu wachache?
Shipping haina siasa mambo ya kuokota watu nje ya professional itaendelea kutugharimu.
Mkuu heshima yako, kabla ya TASAC kuanza mabaharia na watalaamu wa Marine walipendekeza kuanzishwa kwa Tanzania Maritime Authority kama ilivyo kwa wenzetu nchi nyingi.

Ngoma ikaenda kisiasa na mwisho ikawa ni kurudisha Shirika la meli kama awali, lakini mswaada ulipendekezwa ianzishe TASAC baada ya ushawishi ikapita
 
Mkuu haya malalamiko yako Ni ulya msing tafuta namb za msingwa umwatup hili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…