tenanzinyo
Member
- Dec 28, 2012
- 64
- 23
Yule mchambuzi mahiri wa habari za michezo hapa Tz anayepiga mzigo katika redio na tv ya watu Clouds Fm na Clouds TV Shaffih Dauda kwa mara nyingine tena amepigwa panga katika kinyang'ang'anyiro cha kuwania uongozi wa shirikisho la kandanda nchini Tff. Hii ni mara ya tatu mfululizo kwa mchambuzi huyu kutoswa ktk chaguzi mbalimbali zinahusisha tasnia ya michezo hapa Nchini,alianzia kule kwenye TASWA,baadaye DRFA na leo hii TFF!Swali ni je kwanini wanamtosa mchambuzi huyu ambaye nfkr km watampa nafasi anaweza kupeleka mpira wetu ktk level nyingine?