Kulikoni Shaffih Dauda Kuangukia Pua kila Chaguzi?

Kulikoni Shaffih Dauda Kuangukia Pua kila Chaguzi?

tenanzinyo

Member
Joined
Dec 28, 2012
Posts
64
Reaction score
23
Yule mchambuzi mahiri wa habari za michezo hapa Tz anayepiga mzigo katika redio na tv ya watu Clouds Fm na Clouds TV Shaffih Dauda kwa mara nyingine tena amepigwa panga katika kinyang'ang'anyiro cha kuwania uongozi wa shirikisho la kandanda nchini Tff. Hii ni mara ya tatu mfululizo kwa mchambuzi huyu kutoswa ktk chaguzi mbalimbali zinahusisha tasnia ya michezo hapa Nchini,alianzia kule kwenye TASWA,baadaye DRFA na leo hii TFF!Swali ni je kwanini wanamtosa mchambuzi huyu ambaye nfkr km watampa nafasi anaweza kupeleka mpira wetu ktk level nyingine?
 
Shafii ni sawa na Wanenguaji wa dansi,akiwa jukwaani anakata mauno mpaka raha lakini ukienda nae kitandani,zero.
Pengine nae akikaa studioni ni muongeaji sana,lakini akibananishwa engo fulani,zero.
 
Yule aliyekua anajiita Dr Leak mchambuzi wa maswala ya mpira si yupo TFF! Mbona hamna jipya?
 
Pole yake hakuwa na sifa aendelee kutangaza tuu!
 
Shafii c lolote c chochote kada wa simba yule...pale dogo mwenye upeo jofrey leya tu , shafii kujieleza tu tatizo...
 
ninavyomsikiaga akichambua soka hapo clouds sikujua kama angeangukia pua, mh ama kweli ukubwa wa pua si wingi wa kamasi.. pole shaffih Dauda
 
yaani usinikumbushe jana full kulalamika huku malaya love anaplease alex ndio anamchochea acha nilicheka sana maana alipigwa chini drfa akasingizia alienda kufanya uchunguzi sasa huku tff ndio imemuuma balaa akaungane kaka wambura wakate rufaa hana ufahamu na katiba ya tff..
 
Mimi huwa namkubari zaidi huyo Dogo Jeff Leya na Edo Kumwembe ila Shaffii ni Shabiki sana, hivyo kama ilivyojidhihirisha ushabiki wake pale aliposhindwa ktk uchaguzi wa DRFA ndio uliopelekea kuonekana kuwa hajui katiba ya TFF hii pia na kwandugu yangu Wambura yeye ni mwanamichezo lakini hajui kuishi michezoni.
 
shaffih anaweza ttz vyama vyetu vya michezo vina ubabaishaji mwingi hawataki watu wa kweli!namshaur brother shaffih abakie kwny uchambuz tu maswala ya uongoz awachie wenyewe wanaojiita watu wa "mpira"
 
Samahani kaka matola unaweza dhani nakufatilia sana ila toka hata sijawa member nilikuwa nimekariri jina lako kwakuwa kila penye hate post hukosekani, nadhan ww ni mtu pekee uliyeumbwa bila tatizo na usiye na makosa.
 
hawezi fitna za kugombea uongozi kwenye vyama vya michezo...anachoweza ni kupiga mdomo tu hapo Clouds.
 
ninavyomsikiaga akichambua soka hapo clouds sikujua kama angeangukia pua, mh ama kweli ukubwa wa pua si wingi wa kamasi.. pole shaffih Dauda

Uswahilini kwetu kuna jamaa anajua kuchambua na kuihadithia picha ya kihindi lakini muulize Kamche umemuacha. Namaanisha unamuona anajua sababu wewe hujui kabisa kwahiyo yeye ni chongo kwenye Kengeza
 
shaffih anaweza ttz vyama vyetu vya michezo vina ubabaishaji mwingi hawataki watu wa kweli!namshaur brother shaffih abakie kwny uchambuz tu maswala ya uongoz awachie wenyewe wanaojiita watu wa "mpira"

Anaweza amefanya nini mpaka sasa lakuonekana au ndo huo uchambuzi.
 
Back
Top Bottom