Kulikoni Sitta na Makamba?

Kulikoni Sitta na Makamba?

. Hawa jamaa wajanja sana wamepima upepo wameona hakuna dalili njema na kukumbatia mafisadi ni kujimaliza wenyewe, dawa ni kuwabeba wote.

Changa la macho hilo. Wameamua kuirukia hoja ya kupiga vita mafisadi iwe egenda ya ccm, nyooookooo, moyoni bado ni mafisadi
 
Sioni tofauti kati ya Makamba na Joti wa Komedi Original. Maneno aliyoongea Makamba hayahitaji shahada kujua kwamba hayatoki rohoni. Kama sisiemu ina katibu mkuu kama huyu unategemea SERA ZAKE ZIWAKOMBOE WATANZANIA?

Sitta ameshitukia kuwa hali si nzuri Urambo Mashariki ambao kwa asilia hupenda upinzani na hata yeye analijua hilo kuwa kama asingepambana na mtu ambaye hakwenda shule kwenye uchaguzi wa 2005 basi angepigwa chini.
 
Makamba ni mnafiki mkubwa sana> tena kama ccm hawajajua huyu ndiye anaekiharibu chama. Sijui yukoje huyo jamaaa

Akili yake ni ndogo sana ndio maana hana aibu. A rational man can not do that.
 
Makamba ndo KATIBU MKUU TAIFA WA CCM..Kwa nafasi yake hiyoo anaongoza sekretariati ya chama hicho tawala na katibu wa vikao vyotee vya juu vya chama..

Tukimjadilii kama kiongozi wa chama kitaifa tutatambua nguvuu yakee kichama.


Nguvu ya kuongea pumba???
 
Ninachompendea Makamba ni kwamba ana mbinu na staili nyingi za kuomba radhi hasa anapogundua amekosea. Sitta msamehe Katibu wako Mkuu, kamshika mkono hadi mama yako mzazi, hakuna samahani nzito kuliko hiyo. Tatizo ni kwamba Makamba akichokonolewa kidogo tu atalipuka na kuropoka tena!
 
Kwenye political game kila kitu kinawezekana. Hii ndio namna pekee ya kujisafisha mafisadi kwakuwa wamesababisha imani ya wananchi kwa ccm kupotea kabisa. Umesahau JK alipoulizwa msimamo wake wakati akijibu swali? Alipingana na alichosema Chiligati wakati huyo ndo alitumwa kusema msimamo wa chama. Tatizo naliona pale Makamba atakapokanyaga kule Kyela au kwa Simanjiro na Same. Atapokelewa hivyohivyo? CCM wamechezea wakati na watu wameshaamka hali ni mbaya sana kufikia kilele cha 2010
 
Huyu mzee ni msanii na kigeugeu sana, nani kama zuzu hivi, mimi binafsi namlinganisha na askari wa jiji, ambao ukiwaambia kamata hata bila kuuliza watakamata. makamba ni kikaragosi cha mafisadi wanamchezesha kadiri watakavyo, ndio maana sasa sishangahi akizikana kauli zake mwenyewe, this old boy is capable of denying his own parents so long as inamhakikishia maslahi yake kisiasa, alichogundua ni kuwa yeye na wenzie chiligati na guninita wanacheza ngoma tofauiti na wimbo wa mwenyekiti wao sasa nachofanya ni kijaribu kubadili step za uchezaji ili aende sawa na wimbo wa JK, lakini kwa sababu He is a kind of short memory guy, amekwisha sahau kuwa juzi tu alikwa anacheza tune ya mafisadi na watanzania wakiwemo wana Urambo mashariki walimuona akicheza tune hiyo. Hafai huyu mzee na kama CCM hawajui huyu ndio anakimaliza chama chao, hana tofauti sana na Kingunge. Msishange atabadilika tena!
 
Uchambuzi Bomba ila naamini there is more to it. Kwa mfano mtaji wa kutegemea ujinga na umasikini wa wapiga kura kulinganisha na masilahi yao/yetu ya kijamii na uchumimi yanaitatiza ccm.
 
Hivi mnajua nani alipendekeza kwa JK jina la makamba kuwa katibu mkuu?? kumbuka aliingia kwenye sekretariati ya chama akiwa pamoja Rostam. Chungeni sana sana hatua hiyo iliyochukuliwa na makamba!! Rostam hata afanyeje hatageuka kuwa mwafrika na hivyo hivyo mtu aliye wahi kula nyama ya binadamu hawezi kuacha. Kuacha ufisadi ni kugumu sana ni mpaka utokewe na roho mtakatifu.
 
Huyu mzuri kinachomsaidia Mungu alimuondolea aibu zote. Tena akasema Mzee Six ni ndugu yake hawezi kumtenda hivi!
 
Wakuu Rejea Makala ya MZee wangu Mwanakijiji, Yaliyasema haya bwana, hata hawa wanaojiita kuwa Makamba wa Ufisadi wakina Mwakyembe watashindwa sehemu ya kushika wala kuzungumza, Kuendelea kumzungumzia Makamba sisi wote tunakuwa sawa na yeye, Wanajua kwanini aliwekwa hapo, Ni ajabu sana, anatia hasira sana
 
Yote tisa, kumi ni kwamba Mpendwa wetu Sita anatakiwa kuwa mwangalifu sana na hawa mafisadi, kwa maana kama alivyochangia mmoja wa wachangiaji Makamba kama walivyo mafisadi wengine ni mnafiki tu. Wameshindwa kumng'oa sasa wanajifanya kumuunga mkono.
 
Jeshini ukiwa msitari wa mbele kurudi nyuma ni mbinu pia. Adui mwenye akili hatalichukulia tukio hilo kwa papara. WAPIGANAJI LAZIMA WAJIANDAE, LINALOKUJA NI PIGO LA MWISHO. hawatapona. Hiyo ndiyo CCm bwanaaaa.
 
Shida ni sisi wenyewe hatutaki mabadiliko. Pima tu humu JF angalia upepo unavyokwenda...... utagundua!!! Tunaiuza nchi yetu kwa kwa peremende.
 
Hakuna asiyemjua makamba kuwa ni mtu wa kuuma na kupuliza,kama alivyosema mwenyewe kuwa 6 ni mjanja na ndio maana kamshindwa na pia ccm imemtuma kwa kuzingatia upepo wa kisiasa ulivyo kwa sasa.
Naona anazidi tu kujichora..............ccm wanatapatapa wameishiwa hawana lolote................
 
Hakuna kitu kipya hapa labda tusubiri kuona kamati ya Mzee mwinyi aje naye atasema nini, Lakini sasa hivi vita dhidi ya Ufisadi imefidasiwa na wahusika. Dr. Slaa ndiye mwenye Vita lakini CCM wanaiba tu.
 
Ninachompendea Makamba ni kwamba ana mbinu na staili nyingi za kuomba radhi hasa anapogundua amekosea. Sitta msamehe Katibu wako Mkuu, kamshika mkono hadi mama yako mzazi, hakuna samahani nzito kuliko hiyo. Tatizo ni kwamba Makamba akichokonolewa kidogo tu atalipuka na kuropoka tena!
sa si wangekuja wale wenyewe walioinjinia mpango wa kutaka kumwondoa Sitta? Kwa nini waendelee kutuma wapambe? radhi yao haitakubalika mpaka watakapokuja na wao kumshika mkono mama
 
Back
Top Bottom