Uchaguzi 2020 Kulikuwa na ulazima gani kununua ndege za kibiashara kwa cash kuliko kununua matrekta na kuyagawa kila kijiji ili kulitupa jembe la mkono?

Subirini mkiingia madarakani mnunue matreakta hakuna shida waliompigia kura ndio walioenda haya na nyie mpigieni wenu anunue matrekta manajifanya mnajua sana wakati hapigi kura na mkipga mnakosea
Mtoa mada ameleta hoja nzuri sana, uwekezaji kwenye miundombinu ya sekta ya kilimo ingeleta tija kubwa sana kwa wananchi wengi. Nadhani si kila hoja tunaingiza mambo ya siasa. Magufuli kuna mambo anafanya makosa sana.
 
Akili za Magufuli anazijua yeye mwenyewe Magufuli
 

Sawa na Milion 50 kila kijiji nitajie Dar Es salaam ina vijiji vingapi?
 
Ipo hivi, manunuzi ya izo ndege hayskupitishwa na bank. Ni siri ya alyezinunua na kampuni iliyouza. Ili atupige akaona anunue kwa kash ili kesho tusijehoji pesa zinazolipwa.
 
Kutetea ujinga ni ujinga pia. Kununua ndege sio shida. Shida inakuja unanunua ndege bila mipango ya kuzifanya zizalishe kwa tija. Au labda kununua tu ndio sifa iliyokusudiwa.

Unataka kushindana na KQ ET kwa kununua airbus wakati uwezo wao ni kutumia dash 8 kutoka dar kigoma, mtwara nk. Je tuna abiria wa kujaza airbus kila siku kwenda mwanza, kilimanjaro au znz maana hiyo ndio mikoa yenye kuonekana inahitaji ndege nyingi.

Ok fanya hayo yote ila watumishi wako wape neema basi. Unadai nchi haina pesa, itakuwepo vipi na pesa wakati pesa inaenda kwenye mradi ambayo tija yake ni ndogo kwa wakati huu.

Ukihoji hayo mnatafutana.
 
Acheni kupayuka hovyo Atcl ilipokufa mlipiga kelele kuwa tunahitaji shirika la ndege la taifa. Leo limefufuliwa mnaanza kuponda bila sababu.

Kununua ndege kwa idadi hiyo kwa fedha za kigeni taslimu ilikuwa ndio sharti la kufufua ATCL ?
 
Kwani watalii walikua hawaji kwa kua hatuna ndege kuna mengi ya kufanya ku promot utalii na sio hizo propaganda za ndege kukuza utalii
 
Matrekta yapo mengi tu huku mtaani, acheni visingizio vya kijinga. Tena yawezekana unayesema hvyo hata hujihusishi na kilimo. Trekta zmelala tu huku mtaani zmekosa kazi wewe unashauri turudi kipind cha ujamaa.
 
Eti kila Kijiji kipewe trekta akili Huna Kuna vijiji Ni wafugaji sio wakulima na Kuna vijiji hawalimi hulima mazao ya kudumu Kama mikorosho ,Chai ,kahawa nk..
Hakuna kijiji kisichokuwa na wakulima nchini,kwani mfugaji haitaji trekta,unaijua kazi ya trekta
 
Kuna mgombea anasema nchi hii ni tajiri na pesa zipo huku wananchi wengi walishasahau kitu inaitwa chai wanabahatisha mlo mmoja tu kwa siku, haku si ni kuwatukana watz
 
Wewe bado unakuja na mawazo ya kizamani namna hiyo🤔? Naomba kujua elimu yako tafadhali.
 
Tatizo la Afrika siyo katiba, tatizo ni mfumo wa uongozi hata katiba tuliyonayo bado kuna mazuri yake yanavunjwa kila siku na mheshimiwa na spika na jeshi la polisi. Hata ilitwe katiba nzuri vipi bila commitment na vyombo husika kufanya mambo kwa usahihi pasipo uoga haina maana.

Kenya juzi nimeona wanalalamikia katiba yao wanataka eti ipigwe kura ya maoni na Raila Odinga ndiye anayeongoza hii movement. Nikabaki nashangaa si juzi juzi tu wamepata katiba mpya wakasema ni dawa ya matatizo yao yote.
 
Zile milioni 50 kila kijiji zilitosha kununua trekta kila kijiji. Bei ya airbus moja ni matrekta mangapi. Kijiji kingelima hekari ngapi, ajira ngapi zingetengenezwa. Sijui lini nitapanda hayo mandege kama nauli ya basi tu inanishinda
 
UNATAKA KUMFUNDISHA BABA KUTAWALA NYUMBA?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…