SoC03 Kulinda amani ya nchi

SoC03 Kulinda amani ya nchi

Stories of Change - 2023 Competition

AlexOnesmo

New Member
Joined
Jul 22, 2023
Posts
2
Reaction score
1
Ili tuendelee kuilinda amani ya nchi yetu,

Kwanza kabisa viongozi wa nchi wanatakiwa wawe waadilifu, waaminifu pia wawe na hofu ya MUNGU kwa lolote wanalolifanya ili kuwatumi wananchi wao.

Watakapokuwa na hofu ya MUNGU wataogopa kufanya kinyume au kwenda tofauti na sheria za nchi.
Pia uzalendo, unapokuwa mzalendo wa nchi yako utaweza kuiongoza vyema kwani utaamini sina sehemu yoyote ya kwenda endapo nitaharibu nchi yangu, nitafanya juhudi kuilinda na kuitetea nchi yangu ili amani na maendelea viwepo.

Kusuruhishana Kama kunatofauti ya viongozi wa nchi, tunapaswa kutatua tofauti zozote zinazoweza kuwepo ndani ya viongozi wanaoiongoza nchi kwani migogoro midogo ndoinayoweza kuvunja amani katika nchi, na maendeleo ya nchi kwa ujumla, viongozi wanapaswa kuelewana kuwa kitu kimoja kwa shughuli yoyote ya kimaendeleo ndani ya nchi bila kujali vyama vya siasa, kushirikiana na wananchi wake kwa jambo lolote ili kuleta uhusiano mzuri wa serikali na wananchi wake hasahasa kwenye miondombinu ya nchi.

Viongozi wnapokuwa wanaelewana na wanajadiliana kwa pamoja kila jambo la kujenga nchi bila kujali vyama vya siasa basi nchi itakuwa imara na itakuwa na maendeleo makubwa zaidi na hakuna mtu yeyote wa nje ya nchi anaeweza kuja kuibomoa wakati viongozi wote ni kitu kimoja
 
Upvote 1
Back
Top Bottom