Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
Sheria ya ndoa ipo wazi watu wawili wanapoishi pamoja kama mke na mume watahesabika kuwa ni wanandoa kama hakuna anayebisha yaani (rebuttable evidence). Vile vile wanandoa wanapokuwa wametengana kwa kipindi kinachozidi miaka miwili au zaidi watahesabika kwa sheria hiyohiyo si wanandoa hii ni kwa sababu sheria ni msumeno na inakata pande zote mbili.
Mdai ambaye ni mume wa Josephine anakiri mahakamani ya kuwa yeye na Josephine hawakuwa wanaishi kama wanandoa kwa zaidi ya miaka mitatu jambo ambalo hata mkewe wake wa zamani anakiri.
Hivyo kuna rebuttable evidence baada ya miaka miwili ndoa hiyo ilikuwa imekufa yaani irreparably broken na wanandoa hao wa zamani walikuwa wamtengana kwa matendo yao ya hiari yao. Ikumbukwe ndoa msingi wake mkuu ni hiari na hakuna mahakama yoyote duniani yenye mamlaka ya kuwalazimisha watu ambao hawako tayari kuishi pamoja kama mke na mume kuishi hivyo. Hivyo ni umbumbumbu wa sheria kukimbilia mahakamani kwenda kudai ulidhalilishwa na mtaliki wako baada ya zaidi ya mwaka mmoja wa kisheria kwa sababu huyu sasa siyo tena mke wako. Mlalamikaji alipaswa kulalamika ndani ya miaka miwili ya kisheria baada ya kutengana na mkewe badala ya kusubiri miaka mitatu kupita na aliposikia mtaliki wake sasa amepata mtu mwenye uwezo wa kifedha kukimbilia mahakamani kudai fidia ya Tshs bilioni moja wakati yule sasa siyo mke wake bali ni mtaliki hata kama hakuna aliyeenda mahakamani kudai talaka.
Hili Mlalamikaji hana ubishi nalo na ndiyo maana amejisweka kwenye nyumba ya mwanamama mmoja wa CCM ambaye anaishi naye kama mume na mke. Mwanamama huyo hivi sasa anagombea jimbo moja hapo Dar kwa tiketi ya CCM.
Ni dhahiri Mlalamikaji alielewa ya kuwa ile ndoa ya mume mmoja kwa mke mmoja until death does us apart was all water under the bridge na ndiyo maana ameamua kuwekwa kimada na kigogo mmoja ndani ya chama cha mafisadi na ambacho ni maarufu kwa kujiita ni CCM.
Sasa hizi purukushani za kutumiwa na mafisadi eti kwa sababu ya ujira mdogo atakao ulamba yanatoka wapi kama siyo kuidhalilisha mahakama na kujishushia yeye mwenyewe heshima ya kiutu uzima mbele ya jamii. Baada ya uchaguzi kupita, CCM kama kawaida yao watamtelekeza huyu ***** na wala hawatataka kuhusishwa naye tena. Si mnawajua CCM na sera yao ya use and dump? Si sera hii ndiyo imetuleta laana hiyo ya umasikini wa kutupwa? CCM ni magwiji wa kutulamba miguu kabla ya uchaguzi lakini wakisha pata baraka zetu huwa hatuwaoni hadi uchguzi wmwingine ndiyo hutukumbuka kwa fulana, kofia, kanga na wakati mwingine ubwabwa na nyamapori za kutokoswa.
Mahakama Kuu inapaswa kutupilia mbali upuuzi huu ili iendelee kushughulikia maswala yenye tija kwa jamii