Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,773
- 1,174
๐๐๐น๐ถ๐ป๐ด๐ฎ๐ป๐ฎ ๐ป๐ฎ ๐ช๐ฎ๐ฟ๐ฎ๐ธ๐ฎ ๐๐ฎ ๐๐ฎ๐ฟ๐ฎ๐๐ฎ ๐น๐ฎ ๐ ๐ฎ๐ฎ๐๐ธ๐ผ๐ณ๐ ๐๐ฎ๐๐ผ๐น๐ถ๐ธ๐ถ ๐ง๐ฎ๐ป๐๐ฎ๐ป๐ถ๐ฎ, ๐๐ถ๐ณ๐๐ฎ๐๐ฎ๐๐ผ ๐ป๐ถ ๐ต๐ฒ๐ธ๐ถ๐บ๐ฎ ๐ฎ๐บ๐ฏ๐ฎ๐๐ผ ๐๐ถ๐ป๐ด๐ฒ๐๐ฒ๐๐ฎ ๐ธ๐๐๐๐บ๐ถ๐ธ๐ฎ
Moja, Kama ilivyoandikwa kwenye kitabu cha Mathayo 5:9
Mt 5:9 SUV
Neno la Mungu linasema.. [9] Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu.
Kama Kanisa ni muhimu kujua nafasi yake kwenye jamii kwa kusimama kuwa wapatanishi wa Serikali na Wananchi, kuliko kusimama upande wa wananchi peke yake kama waraka wao ulivyosema. Kwa sababu nafasi ya Kanisa kwenye jamii sio kuwasemea wananchi au kuisemea Serikali bali kufanyika daraja kati ya pande zote mbili.
Vile vile, Kanisa huchangia kuwa na Jamii bora kwa kusaidia kutii sheria, uadilifu, kufanya kazi kwa bidii, na kuwa raia waaminifu.
Pili, TEC walitakiwa kuomba nafasi ya kukutana na Serikali na kutoa mapendekezo yao.
Katika Kitabu cha Yakobo 3:17-18
Yak 3:17-18 SUV
Neno la Mungu linasema..
[17] Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, TAYARI KUSIKILIZA MANENO YA WATU, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki. Na tunda la haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani.
Kama Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania wakiwa ni wawakilishi wa Kanisa Katoliki, wangeomba nafasi ya kukaa pamoja na Serikali ili watoe mapendekezo yao kufuatia kilichotokea ili kuweza kuijenga Nchi kwa pamoja. Hakuna njia nyingine ambayo Kanisa imepewa kwenye maandiko ya kuhusiana na tawala na uongozi mbalimbali isipokuwa kwa NJIA YA HEKIMA.
Na hii ndio njia ya hekima ambayo tunaisoma katika Maandiko matakatifu ya Mungu, Kitabu cha Waefeso 3:10 โ yanayosema..
Efe 3:10 SUV
[10] ili sasa, KWA NJIA YA KANISA, HEKIMA YA MUNGU iliyo ya namna nyingi IJULIKANE NA FALME NA MAMLAKA katika ulimwengu wa roho.
Tatu, Uponyaji wa kweli unaanzia kwa Mungu kupitia Yesu Kristo.
Katika Kitabu cha 2 Wakorintho 5:19 - Neno la Mungu linasema..
[19] yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho.
Watu wote walioumiza na walioumizwa ni Watu wa Mungu. Wote wanahitaji msaada wa Mungu ili kuwafanya wawe bora. Ianzie Kanisani kwenye kuwasaidia watu kupona majeraha ya ndani kuliko kuchochea chuki dhidi ya Taifa lao. Tanzania itajengwa na watanzania wenye mioyo iliyo na matumaini makubwa kwa Mungu juu ya maendeleo ya nchi yao.
Nne, Mamlaka zote zinatoka kwa Mungu, hivyo ni tendo la Imani pia kuiachia Serikali mpya ya Awamu ya 6 kushughulika na yote ambayo Mheshimiwa Rais aliyasema kwenye Hotuba yake alipokuwa akifungua Bunge ikiwa ni jitihada zao katika kuliunganisha Taifa letu na kuijenga Tanzania moja.
Kama ambavyo tumekuwa tukiwaeleza tangu awali, Serikali hii ya Awamu ya 6 ni Serikali sikivu na Serikali inayojali, hasa kwa wakati huu tunapotafuta kujenga na kuponya majeraha tuliyopata kama ambavyo Mheshimiwa Rais alivyosema kwenye hotuba yake alipokuwa akifungua Bunge.
Mtu yoyote akisikiliza kwa umakini Hotuba ya Mheshimiwa Raisi atagundua nia yake ya dhati kwenye kuikumbatia nchi nzima kama mama na makundi yake yote, yakiwemo makundi yaliyoathiriwa na changamoto zilizotokea wakati wa uchaguzi.
Hakuna ambaye angependa kuongoza Taifa ambalo limegawanyika au linamaumivu, na ndio maana Mheshimiwa Rais aliweka wazi kuwa ameamua kuunda TUME MAALUMU itakayochunguza yote yaliyotokea kwenye uchaguzi na KILA ALIYEHUSIKA ATAWAJIBISHWA NA KUWAJIBIKA KATIKA NGAZI ZOTE.
Tumeuona Waraka wa Viongozi wa dini wa Kanisa Katoliki Wahashamu na Ma-Baba Askofu ambao sisi tunawaheshimu mnoo, na tunaamini yote waliyoyaandika ni kwasababu wameisikiliza Hotuba ya Mheshimiwa Rais na ndio maana yote ambayo wameyaeleza kwenye waraka huo, asilimia 70-90 Mheshimiwa Rais aliyazungumzia kwenye hotuba yake alipokuwa anafungua Bunge la 13, hivyo KANISA NA WANANCHI WOTE KWA UJUMLA waiamini Serikali yao kuwa inajali na inasikiliza na kama ambavyo Mheshimiwa Rais alivyosema kwenye Hotuba yake tuone Rais na Serikali yake watakalolifanya baada ya kusikiliza Ripoti ya Tume itayoundwa na kuleta majibu ya kiuwajibikaji.
Bado nipo kwenye maumivu ya moyo juu ya kinachoendelea kwenye Kanisa langu KATOLIKI.
Kila siku zinavyokwenda naona tunalizamisha Kanisa letu na kuendelea kuwagawa Waumini na kanisa kiujumla na kupelekea udini ndani ya nchi yetu.
Hili si Kanisa ninalolijua, lililotupa mafunzo ya unyenyekevu na utii kwa Mamlaka za Nchi.
Hili si Kanisa langu ninalolipenda kwa miaka yote 47 ya umri wangu.
Kanisa letu linatoka kwenye mstari kila kukicha na linatoka kwenye kazi ya kutibu roho zetu na linaenda kuumiza na kizichana roho zetu.
Kanisa letu limetoka kuwa Kanisa la Mungu na Mkakati wa kuwapika, kuwajenga Vijana kuwa Viongozi bora kabisa Nchini kama lilivyofanya kwa Viongozi wetu na Wazee wetu kama Mwalimu Nyerere, Mzee Mkapa, Wazee wetu kina Simbakalia, Profesa Mahalu, Bernard Membe na wengine wengi sana ambao kanisa liliwalea, kuwafunza na kuwajenga kuwa Viongozi waliotukuka kwenye Taifa leo.
Namuonea huruma sana Kaka yangu Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, Makamu wa Rais wa sasa ambaye ni Mkatoliki safi kwa namna anavyopitia haya yanayotoka kwenye Kanisa letu tunalolipenda.
Kanisa lina Makamu wa Rais ambaye wamemlea na kumkuza wenyewe. Kwa njia zingine tunasema wana Direct contact ndani ya Viongozi wakuu kwenye Nchi akiwa ni namba mbili. Najua na nakupa pole sana Daktari Emanuel Nchimbi maana haya yanayofanywa na Kanisa letu yanakuumiza na kukukwaza mno ila kwa kuwa Kanisa letu limetoka kuwa Kanisa la KIMKAKATI wa kuwafunda na Kuwajenga VIONGOZI na kugeuka kuwa Kanisa la UWANAHARAKATI la kuwabomoa Viongozi wa Serikali na kuwagawa Waumini wao na Wananchi kwa Ujumla. Yani limegeuka Kanisa la kupingana na Serikali. HILI LINALITIA AIBU KANISA LETU.
Kanisa hili ni letu na siyo la Maaskofu peke yao. Haya yanayoendelea kwenye Kanisa letu kama itafanyika takwimu za haki na ukweli basi nina uhakika Kanisa hili limepoteza na litapoteza Waumini wengi mno kuliko kipindi chochote kilichowahi kutokea Nchini kwetu. Na haya yamewahi kutokea Nchini Kenya, Uganda, DRC, Burundi, Rwanda na kwengineko ambapo leo hii kwenye Nchi zote hizo nilizozitaja Kanisa limepoteza nguvu yake kwasababu ya kujiingiza kwenye Siasa na tena siasa za Kiuwana-harakati. Hili linapaswa kulindwa ndani ya kanisa letu Katoliki lisitokee hapa TANZANIA. Heshima ya Kanisa hili ni kubwa sana tusikubali kupelekwa tunakopelekwa.
WAPI VIONGOZI WETU WA KIROHO MNATUPELEKA?
Haya ndiyo yale mafunzo ya hili KANISA?
WAKATOLIKI TUAMKE NA TUZINDUKE KULINDA HESHIMA YA KANISA LETU NA KURUDI KWENYE MSTARI WETU WA KULILEA TAIFA HILI.