Kulipa deni ni mtihani

co fm

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2016
Posts
1,541
Reaction score
2,487
Wanajamvi kama unataka kufanya jambo lako na hela inapungua bora usubiri tu upate hela umalizie jambo lako maana sio poa. Nilikuwa nataka kununua kitu last month hela ikapungua kama laki mbili hivi, basi nikamcheki mshikaji wangu aniongezee then tarehe 21 ntamrefund nikitegemea mshahara kuingia, so mshahara umeingia toka Jumatatu bado naona ngumu kumlipa yaani sio poa na hela ninayo.
 
Umechukua nyingi sana iyo mkuu. Siku hizi wagumu tunafaulu mtihani wa ugumu wa maisha kwa kukopa tu elfu25 ikizidi sana 35.
 
una pepo lakutokulipa madeni
 
We ndio mimi.

Mi Ijumaa nilikuta missed call ya madam mmoja tunapiga nae kazi. Sikua na dakika nikamtext. Akaniambia Mad Max mbona unatext kama haupo vizuri kiuchumi sema. Nikamuambia ukweli kwamba natembelea rim. Akanitoa 30k. Salary Monday ikaingia. J4 hatujaenda job. Leo dah nimeitoa kinyonge sana.

Na usijiroge ukakaa na deni zaidi ya wiki wakati unaweza lipa. Utahisi kama unaonewa hivi wakati ulivyopewa ulishukuru sanaaa.
 
Yaan hela unayo ila kulipa unaona tabu. Katika makosa sitokaa nikarudia ni kukopesha sababu ikifika muda wa kulipa kuna pipo zinajizungushaaaa.
 
Mimi kwa kweli siku hizi sikopi wala sikopeshi mtu.Tigo nivushe wananipa access ya kukopa hadi laki tano na nawalipa ndani ya mwezi.so nikiishiwa tu huwa nazama tigo nivushe ndiyo mkombozi wangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…