Francis fares Maro
JF-Expert Member
- Jun 20, 2021
- 1,227
- 1,339
Ndugu wanabodi,
Nimefwatilia Kwa kina mijadala hii ya Tozo na Kodi ya majengo
Niseme machache!
Tulipe kodi kwasababu Kodi ndio msingi wa maendeleo yetu,bila Kodi nchi Itakua ngumu sana hii,hizi Kodi ndio tunaona mabarabara, vituo vya Afya, watumishi kupandishwa madalaja, madarasa, Elimu Bora, madawa hospitalini, tunapunguza vifo vya mama wajawazito, maji safi na salama nchi nzima.
Bila Kodi maana yake Sisi kama nchi tutaendelea kuwa tegemezi,tutataka tufanyiwe kila kitu na wahisani, tutashindwa kujiendesha, tutashindwa kupanga na kufanya maendeleo yetu, tunaweza kusema Tozo Sawa lakini zimekua kubwa lakini wakati wa kutoa maoni tulikua wapi?
Tunapenda uongo na umbea tunaacha mijadala ya maana na msingi ya kujenga nchi tunaenda kushadadia vitu vya kipumbavu kabisa!
Awamu ya Tano
JPM aliweka wazi kabisa lazima tulipe Kodi ili tujitegee tuache kusubiria misaada kutoka magharibi na uchina huko ambayo inatunyonya sana!
Nadhani ni wakati Ndugu zangu tufunge mikanda tulipe Kodi tujiendeshe wenyewe, tuweze kufanya hata tafiti zetu, vijana wetu tuwapatie mikopo wajiajiri kwa namna hii Mama zetu tuwatue Ndoo, tupate umeme huko vijijini, barabara zitengenezwe, reli ya SGR, bwawa la Nyerere, watoto wetu waache kukaa chini,walimu walipwe madeni yao,wastafu nao asiachwe namna hii lakini vitu vyote hivi ni msingi wa kulipa Kodi.
TULIPE KODI KWA MAENDELEO YETU