Kulipa mahari ni zawadi au udhalilishaji wa mwanamke?

DJ SEPETU

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2017
Posts
8,413
Reaction score
12,336
Juzi kati rafiki Yangu mmoja alitutoa dar hadi huko bukoba kama kampani wakati anaenda kumposa binti flani.

Ni familia nzuri na yenye uwezo wa kati wacha Mungu.

Kilichonishangaza ni kiasi cha mahari ya million 8 aliyopangiwa jamaa yetu

Ingawa jamaa anampenda huyu dada ila nadhani ataweza ghairi sababu ya hii mahari
 
Mil8 halafu huyo rafiki yako bado anaishi nyumba ya kupanga?(tagadhali usiseme mambo ya vipaumbele hapa) toa milioni mbili hizo zilizo baki wakanunue kiwanja sehemu nzuri
 
makadilio ya mahali yaendane na uwezo wa muhusika. mahali sio kodi.
mahali isitumike kama mtaji wa kukwamua ukoo kutoka kwenyw umasikini.

Mahali linapaswa kuwa tendo la furaha, ndio maana ikaitwa Zawadi sio kukomoana, au kukwamisha.
kama uwezo wangu ni laki nne, ntawambia...
 
Wazungu hili jambo kwao ni udhalilishaji na hii ni kwakuwa kwa mujibu wa historia wazungu walikuwa watu wa mapangoni hivyo kuna mambo mengi kwao ni kinyume. Mahari ni lazima hata utoe kandambili km ndo mmepatana basi ni mahari, Binafsi M8 sitoi hata M1 sitoi na nikitoa ukweni wasijipendekeze kuniomba hata pesa ya soda manake waliamua kunikomoa namie nalipa fadhila.
 
Hata kamilioni hutoi mkuu[emoji23] [emoji23]
 
Ni kumdhalilisha mwanamke ndio maana wazazi wengine wanamwachisha mtoto masomo ili tu wapate mahari . Kama mwanamke ananipenda kama ni mahari tutatafuta pamoja ili tuwape wazazi wetu (pande zote) zawadi kwa kutulea
 
Wazungu hili jambo kwao ni udhalilishaji na hii ni kwakuwa kwa mujibu wa historia wazungu walikuwa watu wa mapangoni hivyo kuna mambo mengi kwao ni kinyume. Mahari ni lazima hata utoe kandambili km ndo mmepatana basi ni mahari, Binafsi M8 sitoi hata M1 sitoi na nikitoa ukweni wasijipendekeze kuniomba hata pesa ya soda manake waliamua kunikomoa namie nalipa fadhila.
Aiseee...ha hahahaa haha
 
Bora hata pesa kuliko n'gombe!
Kweli unaweza kubadilishana mtoto wako na n'gombe au mbuzi!hii ni udhalilishaji zaidi
 
Back
Top Bottom