Kulipa mahari ni zawadi au udhalilishaji wa mwanamke?

Kulipa mahari ni zawadi au udhalilishaji wa mwanamke?

Mahari ni zawadi kwa wazazi kwa kukutunzia vyema mkeo lakini siku hizi imekua kama chanzo cha kupatia pesa. Mtu unakubali mumeo mtarajiwa alipe 8M hivi mkienda kuanza maisha akisema hana hela ya kula utamlaumu?.. Wanawake wengine wanaona sifa kabisa kulipwa mahari kubwa bila kujua anamuumiza mwenzie. Tena utakuta kijana wa watu ndo anachakarika ila mahari mtu anataja mamilioni.
 
Waweza jikuta mwanaume anaghairi!
 
Huyo mchumba wa kiume hatakiwi na wakwe zake, ukiona mtu anakutwanga kipigo kama hicho kuna siri nyuma ya pazia. Narudia huyo rafiki yako hatakiwi na wakwe zake sasa afanye uchunguzi ataona ninachomaanisha.
 
Ni kumdhalilisha mwanamke ndio maana wazazi wengine wanamwachisha mtoto masomo ili tu wapate mahari . Kama mwanamke ananipenda kama ni mahari tutatafuta pamoja ili tuwape wazazi wetu (pande zote) zawadi kwa kutulea
Kwa sheria ya Kiislam mahari ni zawadi anayopewa binti kwa kukubali kuolewa na anapewa anayeolewa sio wazazi na anapanga anaeolewa ndo anasema anataka nini
 
Mahari lazima itolewe ila isiwe mahari ambayo inafanya mtu akiwa ndoani awe anamkomoa mwanamke .

Mahari itolewe ,ujue nn ,hata ivo inamwongezea heshima sana mwanamke wako..... Embu sikia "" Fulan katolewa mahari "" inasound vipi?? .

Kuna maelezo mengi hupatikanika ndani ya mahari.
 
Huu utamaduni upo tangu enzi za zamani..wengine wanasema zawadi, wanaharakati wengine wanasema udhalilishaji
Hata utamaduni wa kukeketa wanawake upo tangu enzi kwenye zile jamii wanazokeketa.
Je huo utamaduni wa kukeketa usipigwe vita kwa sababu upo tangu enzi za zamani.

Think big.
 
Swali chokozi,km mdada kaisha zalishwa na MTU mwingine unamlipia mahari ?

Au mwanamke yupi anayestahili mahari,aliyetayari na mtoto au bado?
Kimila zetu, ukilipa mahari ukaoa.

Hata mtoto aliyezalishwa huko nyuma anakua wako, hivyo hata mzazi mwenza akija kumdai kuna gharama atatakiwa kuzilipa kwako.
 
Mahari ni zawadi na sio udhalilishaji, ila kinacho wabana ni ile hali ya familia ku panga kiasi cha mahari, ingekua sawa kama wanaume wangekua wana jipangia wenyewe, lakini asioe bila kutoa mahari. Hii ya familia kupanga ndo inayopelekea wanaume kukimbia maana wanatajiwa kiasi kikubwa na familia zingine wamegeuza mahari ndo pakupatia mtaji.
Na sio ukitajiwa tu unakimbia hata mahari huwa wana bargain bwana, unamoenda mtu si unaomba upunguziwe.
 
Back
Top Bottom