Kulipa mahari ni zawadi au udhalilishaji wa mwanamke?

Ni kumdhalilisha mwanamke ndio maana wazazi wengine wanamwachisha mtoto masomo ili tu wapate mahari . Kama mwanamke ananipenda kama ni mahari tutatafuta pamoja ili tuwape wazazi wetu (pande zote) zawadi kwa kutulea
Hiyo ya kuachisha mtoto shule ili mahari ipatikane ni ya wapi tena? anayeoa ndo anayetakiwa atafute mwenyewe mahari. Sasa kama mahari mpaka wadogo zako waachishwe shule ndo ipatikane, utaweza kweli kimuhudumia mkeo? na kulipiwa mahari na wazazi sio sawa maana ni kuruhusu wao baadae waje kuingilia maamuzi kwenye ndoa yako maana hutakuwa na sauti utabaki kukumbushwa tu tulikuolea huyo mke.
 
Wazazi waliangalie sana hili jambo huwa linaletekeza mambo mengi sana kwenye ndoa, hususani kama mwanaume ataamua kupambana na kulipa hivyo hivyo hali ya kuwa inamuumiza. Haviwi na mwisho mzuri hivi vitu.
Nafikiri itakuwa nzuri zaidi kama wasichana wakipewa nafasi ya kupanga mahari kwa wenza wao kwasababu wao ndio wanaojua uwezo wa wanaume wao. Sio mwanaume anauwezo wa kulipa laki tano anafika nyumbani kwa binti anaambiwa milioni tano huko ni kukomoana.
 
Swali chokozi,km mdada kaisha zalishwa na MTU mwingine unamlipia mahari ?

Au mwanamke yupi anayestahili mahari,aliyetayari na mtoto au bado?
kwa hiyo sisi tuliozaa mnatuchukua kama mizoga eti?
 
Kitendo cha binadamu (Mwanamke) kulipiwa mahari mi binafsi naona ni udhalilishaji wa kiwango cha juu sana.

Hakuna cha zawadi wala nini, zawadi hainaga masharti, wewe unaambiwa leta 1m alafu useme zawadi? Zawadi mtu hapangiwi, kwa ufupi utamaduni huu ni kuuza watu.

Mungu anipe mtoto wa kike sitakuja kudai mahari wala sitapanga kiwango, akipata mchumba kikubwa ntaangalia kama huyo jamaa anaweza kuishi na mke na ana akili timamu za kutafuta maisha na kujenga familia.

Kutoa mahari kunafanya wanawake wanateseka kwenye maisha yao maana wanaume wengine tuko rough sana
 
Tamaduni tuliyojiwekea waafrika..na ni kama ahsante kwa wazazi wa mwanamke

Ila binafsi mwanaume wangu ajikakamue hata kutoa nusu yake tu
 
Mahari million 8 hapana aisee [emoji31][emoji31][emoji31]
Hao wazazi hawataki binti yao aolewe
 
Sasa hapo kwenye ml8 unafikikili uta bargain million moja au laki tano tuwe makini mdogo wangu ashawai kutajiwa ngombe saba mbuzi kumi na mbili na ml5 kisa tu kaenda na gari ya mjomba yake kuepusha zile purukushani za usafi yeye alijua atatajia laki tano atoe nusu
 
Utoaji wa mahari ni tamaduni za kale na kipagani na zilishapitwa na wakati, hao wazazi hawamjui Mungu kama ulivyosema ya kwamba ni wacha Mungu siyo kweli hao ni wapagani tu sema wamejificha kwenye mwamvuri wa dini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…