Kulwa Masanja Isenge anyakua milioni 5 katika Shindano la 'Stories of change' 2022

Kulwa Masanja Isenge anyakua milioni 5 katika Shindano la 'Stories of change' 2022

Nimeona kwa kiasi kikubwa washindi ni wavumbuzi na wabunifu "Innovators" sio walioleta maandiko ya kushawishi mabadiriko.

Naona kuna haja katika hizi tuzo muweke kipengele cha Uvumbuzi au Ubunifu na kuwe na tuzo yake ili mtu ambaye atavumbua au kubuni kitu flani cha manufaa kwa jamii kwa kushare mawazo yake hapa JF apewe tuzo.

Ni mawazo yangu lakini.
 
Uko sahihi kabisa, hili shindano bado halieleweki linahitaji watu wa aina gani.
Nimeona kwa kiasi kikubwa washindi ni wavumbuzi na wabunifu "Innovators" sio walioleta maandiko ya kushawishi .
 
Mad Max

Nimeona comment yako kwenye qoute ambayo tayari ishafutwa/ushaifuta.

Nimepitia profile za washidi wa 1 hadi 5, wa 3 wametumia ID zenye vifupisho vya majina yao halisi, Mmoja ametumia jina halisi(Nathaniel Mpasi), mwingine katumia ID fake.

Kati ya hao 5, wanne wamefungua ID zao mwezi July pindi shindano lilipoanza, Mmoja(Nathaniel) yeye ID yake ni ya mwaka 2014.

Waliofungua ID mpya nina imani hawalitaki kutunza anonymity zao kwa ID fake za siku zote endapo wangeshinda, kwani ukishinda unatakiwa utoe details zako halisi kama tunavyoona walivyotangazwa kwa majina halisi.

Kwa hiyo hoja ya kusema washindi wapo kimkakati/kimchongo hapo nakataa, hawa washindi wengi wao waliandika mabandiko kadhaa ambapo wameshinda bandiko moja moja lililobora.
 
Nimeona kwa kiasi kikubwa washindi ni wavumbuzi na wabunifu "Innovators" sio walioleta maandiko ya kushawishi mabadiriko. Naona kuna haja katika hizi tuzo muweke kipengele cha Uvumbuzi au Ubunifu na kuwe na tuzo yake ili mtu ambaye atavumbua au kubuni kitu flani cha manufaa kwa jamii kwa kushare mawazo yake hapa JF apewe tuzo.
Ni mawazo yangu lakini.
Naamini hoja hizi umeweka kabla ya kusoma maandiko yote 20 yaliyoshinda, ambamo ndani yake kuna masuala ya Afya, Tamaduni, elimu, ujasiriamali nk.

Naomba uiangalie post ya kwanza kusoma nyuzi zote 20.

Lakini pia ningependa uniambie kama 'Innovation' haileti mabadiliko?
 
Naamini hoja hizi umeweka kabla ya kusoma maandiko yote 20 yaliyoshinda, ambamo ndani yake kuna masuala ya Afya, Tamaduni, elimu, ujasiriamali nk. Naomba uiangalie post ya kwanza kusoma nyuzi zote 20.

Lakini pia ningependa uniambie kama 'Innovation' haileti mabadiliko?
Mkuu mimi nimesoma hoja zote.
Hoja yangu ni ndogo tuu kwamba ili hizi tuzo zilete mantiki zaidi na zieleweke zaidi ni vyema vipengele "categories" vibainishwe na viongezwe vyema vinginevyo kila mwaka washindi wengi watakuwa wanaangukia katika mizania ya uvumbuzi na ile dhana ya mabandiko yenye kuleta ushawishi wa kimabadiriko yawe ya kisera,

kiutendaji na kiuelewa yatakuwa yanakosa ushindani kwenye uvumbuzi na kumezwa na uvumbuzi.

Yaani kwa mfumo huu tutegemee uvumbuzi na ubunifu kuchukua nafasi zaidi katika hizi tuzo kila mwaka.

Ndio maana napendekeza kupengele cha ubunifu na uvumbuzi kiongezwe ili mtu kama aliebuni mfumo wa kulinda kura aingie huko.

Ni mawazo sio kwamba napinga zoezi hili ni zuri ila liboreshwe zaidi na kutoa wigo mpana wa kinyanja.

Chivundu
 
Safi sana JamiiForums, mabadiliko katika jamii yanaanza na kuzingatia watu makini na vitu kama hivi. Nina imani Mgeni rasmi atafikisha mbali hizo nyuzi zote kwa utekelezaji kwa mamlaka zilizoguswa.
 
Mad Max

Nimeona comment yako kwenye qoute ambayo tayari ishafutwa/ushaifuta.

Nimepitia profile za washidi wa 1 hadi 5, wa 3 wametumia ID zenye vifupisho vya majina yao halisi, Mmoja ametumia jina halisi(Nathaniel Mpasi), mwingine katumia ID fake.

Kati ya hao 5, wanne wamefungua ID zao mwezi July pindi shindano lilipoanza, Mmoja(Nathaniel) yeye ID yake ni ya mwaka 2014.

Waliofungua ID mpya nina imani hawalitaki kutunza anonymity zao kwa ID fake za siku zote endapo wangeshinda, kwani ukishinda unatakiwa utoe details zako halisi kama tunavyoona walivyotangazwa kwa majina halisi.

Kwa hiyo hoja ya kusema washindi wapo kimkakati/kimchongo hapo nakataa, hawa washindi wengi wao waliandika mabandiko kadhaa ambapo wameshinda bandiko moja moja lililobora.
Nimekusoma bro. Umefanya research vizuri, shukrani umenieleza vema.

Post mods watakua wameitoa ila umenijibu vizuri thanks man.
 
Back
Top Bottom