SoC02 Kumaliza shule siyo tiketi ya kuoa ama kuolewa

SoC02 Kumaliza shule siyo tiketi ya kuoa ama kuolewa

Stories of Change - 2022 Competition

Alana

Member
Joined
Sep 8, 2022
Posts
14
Reaction score
9
"Subiri nimalize shule" imeongeza idadi kubwa ya wasomi ambao wameshindwa kutimiza malengo yao. Wengi hudhani ya kwamba, kuhitimu masomo ndiyo mwanzo wa kuanzisha familia. Wakike kwa waume wanasahau ndoto zao za awali na kukimbilia kuoa ama kuolewa pasipo kutimiza zile ndoto walizokuwa nazo wakiwa wanasoma. Mfano, Mwanafunzi anaposhawishiwa kuingia katika mahusiano ya kimapenzi, hupendelea kusema "Subiri nimalize shule". Badala ya "Subiri nitimize ndoto zangu za maisha".

Baada ya kuhitimu masomo, Ni wakati mzuri wa kutumia elimu yako kutafuta fursa za maendeleo na kuwa chachu ya mabadiliko chanya katika jamii.

Kuoa ama kuolewa Ni haki ya Kila mtu, lakini Ni vizuri kuipata kwa wakati sahihi. Unamaliza shule, akili yako yote inawaza kuolewa ama kuoa na unasahau zile ndoto ulizokuwanazo. Mfano, Mwanafunzi aliyetoka kwenye familia ya hali duni huwa na ndoto kubwa ya kubadilisha maisha ya familia yake, anaweka bidii na jitihada katika kusoma ili kuitimiza hiyo ndoto lakini mwisho wa siku wimbi la mapenzi linamshambulia na hatimaye kuwa msomi asiye na maendeleo.

Kuanzisha familia ikiwa hauna kipato itasababisha ugumu wa maisha kwako na familia yako. Japo kuna watu ambao huamini kwamba,ndoa kwanza, utafutaji utafuata. Watu wa kundi hili mara nyingi huelemewa na majukumu mengi. Kuanzisha familia sio jambo lelemama Kama hujatengeneza kwanza maisha. Kutokana na majukumu kuwa mengi, mke au mume hushindwa kuwajibika ipasavyo kwenye familia zote za upande wa kike na kiume.

Kabla ya kuoa ama kuolewa, kumbuka ulikuwa na familia yako ambayo kila wakati ulipanga Mambo mazuri kwaajili yao. Ulisoma kwa bidii ili uwajenge wazazi na uwape maisha mazuri lakini ndoto hizo umeshindwa kuzitimiza kwasababu umeolewa au umeoa wakati ambao hauna kipato au kutengeneza maisha yako.

Majukumu ya malezi yanapokuja, huwezi tena kuwatimizia wazazi wako Kama yale uliyoyapanga kabla hujaoa ama kuolewa.

Mfano, Binti mmoja aliyefahamika kwa jina la Zera, alijibidiisha Sana katika masomo yake na siku zote alifanya vizuri katika mitihani. Sababu kubwa ya kusoma kwa bidii Ni kutokana na hali mbaya ya maisha walikuwa nayo katika familia yake. Katika nyakati zote alizokuwa shuleni, alikuwa hakosi kutongozwa na wavulana tofauti tofauti lakini msimamo wako ulikuwa mmoja tu "Kama unanipenda, subiri nimalize shule" Siku zilisonga mbele,Zera alifanya vizuri mpaka alipofika chuo kikuu. Akiwa chuoni alianza kutengeneza urafiki na mwanachuo mwenzake Gotan. Ahadi zao zilikuwa waoane baada ya kuhitimu elimu ya chuo kikuu. Hakika baada ya kuhitimu elimu ya chuo kikuu, Zera aliwaambia wazazi wake "Mama na Baba, Mimi nimekua mtu mzima Nataka kuolewa…." Mama Zera akashtuka "Ebo! Umekuwa mtu mzima! Unataka kuolewa! Masikini!

Nilidhani baada ya kuhitimu elimu yako, ungetafuta kwanza kazi! Weee sio yule uliyenipa ahadi nyingi?"Mama nitabadilisha maisha yetu! Nikimaliza shule nitafanya kazi kwa bidii!". Haya Leo yako wapi? Tazama, wazazi wako hatuna uwezo, tulikusomesha kwa shida Sana, na Sasa tunategemea wewe ndiye utakayewasomesha wadogo zako, Haya Sasa niambie, umefikiria kweli?".

Zera aliinamusha kichwa chini kwa aibu huku akiongea kwa woga " Mama.. hayo yote sijayasahau… nitayafanya hayo yote hata nikiolewa…"

Mama Zera alipianza kupandisha jazba, Baba Zera akamshika mkono mke wake na kumtuliza," Ahaaaaa..mke wangu! Hili sio jambo la vita… tumuache mtoto afanye anachokipenda… Sisi kazi yetu kwake imeisha… hayo mengine ataamua yeye mwenyewe Kwani elimu amekwishaipata!"

Sauti ya Baba Zera ilushusha jazba ya Mama Zera, ndipo walipomruhusu Zera kuolewa. Taratibu za ndoa zilianza na hatimaye Zera aliweza kuanza maisha na Gutan.

Screenshot_20220910-182822~2.png


(chanzo;mwananchi blog)

Ajira ilikuwa ni suala gumu kwao, siku zote walikuwa ni watu wa kutuma maombi ya kazi na kwenda kwenye usaili pasipo kupata kazi. Ndani ya muda huo, walipata watoto watatu. Wa kwanza mwenye miaka 5, wapili mwenye miaka 3 na wamwisho mwenye mwaka mmoja.

Ugumu wa maisha uliongezeka kutokana na kuwa na familia kubwa pasipo kipato. Biashara walizoanzisha, zilikufa. Familia ya Zera ilishindwa kuhudumiwa vyema na wakati mwingine Zera alirudi nyumbani kwa wazazi wake kuomba chakula ili akalishe watoto wake. Mbaya zaidi wazazi nao hawakuwa na chakula.


Screenshot_20220910-184332~2.png

(Chanzo: Shutterstock)

Maisha magumu yaliendelea kuwatafuna wote wawili na familia zao kutokana na kushindwa kujipanga mapema hali ya kiuchumi. Ugomvi haukuisha kati yao, lugha ya upendo ilipotea.

Screenshot_20220910-181353~2.png

(Chanzo: Shutterstock)
Mwisho wa siku, Gutan alimtelekeza Zera na kumuachia watoto.

Hakika Zera alipata maumivu Sana, kiasi kwamba upepo, majengo,majani yalimuonea huruma.

Wazazi wa Zera walifariki kutokana na njaa, wadogo zake walikuwa ni wagonjwa Sana. Hali hiyo ilimfanya Zera kurudi nyumbani kwao. Maisha yaliendelea kuwa magumu, kiasi kilichopelekea Zera kuwaacha watoto pamoja wadogo zake wagonjwa ili akatafute kazi.

Niikatishe stori, nirudi kwako msomaji, unadhani Zera alikosea wapi?.

Wanafunzi wanajitaji kufanya mabadiliko katika maisha yao. Haimaanishi kuoa ama kuolewa ni jambo baya, ila ni jambo jema. Ila baada ya kuhitimu ni muda wa kutimiza ndoto za maendeleo kabla ya kuingia katika ndoa ili kutengeneza msingi mzuri wa maisha Bora.

Maisha Bora yatapelekea Ndoa yenye Furaha, uwajibikaji, heshima na upendo wa kudumu. Hali ngumu ya maisha ndiyo inayopelekea ndoa nyingi kuvunjika, kutelekeza familia, migongano mingi kwenye familia,ukosefu wa elimu Bora kwa watoto pamoja na ukosefu wa mahitaji muhimu Kama vile nguo, chakula na maradhi.

Hivyo basi kauli nzuri kwa mwanafunzi awapo shuleni wakati anaposhawishiwa kuingia kwenye mahusiano Ni "Kama unanipenda subiri nitimize malengo yangu" Badala ya "subiri nimalize shule". Tutambue ya kwamba, kuna maisha baada ya shule. Unapoamua kuolewa au kuoa hakikisha umejiandaa ipasavyo ili kumudu Mambo yote ya familia. Daima utayapenda maisha. Hivyo basi, kumaliza shule siyo tiketi ya kuoa ama kuolewa. Ukiona umejiandaa ipasavyo waweza kuoa ama kuolewa ila kama utaona hujajipanga kimaisha, jipe muda, tafuta kwa bidii na baada ya mafanikio oa ama olewa kwa mtu wa ndoto zako.
 

Attachments

  • Screenshot_20220910-182822~2.png
    Screenshot_20220910-182822~2.png
    37.5 KB · Views: 17
  • Screenshot_20220910-184332~2.png
    Screenshot_20220910-184332~2.png
    40.4 KB · Views: 17
  • Screenshot_20220910-182822~2.png
    Screenshot_20220910-182822~2.png
    37.5 KB · Views: 18
Upvote 4
Habari yako ndugu.

Hongera kwa nakala nzuri yenye mawaidha na tija kwa jamii.

Kura yangu umepata!!

Nikiamini katika uchakataji wako wa mambo na uwezo wako wa fikra na ubunifu, naomba ukipendezwa, kuipigia kura yako na kuchangia mawazo au mapendekezo juu ya nakala inayohusu Afya zetu Watanzania:-


Ahsante!! Nashukuru sana....MUNGU akubariki
 
Back
Top Bottom