Kumbe aliyekuwa anaogopewa ni hayati Magufuli lakini siyo utawala wake, Magufuli Bus Terminal mambo ni vurugu tupu!

Kumbe aliyekuwa anaogopewa ni hayati Magufuli lakini siyo utawala wake, Magufuli Bus Terminal mambo ni vurugu tupu!

Stand inachukua MABASI machache kuliko ilivokuwa UBT

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Stendi iliyojengwa kisiasa zaidi, Singida stendi ni kubwa kuliko Mbezi, la msingi kwa stendi ni eneo la mabasi siyo show OFF za kibashite za majengo.
CAG alipoliongelea alionekana mpinga LEGACY ya mwendazake yule.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Magufuli alikuwa anaogopwa na Mazezeta lakini sisi tulikuwa tunakomaa nae tu
icon_lol.gif
 
Ni vigumu kama hakuwaweka karibu nae.Hata wazazi wasipoweka mifumo imara kwa familia kila kitu hupotea pending wanapokufa.Tujifunze kuanzia ngazi ya familia
Lakini mkubwa haambiwi tazama.
 
Ahaaa, ndugu kama ulipoteza vijisenti basi sahau. Hata ngoma ikirudiwa hutoboi.

Sina senti yoyote niliyopoteza hapa nayaanika tu majizi ya Kura. Kama unajiamini, kawashauri ccm yako waseme uchaguzi unarudiwa kama hujakimbia kulinda kaburi la dhalimu hapo chattle.
 
Magufuli hakujenga system alijiamini yeye kama yeye. Sasa hii ndio shida sasa.
Hata yeye kujiamini kwake kulitokana na inferiority complex aliyekuwa nayo. Watu wenye mapungufu hupenda kujifanya wana uwezo mkubwa na nguvu. Kumbe ni kinyume chake
 
Kiukweli hayati Magufuli aliogopwa yeye binafsi na wala siyo utawala wake kwa sababu kuna maeneo mambo ni vurugu tupu lakini watendaji ni wale wale.

Nimefika Magufuli Bus Terminal utaratibu wa ukataji tiketi na mpangilio wa mabasi ni hovyo kabisa.

Kwenye parking ya mabasi yaani wanapaki hadi barabarani na kuzibiana njia, basi la kuondoka saa 12 asubuhi linaweza kuondoka saa 1:15 kwa sababu tu ya kuzibiwa njia na mabasi mengine.

Mkuu wa mkoa liangalie hili.

Pili kwa sababu parking ina uwezo wa kuchukua mabasi 108 na mabasi yanayotoka asubuhi ni zaidi ya 200 basi yaruhusuni mabasi yanayoanzia Shekilango yasiingie hapo stendi kuu Mbezi.

Eid Mubarak!
Kule juu wanapokata ticket wameka vimeza kama wauza peremende no vyumba kama ile ya dodoma🤣 yaani vurugu tupu
 
Wanadamu na ubinafsi, ili uwabadlishe lazima uwe mwamba kwelikweli

Sasa hivi huko Nyerere atakua anamwambia hata yeye alisalitiwa hivyo hivyo kwenye falsafa ya ujamaa

Gadafi nae anamkumbusha vile yeye alifanya mema sana kwa watu wake tena kwa miaka mingi lakini walimuua

Endelea kupumzika kwa amani kipenzi chetu John Pombe Magufuli, Mwamba, Shujaa na rais wa karne

Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki rais wetu Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote
Hebu peleka puuz huko
 
Kiukweli hayati Magufuli aliogopwa yeye binafsi na wala siyo utawala wake kwa sababu kuna maeneo mambo ni vurugu tupu lakini watendaji ni wale wale.

Nimefika Magufuli Bus Terminal utaratibu wa ukataji tiketi na mpangilio wa mabasi ni hovyo kabisa.

Kwenye parking ya mabasi yaani wanapaki hadi barabarani na kuzibiana njia, basi la kuondoka saa 12 asubuhi linaweza kuondoka saa 1:15 kwa sababu tu ya kuzibiwa njia na mabasi mengine.

Mkuu wa mkoa liangalie hili.

Pili kwa sababu parking ina uwezo wa kuchukua mabasi 108 na mabasi yanayotoka asubuhi ni zaidi ya 200 basi yaruhusuni mabasi yanayoanzia Shekilango yasiingie hapo stendi kuu Mbezi.

Eid Mubarak!
Vipi pale Chato airport, utaratibu ukoje?
 
kiuhalisia ile standa ya mabasi ni ndogo kwa kufananisha na Ubungo terminal....sidhani kama walifanya research na kujua idadi ya mabasi yanayofanya route kwa siku....
 
Bi Samia ana kibarua kigumu mbele yake, inaweza kuchukua karibia miezi 18 kuweza kurudisha Utawala wenye kufuata Sheria na taratibu za Nchi, Magufuli alifanya kazi yeye kama yeye na hakuzingatia maisha ya raia wengine kwa kupuuza au kuzifutilia mbali taratibu za mipango miji.
Na lazima mama akubali lawama itakapobidi kwani sehemu nyingi taratibu zilivunjwa ili mtu mmoja apendwe, sasa ili sheria ndio zisimamie lazima kuna kilio tu kwa watu, mfano hai ni tatizo la wamachinga!!ki ukweli imekuwa kero, na waendesha bajaji mikoani tofauti na dar kutaka kufanya kazi za daladala!!wakati sheria hazisemi hivyo!!lakini wakiambiwa wafuate sheria utasikiaa, baba yetu magufuli tunaanza kunyanyaswa!!!
 
Kila alichoanzisha Magufuli kitafeli tuu!!! Hakuna jinsi hii ni kwa sababu alikua anafanya vitu bila kua na strategy!!! Alitaka sifa tuu!!!
Anzia ndege,
Stendi ya mbezi
Kuanzisha somo la uzalendo nk
Achilia aeapoti ya chati
Inshort atajua kama mobutu angalia picha za kijiji cha mobutuView attachment 1783549
FB_IMG_1620754559781.jpg
View attachment 1783550
 
Katiba mpya iendane na utamaduni wa kuheshimu katiba kinyume na hivyo yawezakuwa ni kazi bure.
Katiba ikiwa nzuri itaheshimika tu, kumbuia watu wanaidharqu katiba kwa kuwa ina mapengo mengi na kwa upande fulani inategemea utashi wa mtu mmoja.
 
Wanadamu na ubinafsi, ili uwabadlishe lazima uwe mwamba kwelikweli

Sasa hivi huko Nyerere atakua anamwambia hata yeye alisalitiwa hivyo hivyo kwenye falsafa ya ujamaa

Gadafi nae anamkumbusha vile yeye alifanya mema sana kwa watu wake tena kwa miaka mingi lakini walimuua

Endelea kupumzika kwa amani kipenzi chetu John Pombe Magufuli, Mwamba, Shujaa na rais wa karne

Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki rais wetu Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote
Sambona hawajabadilika pamoja na umwamba kweli
 
Back
Top Bottom