Kumbe ambao hawajaoa/kuolewa amri ya saba haiwahusu? au Usizini maana yake nini Wajuvi

HOST NOT FOUND

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2023
Posts
1,192
Reaction score
3,486
Nimekuwa nikitafakari kuhusu Amri ya Saba: “USIZINI” (Kutoka 20:14), na hapa ndipo nimekwama kidogo.

Kama kwa maana ya kawaida uzinzi ni mtu aliye kwenye ndoa kufanya tendo la kingono nje ya ndoa, je, hii means vijana ambao hawajaoa/kuolewa hawahusiki kabisa na Amri ya Saba wanapofanya sex?

Kwa mfano, two unmarried people wakifanya tendo la ndoa, Biblia inasema wamezini au wamefanya uasherati? Na kama ni uasherati, kwa nini Amri ya Saba inasema specifically “Usizini” badala ya kusema “Usifanye uasherati”?

Nataka kuelewa hili biblically, not by assumptions. Pia ningependa kujua tofauti halisi kati ya uzinzi, uasherati, zinaa na “adultery/fornication” katika lugha ya Biblia.

Wajuvi wa Biblia na Hebrew/Greek, karibuni mtufafanulie.
Tusibishane kwa hisia; tuangalie context, original meaning na scriptures.
 
Kuzini ni kuingiliana kimwili kati ya mwanamke na mwanaume nje ya sheria na mpango wa Mungu......

Mpango wa Mungu ni kuoa au kuolewa kwanza ndio ufanye hilo tendo nje na hapo ndio inaitwa zinaa.....

Wajuvi watanisahihisha
 
Kwa msingi upi wa kibiblia Mkuu?
Asante mkuu! Kwa mjibu wa
Mathayo 5:28.
Yesu hakuja kutangua torati wala manabii, bali kutimiliza!

Anasema "mmesikia kwamba imenenwa USIZINI lakini mimi nawaambia,
Amtazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha kuzini naye moyoni mwake"

Hapa anamaanisha wanaume wote bila kujali ameoa au hajaoa!
 
Hata wangesema uasherati, ungekuja na uzi kuuliza kuhusu uzinzi.

Pia, soma mizizi saba ya dhambi

Kwa kifupi, fanya mapenzi ukiwa kwenye ndoa. Tofauti na hapo, fanya kwa utashi wako, usitafute mianya kwenye maandiko ya kidini.
 
Kuzini ni kuingiliana kimwili kati ya mwanamke na mwanaume nje ya sheria na mpango wa Mungu......

Mpango wa Mungu ni kuoa au kuolewa kwanza ndio ufanye hilo tendo nje na hapo ndio inaitwa zinaa.....

Wajuvi watanisahihisha
Kwa msingi upi wa kibiblia, Mkuu,? kwamba "Kuzini ni kuingiliana kimwili kati ya mwanamke na mwanaume nje ya sheria na mpango wa Mungu......"
 
Nimekuwa nikitafakari kuhusu Amri ya Saba: “USIZINI” (Kutoka 20:14), na hapa ndipo nimekwama kidogo.

Kama kwa maana ya kawaida uzinzi ni mtu aliye kwenye ndoa kufanya tendo la kingono nje ya ndoa, je, hii means vijana ambao hawajaoa/kuolewa hawahusiki kabisa na Amri ya Saba wanapofanya sex?

Kwa mfano, two unmarried people wakifanya tendo la ndoa, Biblia inasema wamezini au wamefanya uasherati? Na kama ni uasherati, kwa nini Amri ya Saba inasema specifically “Usizini” badala ya kusema “Usifanye uasherati”?

Nataka kuelewa hili biblically, not by assumptions. Pia ningependa kujua tofauti halisi kati ya uzinzi, uasherati, zinaa na “adultery/fornication” katika lugha ya Biblia.

Wajuvi wa Biblia na Hebrew/Greek, karibuni mtufafanulie.
Tusibishane kwa hisia; tuangalie context, original meaning na scriptures.
Kijana, ukisoma Agano la Kale soma pia na Agano Jipya. Yesu anasema katika Mt 5:28:
Kila mtu amtazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.

Kila mtu means any person, awe ameoa au hajaoa, akimtamani tu mwanamke, amezini.

Tafsiri halisi ya uasherati ni mahusiano ya kimwili kwa watu ambao hawajaoana.

So, nionavyo mimi, watu ambao hawajaoa wanafanya dhambi zote mbili kwa mpigo: uzinzi na uasherati, kwa sababu kabla ya kufanya uasherati wanaanza kwanza kutamani. Hapo vipi
 
Hata wangesema uasherati, ungekuja na uzi kuuliza kuhusu uzinzi.

Pia, soma mizizi saba ya dhambi

Kwa kifupi, fanya mapenzi ukiwa kwenye ndoa. Tofauti na hapo, fanya kwa utashi wako, usitafute mianya kwenye maandiko ya kidini.
Sidhani kama nimekuwa natafuta “mianya” kwenye maandiko. Swali langu ni la msingi kabisa, kama Biblia inatenganisha uasherati na uzinzi, kwa nini tusijue tofauti yake na maana ya “Usizini” badala ya kuhitimisha tu kwamba yote ni kitu kimoja?

Na kuhusu “mizizi saba ya dhambi,” hiyo haijibu moja kwa moja swali nililouliza. Nataka msingi wa maandiko unaoonyesha kwamba mtu ambaye hajaoa akifanya tendo la kingono anaitwaje kibiblia, mzinzi au mwasherati?
 
Back
Top Bottom