Kumbe ambao hawajaoa/kuolewa amri ya saba haiwahusu? au Usizini maana yake nini Wajuvi

Kumbe ambao hawajaoa/kuolewa amri ya saba haiwahusu? au Usizini maana yake nini Wajuvi

Tuanze na maana ya kuzini kwanza.
Kuzini ni kufanya tendo la ndoa na mtu ambaye sio mke au mume wako halali, mpaka hapo hii haituhusu ambao bado hatujaoa wakuu 😁
 
Kaz mnayo muwe mnatembea mmetizama chini Ili msitaman mkazn
Mkuu... Kuna kasalamu kawakatoriki kanasema "Akamkazia macho! akampenda" kupenda sio dhambi kwahiyo ni bora umkazie macho umpende na sio kumtamani.
 
Ngono ipo exclusive kwa watu ambao wamefunga ndoa(Tendo la ndoa) ikifanywa na watu ambao hawapo kwenye ndoa ndio huitwa kuzini..

Mtu aliekua kwenye ndoa akichepuka inaitwa Uasherati sio Kuzini kama ulivyosema..

Jiulize why mtu akipata gonjwa la ngono tunasema GONJWA LA ZINAA??
 
Tuanze na maana ya kuzini kwanza.
Kuzini ni kufanya tendo la ndoa na mtu ambaye sio mke au mume wako halali, mpaka hapo hii haituhusu ambao bado hatujaoa wakuu
Asante mkuu! vp kuhusu
Mathayo 5:28...
Yesu anasema amtazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha zini?
 
Kijana, ukisoma Agano la Kale soma pia na Agano Jipya. Yesu anasema katika Mt 5:28:
Kila mtu amtazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.

Kila mtu means any person, awe ameoa au hajaoa, akimtamani tu mwanamke, amezini.

Tafsiri halisi ya uasherati ni mahusiano ya kimwili kwa watu ambao hawajaoana.

So, nionavyo mimi, watu ambao hawajaoa wanafanya dhambi zote mbili kwa mpigo: uzinzi na uasherati, kwa sababu kabla ya kufanya uasherati wanaanza kwanza kutamani. Hapo vipi
Nimekupata Mkuu
 
Asante mkuu! Kwa mjibu wa
Mathayo 5:28.
Yesu hakuja kutangua torati wala manabii, bali kutimiliza!

Anasema "mmesikia kwamba imenenwa USIZINI lakini mimi nawaambia,
Amtazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha kuzini naye moyoni mwake"

Hapa anamaanisha wanaume wote bila kujali ameoa au hajaoa!
Sawa Mkuu, Vipi kwa wanawake inakuaje, usizini inaluwa na maana ile ile kama wanaume na kwa msingi upi wa kibiblia?
 
Kijana, ukisoma Agano la Kale soma pia na Agano Jipya. Yesu anasema katika Mt 5:28:
Kila mtu amtazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.

Kila mtu means any person, awe ameoa au hajaoa, akimtamani tu mwanamke, amezini.

Tafsiri halisi ya uasherati ni mahusiano ya kimwili kwa watu ambao hawajaoana.

So, nionavyo mimi, watu ambao hawajaoa wanafanya dhambi zote mbili kwa mpigo: uzinzi na uasherati, kwa sababu kabla ya kufanya uasherati wanaanza kwanza kutamani. Hapo vipi
Yesu amesema ā€œkila mtu amtazamaye mwanamke kwa kumtamaniā€. Kama ā€œkila mtuā€ hapo unamaanisha wanaume, je wanawake wanaomtazama mwanaume kwa kumtamani hawahesabiki kuwa wamezini moyoni? Au kanuni hiyo inawahusu wote, licha ya Yesu kutumia mfano wa mwanaume kumtazama mwanamke?
 
Sawa Mkuu, Vipi kwa wanawake inakuaje, usizini inaluwa na maana ile ile kama wanaume na kwa msingi upi wa kibiblia?
Kweli mkuu! inawezekana hata wanawake wanatuzoom kwa kututamani... ila nimesoma biblia kwa uzoefu wangu! mwanamke kumtamani mwanaume ni mara chache kuna potifa alimwelewa sana yusuph nadhani inawahusu na wao!
 
Sidhani kama nimekuwa natafuta ā€œmianyaā€ kwenye maandiko. Swali langu ni la msingi kabisa, kama Biblia inatenganisha uasherati na uzinzi, kwa nini tusijue tofauti yake na maana ya ā€œUsiziniā€ badala ya kuhitimisha tu kwamba yote ni kitu kimoja?

Na kuhusu ā€œmizizi saba ya dhambi,ā€ hiyo haijibu moja kwa moja swali nililouliza. Nataka msingi wa maandiko unaoonyesha kwamba mtu ambaye hajaoa akifanya tendo la kingono anaitwaje kibiblia, mzinzi au mwasherati?
Kwa kifupi usifanye tendo la ndoa na mtu ambaye hujafunga naye ndoa. Yani USIZINI na usafanye UASHERATI.

Habari za kutafuta mzinzi ni nani na mwahserati ni nani haina maana.
 
Back
Top Bottom