Kumbe ambao hawajaoa/kuolewa amri ya saba haiwahusu? au Usizini maana yake nini Wajuvi

Tuanze na maana ya kuzini kwanza.
Kuzini ni kufanya tendo la ndoa na mtu ambaye sio mke au mume wako halali, mpaka hapo hii haituhusu ambao bado hatujaoa wakuu 😁
 
Kaz mnayo muwe mnatembea mmetizama chini Ili msitaman mkazn
Mkuu... Kuna kasalamu kawakatoriki kanasema "Akamkazia macho! akampenda" kupenda sio dhambi kwahiyo ni bora umkazie macho umpende na sio kumtamani.
 
Ngono ipo exclusive kwa watu ambao wamefunga ndoa(Tendo la ndoa) ikifanywa na watu ambao hawapo kwenye ndoa ndio huitwa kuzini..

Mtu aliekua kwenye ndoa akichepuka inaitwa Uasherati sio Kuzini kama ulivyosema..

Jiulize why mtu akipata gonjwa la ngono tunasema GONJWA LA ZINAA??
 
Tuanze na maana ya kuzini kwanza.
Kuzini ni kufanya tendo la ndoa na mtu ambaye sio mke au mume wako halali, mpaka hapo hii haituhusu ambao bado hatujaoa wakuu
Asante mkuu! vp kuhusu
Mathayo 5:28...
Yesu anasema amtazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha zini?
 
Nimekupata Mkuu
 
Sawa Mkuu, Vipi kwa wanawake inakuaje, usizini inaluwa na maana ile ile kama wanaume na kwa msingi upi wa kibiblia?
 
Yesu amesema “kila mtu amtazamaye mwanamke kwa kumtamani”. Kama “kila mtu” hapo unamaanisha wanaume, je wanawake wanaomtazama mwanaume kwa kumtamani hawahesabiki kuwa wamezini moyoni? Au kanuni hiyo inawahusu wote, licha ya Yesu kutumia mfano wa mwanaume kumtazama mwanamke?
 
Sawa Mkuu, Vipi kwa wanawake inakuaje, usizini inaluwa na maana ile ile kama wanaume na kwa msingi upi wa kibiblia?
Kweli mkuu! inawezekana hata wanawake wanatuzoom kwa kututamani... ila nimesoma biblia kwa uzoefu wangu! mwanamke kumtamani mwanaume ni mara chache kuna potifa alimwelewa sana yusuph nadhani inawahusu na wao!
 
Kwa kifupi usifanye tendo la ndoa na mtu ambaye hujafunga naye ndoa. Yani USIZINI na usafanye UASHERATI.

Habari za kutafuta mzinzi ni nani na mwahserati ni nani haina maana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…