Kumbe Amina wa Ali Kiba alimshtaki Diamond? Ona alivyojibiwa sasa

Kumbe Amina wa Ali Kiba alimshtaki Diamond? Ona alivyojibiwa sasa

Amina Khalef, mke aliyeachana na mwanamuziki maarufu wa Bongo, Ali Kiba amemchukulia hatua za kisheria mwimbaji Diamond Platnumz katika siku chache zilizopita.
Hii ni kutokana na matamshi ya hivi majuzi ambayo msanii huyo wa 'Zuwena' aliyatoa wakati wa majibizano makali mtandaoni na Alikiba.
Ikumbukwe ugomvi wao ulianza mwishoni mwa Julai, pale Diamond Platnumz alipomponda Ali Kiba akisema kuwa amemshinda katika nyanja zote za muziki, licha ya kumkuta kwenye tasnia ya muziki.



Bosi huyo wa Wasafi aliendelea kudai kuwa mke wa Ali Kiba Amina Khalef anafahamu kauli zake jambo ambalo lilizidisha moto.
"Tatizo unaokaa nao hawakuambii ukweli, wanakudanganya & na ndio maana nimekukuta kwenye muziki na nimekupita na kila kitu, kimauzo, kituzo, kifollowers, subscribers, viewers, listeners, kibei za show, kimaendeleo, kifupi kila kitu...kibebes usiongee maana habari yangu hadi na Amina na unayo..." Diamond Platnumz alisema.
Siku chache tu baada ya Diamond Platnumz kutoa kauli hizo, Amina Khalef leo amefunguka kuwa alimchukulia hatua za kisheria.
Kupitia wakili wake aliomba radhi na kusema kuwa taarifa za Chibu ni za uongo, kwa sababu hakuwahi kuwa na majibizano yoyote naye.
Amina Khalef alizidi kufichua kwamba alitaka aombwe radhi ndani ya siku saba, kwa sababu kauli hizo ziliharibu sifa yake.
"Mteja wetu aliyetajwa hajawahi kuwa na mwingiliano usio wa kitaalamu, usio wa kimaadili, usiofaa na/au wa kutia shaka na wewe kama inavyodaiwa. Kwamba wakati wote amekuwa akijiweka mbali na mizozo yote ya mitandao ya kijamii kati yako na msanii mwingine yeyote sio tu kwa mumewe.
Kwamba licha ya maoni yaliyo hapa juu, umekuwa ukiendeleza uwongo, uwongo na upotoshaji wa kashfa dhidi ya mteja wetu katika majukwaa yako mbalimbali ya mitandao ya kijamii. Kwamba kwenye akaunti yako ya Instagram uliyochapisha, na kusababisha kuchapishwa, na kusambazwa sana maneno yenye nukuu 'Habari yangu na Amina nazani Unayo'...Imetafsiriwa kwa upole kudhania kuwa wewe na mteja wetu mlihusika katika ugomvi usio wa kimaadili na wa kimapenzi" Sehemu ya taarifa hiyo. ya tarehe 10 Agosti kutoka kwa wanasheria kusoma.


Siku chache baada ya Amina Khalef kutaka msamaha kutoka kwa Diamond Platnumz, hatimaye amejibu kupitia mawakili wake pia.

Muimbaji huyo wa kibao cha 'Zuwena' alikataa kuomba msamaha kwa sababu alisema hakuwahi kumdharau malkia huyo kama alivyodai.

Kulingana na Diamond Platnumz, alitaja jina la Amina na sio Amina Khalef kwa ukamilifu.
Kwa hiyo jina Amina linaweza kumaanisha mtu mwingine yeyote na si lazima yeye moja kwa moja.
"Mteja wetu amesikitishwa na yaliyomo kwenye notisi yako ya mahitaji ambayo ina madai mazito na yasiyo na msingi juu ya ukweli wake. Mteja wetu hajawahi kusema popote kuwa na mwingiliano usio wa kitaalamu, usio wa maadili, usiofaa na / au wa tuhuma na mteja wako. Ni sana bahati mbaya barua yako haijaeleza katika extenso ambayo na post inayodaiwa ilimtaja mteja wako anayekwenda kwa jina la AMINA KHALEF" Sehemu ya taarifa hiyo ilisomeka.
"Kama matumizi ya 'Amina' ndio tatizo, je imekuingia akilini, ni watu wangapi kwa jina 'Amina' wanaweza kujitokeza na kudai kuchafuliwa?" Iliongeza.
Diamond Platnumz kupitia mawakili wake pia alisema kuwa kauli zake hazina nia ya kumdhuru Amina Khalef, na kamwe hazikumlenga yeye moja kwa moja.
Ukichunguza vizuri hizi kesi zisizo na tija zinalenga kuwanufaisha mawakili na wanasheria kwa kumlipisha mteja legal fees
 
Hakuna kitu kama hicho
Amina ana kesi nzuri tu kwa sababu kitakachoangaliwa ni probability kwa hiyo Aminas wote wakiwa eliminated, basi sioni kwanini asishinde.
Hata kimtandao alikosea diamond kwa kutaja jina la Amina, ataulizwa ni yupi na kwanini amtaje huyo Amina hata kama siyo mke wake Kiba bali ni mama ntilie anayemjua Kiba.
Why mention her??
 
Amina ana kesi nzuri tu kwa sababu kitakachoangaliwa ni probability kwa hiyo Aminas wote wakiwa eliminated, basi sioni kwanini asishinde.
Hata kimtandao alikosea diamond kwa kutaja jina la Amina, ataulizwa ni yupi na kwanini amtaje huyo Amina hata kama siyo mke wake Kiba bali ni mama ntilie anayemjua Kiba.
Why mention her??
Mkuu amna kesi hapo kwasababu katika bandiko la diamond majina yaliyo tajwa ni MALKIA na AMINA sasa huyo mke wa Ally kiba ata mshitak vipi?
 
Write your reply...hawa wasanii ndo mana wengi wao hufa kwa kupigwa shaba
Una mawazo makubwa sana! Huyu kijana atakuja kuishia kubaya... nimesoma mpaka nimetetemeka kwa hasira utadhani mimi ndo huyo mume wa Amina. Japokuwa hakutaja jina kamili huo ni utoto, Ushari, UPUMBAVU na utovu wa nidhamu wa hali ya juu! Huko anakoelekea siko

Aonywe uropokaji wake utakuja kumponza.. aliuwawa rais wa Marekani bwana JFK, Sembuse yeye 😊
 
Huyu mtoto wa tandale namwona mjinga mmoja hivi akina davido na hela zote hawahangaiki na ujinga wa hivi ndio maana mziki wao na nchi yao unachanja mbuga.
Mshamba sana huyo kijana! Habadilikagi huyo MSENGE! HAKUI!

Anaenda kuishia kubaya asipoangalia... ku-misbehave mpaka kumtukana kienyeji mke wa mwenzako au aliyekuwa mke ni ushari wa hali ya juu!

Na waswahili wamejawa unafiki sana! Eti na yeye ana Cabinet na Board of directors wa kampuni ambao hata hawamshauri na ku-manage tabia yake.

NONSENSE!

HUYO **** NAMTAMANI SANA!
 
Amina ana kesi nzuri tu kwa sababu kitakachoangaliwa ni probability kwa hiyo Aminas wote wakiwa eliminated, basi sioni kwanini asishinde.
Hata kimtandao alikosea diamond kwa kutaja jina la Amina, ataulizwa ni yupi na kwanini amtaje huyo Amina hata kama siyo mke wake Kiba bali ni mama ntilie anayemjua Kiba.
Why mention her??
Kisheria haiko hivyo. Ili Defamation ithibitike ni lazima;

(1) Jina litajwe kwa ukamilifu na siyo kwa kubashiri kwa hisia zako

(2) Maneno yaliyotamkwa au kuandikwa (kuchorwa) yawe yanatweza utu wa mtu

(3) Maneno hayo yawe siyo ya kweli (kama ni ya kweli basi hiyo siyo defamation), na mtu/watu waliohusishwa na hayo maneno/maandishi wawe wamefedheheshwa

(4) Aliyedhalilishwa/waliodhalilishwa wawe wanastahili fidia

Bila hivyo vipengele vyote 4 kuthibitika Mahakamani basi hakuna defamation hapo.

Kama diamond kataja AMINA tu bila ubin wake tayari kipengele kimoja kinakuwa hakijathibitika na inatosha kabisa kutupilia mbali shauri hilo.
 
Mkuu amna kesi hapo kwasababu katika bandiko la diamond majina yaliyo tajwa ni MALKIA na AMINA sasa huyo mke wa Ally kiba ata mshitak vipi?
Jina lake ni Amina na alikuwa mke wa Ali kiba.
Akiwa na mwanasheria mzuri jamaa itabidi amlipe.
Preponderance of probabilities, siyo lazima utaje jina kamili, just by implication Amina mke wa Ali kiba hawezi kuondolewa, kufanya hivyo kutakuwa against any logic.
 
Hapo ndio panaposhangaza, alikua anamtukana mume, baadae akataja jina la mke halafu useme hukumaanisha mke kwan wenye jina hilo wapo wengi.

Utetezi wa kitoto sana, yeye kama kidume kweli aseme ndio wakapambane mahakamani.
Sheria haziendeshwi kwa hisia, nina uhakika nikikuomba unionyeshe ni wapi Mond anathibitika kumtukana Ali Kiba huawezi kunionyesha, maana Alichofanya Diamond ni kuweka maandishi kwenye Insta Story yake bila kumtaja moja kwa moja Alikiba.

Wewe na sisi mashabiki wengine ndio tunajua kuwa yale maneno yalimuendea Ali Kiba, ila sheria itataka tuthibitishe kitu ambacho hatuwezi.

SHERIA HAIJATAWALIA NA KUHISI.

Yani hata ile kuthubutu kufungua kesi kwenye issue kama hiyo, inaonyesha udogo na kutokufikiria kwa hao wanasheria.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom