Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 1,386
- 2,833
๐ง๐พ Kutana na Mwanaume mmoja toka Ufilipino alianzisha Teknolojia ya kipekee yenye kupelekea kuleta vuguvugu la kimataifa baada ya kuleta Mwanga kwenye nyumba yake bila kutumia umeme.
๐พ Kupitia chupa ya plastiki, maji na bleach, chupa hizi muundo wake ziko kama balbu za jua zenye kutoa Mwanga mkali bila kutumia umeme wa kawaida.
โก Kwenye jamii Yetu tunajua umeme ni kitu muhimu, ila uvumbuzi huu umepelekea teknolojia kuzidi kushika Kasi sana baada ya kubadilisha takataka kuwa hazina kwa kuweza kubadilisha chupa kuu za Plastiki kuwa vyanzo endelevu vya kutoa Mwanga.
๐ก chupa huweza kujazwa maji, kuwekwa juani na kuchanganywa na bleach kupachikwa kwenye paa upigwa na Mwanga wa jua upelekea kutoa Mwanga sehemu yenye kiza wakati wa mchana ndani ya nyumba.
๐Ili kuongeza athari hadi usiku, chupa hizi sasa zinaimarishwa kwa taa za LED zinazotumia nishati ya jua, na kutoa mbadala safi na wa bei nafuu kwa taa hatari za mafuta ya taa.
Ugunduzi huu unaweza kupeleka mamilioni ya Watu kuweza kupata Mwanga kwenye nyumba zao bila kutumia Umeme hata Maeneo ambayo umeme haujafika.
Unasemaje Teknolojia hii ikiletwa Tanzania ๐น๐ฟ tuachie maoni yako?
Credit to: #bongotech255
Create an account or log in to Instagram - Share what you're into with the people who get you.
www.instagram.com