๐—ž๐˜‚๐—บ๐—ฏ๐—ฒ ๐—ฐ๐—ต๐˜‚๐—ฝ๐—ฎ ๐˜‡๐—ฎ ๐—ฝ๐—น๐—ฎ๐˜€๐˜๐—ถ๐—ธ๐—ถ ๐˜‡๐—ถ๐—น๐—ถ๐˜‡๐—ผ๐—ท๐—ฎ๐—ฎ ๐—บ๐—ฎ๐—ท๐—ถ ๐˜‡๐—ถ๐—ป๐—ฎ๐˜„๐—ฒ๐˜‡๐—ฎ ๐—ธ๐˜‚๐˜๐—ผ๐—ฎ ๐— ๐˜„๐—ฎ๐—ป๐—ด๐—ฎ ๐—ฏ๐—ถ๐—น๐—ฎ ๐˜‚๐—บ๐—ฒ๐—บ๐—ฒ ๐—บ๐—ฎ๐—ท๐˜‚๐—บ๐—ฏ๐—ฎ๐—ปi

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
1,386
Reaction score
2,833


๐ŸงŽ๐Ÿพ Kutana na Mwanaume mmoja toka Ufilipino alianzisha Teknolojia ya kipekee yenye kupelekea kuleta vuguvugu la kimataifa baada ya kuleta Mwanga kwenye nyumba yake bila kutumia umeme.

๐Ÿพ Kupitia chupa ya plastiki, maji na bleach, chupa hizi muundo wake ziko kama balbu za jua zenye kutoa Mwanga mkali bila kutumia umeme wa kawaida.



โšก Kwenye jamii Yetu tunajua umeme ni kitu muhimu, ila uvumbuzi huu umepelekea teknolojia kuzidi kushika Kasi sana baada ya kubadilisha takataka kuwa hazina kwa kuweza kubadilisha chupa kuu za Plastiki kuwa vyanzo endelevu vya kutoa Mwanga.



๐Ÿ’ก chupa huweza kujazwa maji, kuwekwa juani na kuchanganywa na bleach kupachikwa kwenye paa upigwa na Mwanga wa jua upelekea kutoa Mwanga sehemu yenye kiza wakati wa mchana ndani ya nyumba.



๐Ÿš€Ili kuongeza athari hadi usiku, chupa hizi sasa zinaimarishwa kwa taa za LED zinazotumia nishati ya jua, na kutoa mbadala safi na wa bei nafuu kwa taa hatari za mafuta ya taa.



Ugunduzi huu unaweza kupeleka mamilioni ya Watu kuweza kupata Mwanga kwenye nyumba zao bila kutumia Umeme hata Maeneo ambayo umeme haujafika.

Unasemaje Teknolojia hii ikiletwa Tanzania ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ tuachie maoni yako?

Credit to: #bongotech255

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ