Ila ukiziangalia hizo karanga kwa jicho la kibiashara za level ya kimataifa na kihesabu zinafaida kubwa sana.
Ikiwa kila boksi ni shilingi elfu 20 na ndani ya boksi kuna pakti 100 inamaana pakti atauza shillingi 200 kwa bei ya jumla katika hilo box moja. Ikumbukwe reja reja ndio tunauziwa tsh.300!
Chukulia mfano tu kwa miezi sita akifanikiwa kuuza pakiti million 3 tu pekeyake.
200*3,000,000= 600,000,000 millions.
Hio ni kwa kiwango cha wastani ila anaweza uza pakiti zaidi ya hizo. Anapotoa gharama za malighafi na utengenezaji, packaging, logistics, mishahara na mikataba pamoja na malipo ya kodi za serikali ambazo kwa pamoja zaweza fika labda million 300 at maximum. Still atabaki na faida ya million 300 ambayo sio hela ndogo kuipiga ndani ya miezi 6 kwa biashara moja inayoendelea vyema.
Kwa promotional efforts na influence ya Diamond kama brand name wanayotumia kuna uwezekano zaidi ya hizo units(pakti) kuuzika chini ya miezi 6 na kwa kuwa bei ni affordable kila mtu anaimudu, chukulia wateja ambao wananunua boksi zima pekeyao wanakuwa wamenunua pakti 100 at per wale wa vifuko vya elfu 8 wananunua pakti 40 at per.
Hio biashara inaonekana ya kijinga ila ina hela sana
NB: Kweli nchi yetu fursa bado ni nyingi wanangu, tutumie vichwa vyetu vizuri biashara za chini ya shillingi 500 ndio zenye faida inayopatikana kwa wepesi kuliko biashara za mahela mengi hasa mzunguko wa pesa ukiwa uko chini kama hali ilivyo sasa.