Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Mwanzoni zilipotoka habari za kuwepo mkataba wa bandari kati ya Tanzania na kampuni ya DP World nilifikiri hii ni kampuni ya kijanja janja inayoanza shughuli zake nchini. Baadae ilipokuja hoja ya kuwa ni kampuni ya waarabu nikajua athari ya elimu zitolewazo Tanzania.
Nilipojaribu kuangalia historia na utendaji kazi wa kampuni hiyo nikaono kumbe ni kampuni kubwa sana, iliyoanza kazi miaka kadhaa nyuma na kwamba inaendesha shughuli za bandari katika mabara yote na katika nchi zilizoendelea kama Marekani na ndio wapakiaji wakubwa wa ngano za Ukraine pia zikaifikia dunia nzima kiurahisi.
Ramani na kupanuka kwa shughuli za DP world kila siku zinaongezeka mpaka kufikia nchi hata zisizokuwa na bahari.
Zaidi ni kuwa makao makuu yake yako kwenye nchi ya kiarabu lakini viongozi wake na teknolojia wanazotumia havina sura ya uarabu jambo ambalo ni hoja kubwa ya wapinzani wake.
Kama kuna watu wanaopinga mkataba huu kwa maoni yangu wabadili hoja zao zielekee kwenye marekebisho penye mapungu na si kupinga au kutumia kipengele cha uarabu. Wakifanya hivyo watadharaulika na hawataaminika katika misimamo yao mingine ya kisiasa.
Kwa upande mwengine wakisikilizwa na kuachwa mkataba huu basi watazifanya bandari za Tanzania ziwe kama zilivyokuwa karne iliyopita. Zitakuwa kama bandari za kusubiria samaki na majahazi,Meli za mizigo zitaelekea nchi nyengine.