Kumbe fundi simu anaweza kuingiza laki moja kwa siku?

Kumbe fundi simu anaweza kuingiza laki moja kwa siku?

Optimists

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2021
Posts
379
Reaction score
1,082
Simu yangu ilileta shida kidogo nikaenda kwa fundi simu kunibadilishia system charge yangu ya Google pixel akanipiga 25,000/= nikasema nianze kumuuliza maswali mengi jamaa hakua na hiyana, kwanza alinambia kanunua nyumba ya million 18, kwa mwezi hakosi million moja kama faida, alinambia na kushika Chaki kwangu koote siwezi kumfikia, ninachomzidi mimi ni kukopeshwa na serikali tu😄😄.

Nikaanza kumdadisi jamaa nilivyomuona alikua na vioo vya simu vyoote, vifaa vya simu kama Google pixel, iphone, samsung n.k alikua navyo, lakini kifaa alichokua anatumia kwenye ufundi ni dude flan la kupashia joto simu, pamoja na ammeter.

Vijana wangu mnaomaliza vyuo jikite kwenye ufundi wa vitu kama phone pamoja na laptop radio kila kitu, bei za ufundi unajipangia tu, tena kujifunza nadhani ukiongea na fundi haizidi laki 2, unamaliza na ujuzi pamoja na hela ya kuanzia maisha unakua nayo. Fundi alinambia siku akikosa saana ni 50,000/=

Nawasilisha.
 
Ukiwa na roho ya uchawi hata mama nitilie utamwona anapata pesa na utamwonea wivu mpaka fundi viatu anavyopanga foleni.
Tuangalie totally ya maisha yao in term of percentage. Walimu wako juu ya mafundi simu kwa asilimia nyingi. Acha kutamani maisha ya huyo fundi, unatenda dhambi.
Roho ya uchawi itakufanya mpaka bodaboda umwone anapiga pesa sana kuliko wewe mtumishi wa umma au mfanyabiashara.
Huo ni uchawi
 
Kwa fundi simu mwenye mtaji wa vioo vya simu hata vya mil3 ,na akiwa location nzuri hiyo laki Kwa siku ni kawaida tu,na uzuri wa vioo vile vilivyozingua mzigo unarudishwa kiwandani unapewa mwengine
 
Natafuta fundi simu tufanye kazi, sehemu ya biashara ipo hapa maeneo ya survey opposite na Mlimani city, makubaliano na mambo mengine tutazungumza tukionana. PM kwa information zaidi
Ulishapata bosi mi nipo tayari
 
BIASHARA ZINA SIRI SANA.......ukitajiwa amount anayokunja kwa siku unaweza pagawa., ingia wewe
 
Back
Top Bottom