Naona Wiki hii Vijana wa JamiiForums mmeamka na GENTAMYCINE kwani kwani ndani ya Siku Tatu ( 3 ) Wewe ni Mtu wa pili sasa kunianzishia Uzi. Hata hivyo nichukue tu nafasi hii kuwashukuruni kwani kwa kuzidi Kwenu kumfuatilia GENTAMYCINE kwa kila anachokifanya humu hasa ' Kimaandiko ' na kuja ' Kumjadili ' ni ' Kiashirio ' tosha kwamba hii ' Brand ID ' yangu ni Habari ya Mjini na ama hakika naitendea vyema mno ' Signature ' yangu isemayo Purely Talented, Charismatic Fella, Game Changer and Entertainer. Yaani kila Siku mnavyonijadili humu ndiyo mnazidi kunifanya niwe juu na juu zaidi kiasi kwamba sishangai kila siku napokea tu ' Notifications ' za New Followers na kwa Member wa JamiiForums ambaye nimejiunga tu mwaka 2013 lakini hadi sasa nina ' Followers ' 40 si kitu cha mchezo.
Ahsante sana Mwenyezi Mungu / Allah kwa ' Kunibariki ' na ' Vipawa ' vingi na naomba uzidi ' Kunibariki ' ili niwe juu juu zaidi.
Amen / Inshaallah.