mbenge
JF-Expert Member
- May 15, 2019
- 4,864
- 10,483
Vyovyote vile ambavyo itakuwa, CDM kama chama kikuu cha upinzani itabidi ifanye uchaguzi wa mwaka 2025 ili kirejee katika hadhi yake.Kumbe ni kweli umekuwapo mvutano mkubwa kati ya Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na Makamu wake Tundu Lissu.
Lakini mvutano huo sio ugomvi kama mnavyo aminishwa na wapiga propaganda wa CCM bali ni kuwa hawajakubaliana kitu kimoja na ni kwa manufaa ya chama.
Habari kutoka chanzo cha uhakika cha ndani kabisa ni kuwa Mbowe alitaka kweli kuachia kiti na amekuwa akimshawishi Lissu akubali kugombea nafasi hiyo kuu kabisa katika chama.
Pia soma: Kuelekea 2025 - Wanachama, Viongozi CHADEMA wagawanyika kambi tofauti, hofu ya mpasuko yaongezeka
Lakini majibu ya Lissu ni kuwa yeye anaona Mbowe kwa sasa agombee tena nafasi hiyo na yeye ndio maana alitangaza mapema kutaka kugombea nafasi ya makamu mwenyekiti ili Mbowe aendelee kukiongoza chama kwenye mapambano ya katiba mpya na uchaguzi mkuu wa 2025 mwakani.
Haya malumbano ya maridhiano na Samia ni mkakati wa chama kumprove Samia kuwa aliwadanganya na amastahili aadhibiwe na wananchi.
Subirini muone tamko la chama ndio mtaamini CHADEMA imejaa watu wenye akili.
Mgogoro wa Lissu na Mbowe jiulizeni kwa nini upo kwenye maandiko ya maccm zaidi wakio gozwa na Fake pastor zaidi?
CCM inatuchukulia poa sanq, ndiyo inatuchukulia kihurahisi katika kila aina ya uchaguzi unaofanyika. Ni lazima sasa wajifunze na kuzielewa kanuni zote za uchaguzi kabla ya kufanya uchafuzi wao
Wakati umefika sasa kwa wao kumwaga ugali, nasi tumwage mboga ili heshima iwepo. Ni upuuzi na upumbavu mtu kila siku kulalamuka juu ya matendo yao ya kifedhuli wanayozidi kuyafanya.