Mtoto wa nyoka anaweza kuwa chura? Mwembe unazaa maembe na si mapera!
Bata anaweza kulalia mayai ya kuku na akatotoa kifaranga cha kuku....
Akihojiwa na Clouds FM leo, January aliulizwa kama alimshirikisha baba yake katika azma yake ya kwenda kuomba uteuzi...
Wakati anajibu aliweka sentensi kuwa 'nilimwambia kuwa ...baba naenda kugombea, naomba usiniharibie... maana najua yele Mzee anaweza kwenda kule akazungumza neno, ikawa tena bas, ameshaharibu'..
Naye kumbe mropokaji kama baba yake, kwa nini kaanika udhaifu wa baba yake!
Akihojiwa na Clouds FM leo, January aliulizwa kama alimshirikisha baba yake katika azma yake ya kwenda kuomba uteuzi...
Wakati anajibu aliweka sentensi kuwa 'nilimwambia kuwa ...baba naenda kugombea, naomba usiniharibie... maana najua yele Mzee anaweza kwenda kule akazungumza neno, ikawa tena bas, ameshaharibu'..
Hii kauli mimi naichukulia katika mtazamo tofauti kidogo.
Nadhani ameongea hivyo ili kudhihirisha kuwa hajabebwa na baba yake.
na katika uteuzi wake watu waelewe kuwa hakuna mkono wa baba yake.
Na ndio maana anataka jamii iamini kuwa tangu alivyomwambia baba yake kuwa anaenda kugombea, baba yake alikuwa kimya tu, hakushughulika naye. alimwacha ahangaike yeye mwenyewe.
Ni kauli ya Kisiasa zaidi, Haimaanishi.
UROPOKAJI ni tabia binafsi ya mtu na haiwezi kumpima mtu ufanisi wake wa kiutendaji...kama atahukumiwa kwa kusema alilosema fine but hilo pia ni la kifamilia zaidi sidhani kama chama au wanajamii wanaweza kumhukumu moja kwa moja kwa kumnyima fursa ya kuongoza....anapomwomba baba asimharibie inaweza kutafsiriwa kuwa kwa madaraka ya baba chamani basi anaeza kusema kijana bado hajakomaa au baba akatumia nafasi yake kusema "kijana wangu anagombea" na hiyo ikamharibia katika harakati ukaonekana ni mpango wa baba kurithisha mwana ufalme...mi niliielewa tofauti kabisa na nadhani kuna wengine pia wameelewa hivyo kama hawajahusisha itikadi za kisiasa katika kauli hiyo